Elections 2010 Kura za maoni ni kaburi la CCM

Luteni

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
2,274
301
Kama kuna kitu ambacho CCM watakuja kukijutia maishani ni kitendo chao cha kubadilisha mtindo wao wa zamani wa kumpata mgombea na kuanzisha mtindo huu mpya wa kura za maoni wakati uchaguzi mkuu ukiwa ukingoni.

Sina maana ya kusema mtindo huu si mzuri la hasha, ila kitendo walichofanya (timing) ni sawa na kumfanyia majaribio mchezaji mpya wakati wa mechi ya mtoano. Ni makosa makubwa (risk) kupima uwezo wa mchezaji wakati mkitafuta nafasi pekee na ya mwisho kwenye ligi, kwa sababu hakutakuwa na nafasi nyingine ya kurekebisha makosa endapo yatatendeka.

Mchakato huu ungefaa sana kama ungeanza kutumika mwaka jana wakati wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa, kwamba, hata kama kungetokea makosa wakati wa upigaji kura yangeweza kufanyiwa marekebisho, na Chama kingekuwa na muda wa kujipanga upya kukabiliana na vitendo hivyo kabla ya uchaguzi mkuu kufanyika.

Binafsi sioni ni kwa jinsi gani kwa kipindi hiki kifupi kilichobaki kabla ya uchaguzi mkuu vikao vya CCM vinaweza kuleta suluhu kwa wanaodhani (wananchi na wagombea) wamedhulumiwa haki yao ya msingi.

Kinachoendelea kwa sasa, chochote kile kitakachoamuliwa na vikao vya CCM, AIDHA kwa kuwaridhisha waliofanyiwa faulo kwa kumpokonya ushindi mgombea aliyeshinda kura za maoni na kuwapa wanayemtaka AU kwa kuweka pamba masikioni na kutosikiliza vilio vyao, Chama kitakuwa kinajichimbia kaburi.

Maana yangu ni kwamba ni vigumu sana kuwaridhisha wanachama wote (wa pande zote) kwa kipindi kifupi kilichobaki, kwa kufanya hivyo lazima tu utaonekana unaegemea upande mmoja. CCM inafanya majaribio wakati wa mechi.
 
Ninachojiuliza mimi CHAMA TAWALA kinawezaje kuwa hivi na bado watu mkakipigia kura kuendelea kutawala? Mwenyekiti wa CCM na RAIS wa JMT atafanya nini baada ya kuyaona haya yakifanywa hadi na MAWAZIRI wake? Vyombo vya DOLA bado mnaing'ang'ania CCM? Tufanyeje jamani!
 
Namini kwa utaratibu wa sasa CCM wako sawa dawa ni kubadili nau kuondoa kasoro zilizojitokeza ,na itawezekana

.....
 
Namini kwa utaratibu wa sasa CCM wako sawa dawa ni kubadili nau kuondoa kasoro zilizojitokeza ,na itawezekana

.....
wataweza kwa kipindi cha mwezi mmoja uliobaki? huo ndio wasiwasi wangu.
 
Ninachojiuliza mimi CHAMA TAWALA kinawezaje kuwa hivi na bado watu mkakipigia kura kuendelea kutawala? Mwenyekiti wa CCM na RAIS wa JMT atafanya nini baada ya kuyaona haya yakifanywa hadi na MAWAZIRI wake? Vyombo vya DOLA bado mnaing'ang'ania CCM? Tufanyeje jamani!

tatizo ninaloliona mimi ni wananchi wapiga kura. Pamoja na ccm kujionyesha uhalisia wake bado wanaweza kukipa kura!!!!! I said it before; Rushwa = mishipa ya damu ya ccm. No Rushwa no ccm. Actually rushwa ni moyo wa ccm, ukisimama kufanya kazi ndiyo mwisho wa ccm.
 
amakweli mwaka huu ccm wamejianika hadharani jinsi walivyo wataalamu wa faulo..michezo michafu...rushwa...wel done hii ndo silaha yetu wabanchi wameona
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom