Kura za maoni zitaaminika tena?

Kevin Makyao

New Member
Sep 21, 2010
1
0
Baada ya Mwenyekiti wa Chadema kusema kwamba utafiti wa synnovate unaonyesha kwamba Dr. Slaa anaongoza kwa umaarufu mbele ya JK, na baadae Synnovate kukanusha taarifa hizo, kuna dalili kwamba matokeo yatakayofanywa na taasisi hiyo yanaweza yasiwe ya kuaminika kwa wananchi maana sasa inaonekana siaa imeingilia mambo.
 
Kwani wewe ulishawahi kuhojiwa katika hiyo kamati ili kujua kama kweli kula za maoni ni za kweli au za kutunga?
Mambo yote hadharani hapo oktoba 31,achana na kura za kugushi!
 
Synovate WASIFANYE utafiti wa mambo ya siasa. Kwa kweli WAMEPOTEZA UAMINIFU! Binafsi sina imani nao, na pia, watu wengi wanawaona WANABOA! Wafanye utafiti wa mambo mengine.
 
Hivi hukumsikia Hosea(PCCB) wakati anawahutubia wakuu wa polisi kule Arusha alivyosema?!

Alisema wote wanaofanya utafiti lazima wawapendelee watu wanaowapa funds.

Do the maths...
 
Kitu alichofanya Mbowe kinaitwa "preempting". Yaani unasema kitu ili kumzuia mtu mwingine kufanya jambo usilolitaka. Synnovate hata kama wakitoa huyo utafiti wataonekana wanapika matokeo. Hii ndio siasa.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom