KURA ZA MAONI: CCM yazidi kupanda chati, CHADEMA ya pili

Kura za maoni zilioendeshwa hivi karibuni kupitia vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini, zinaonyesha kuwa CCM inazidi kupanda chati huku CHADEMA ikishika nafasi ya pili.

Hata hivyo kwa upande wa wanasiasa mmoja mmoja, imeonekana kuwa Rais Kikwete anaongoza maeneo ya vijijini, wakati Mh. Zitto Kabwe na Mh. Halima Mdee wanakubalika sana maeneo ya mijini, haswa haswa miongoni mwa kada ya vijana bila kujali itikadi za vyama vyao vya siasa.

Waziri Mkuu Pinda 'mtoto wa mkulima' ameporomoka kwa asilimia kumi na mbili (12%), na kupishana kwa karibu sana na Mh. Magufuli.

Miongoni mwa wabunge, aliyeongoza ni Mh. Pindi Chana, akifuatiwa kwa karibu na waheshimiwa Anne Kilango wa CCM, na Kafulila wa NCCR-Mageuzi.

Source: Tanzania Rainbow Syndicate (TRS).

Wee ! mbona ueleweki huo utafiti unaendelea wapi ? aacha kuwajaza ujinga watu, umaarufu wa Kikwete kijijini kuongezeka vijiji vya wapi hivyo ? au vijiji vya bagamoyo ? huyo hakubaliki mjini na vijijini, badala ya maisha bora kwenye slogan yake kwa kila mtanzania imekuwa maisha bora kwa familia yake mwenyewe
 
tubadilikeni sasa mambo ya msingi yanaachwa hawo mawakala wa ccm wanataka tuhamishe mawazo kwenye mambo ya msingi kama umeme,mafuta inflation nk,tujadili ujinga.watanzania wa leo ni tofauti tunatafakuri
 
Back
Top Bottom