Elections 2010 Kura zangu mpeni slaa

Mfamaji

JF-Expert Member
Nov 6, 2007
6,631
1,926
Prof. Lipumba kasema kwenye mdahalo na ITV kuwa kama humpendi yeye kura yake mpe Doctor Slaa.
 
Hiyo watanzania wengi wamesha tambua zaidi kathibitisha tu,asante sana
 
Ni wazi kabisa kuwa kura za Uraisi ni kwa Dr Slaa/CHADEMA. Wafuasi wa CUF na vyama vingine wamekwisha pina hilo nakuona kuwa ili kura zao zilete mabadiliko ambayo watz wengi tunapenda kuyaona wataongeza nguvu kwa upande wa upinzani wenye nguvu. Sote kwa sasa tunafahamu kuwa Dr Slaa wa CHADEMA ndio anakubalika zaidi kwa upande wa Tanzania Bara. Shima watanzania tumeshajaribu kwa miaka 49 ni busara ya kawaida kabisa kufahamu kuwa tunahitaji mabadiliko sasa.
 
Ionee huruma Tanzania, iokoe kutoka kwenye maangamizi ya kizazi cha sasa na kile kijacho kwa kumpigia kura Dr. Slaa. Watanzania tuache ushabiki na tuwe serious ktk mambo ya msingi hususan mustakabali wa taifa letu kwa sasa na siku zijazo. Tumepoteza mambo mengi na kukosa mwelekeo ila tukiamua sasa tunaweza kuona mwanga na kupata mwelekeo. Tujitokeze wote trh 31-Oktoba-2010 na kumwinua Dr. Slaa akamate usukani wa kuliongoza taifa hili
 
Sasa... kama mimi simpendi yeye itakuwaje kura yangu ni yake???

Kwani kuna utata gani hapo? Anawaambia wa CUF hivyo maana kura zote za CUF ni zake. Sio lazima CUF wote wampende. Hii ni kusema kura za Uraisi apewe Doct Slaa na sio yeye maana anajua hatashinda. Usisahau alimpigia debe kwa kusema anamheshimu sana, hamshambulii wala nini.
 
Prof. Lipumba kasema kwenye mdahalo na ITV kuwa kama humpendi yeye kura yake mpe Doctor Slaa
Sina uhakika na hili kwa sababu Prof. Lipumba alijikuza na kujifananisha na mlima Kilimanjaro na huku akimkwaza Dr. Slaa pale alipomwita kichuguu.......Is this really an unequivocal endorsment?

My view is...it is not.
 
Sina uhakika na hili kwa sababu Prof. Lipumba alijikuza na kujifananisha na mlima Kilimanjaro na huku akimkwaza Dr. Slaa pale alipomwita kichuguu.......Is this really an unequivocal endorsment?

My view is...it is not.
I hope siyo yule swahiba kichuguu wa JF
 
Back
Top Bottom