Kura yako ilihesabiwa?

Jobo

JF-Expert Member
May 15, 2008
586
43
Leo nimekaa nikiwaza nchi yangu inapoenda, nikaamua kujiuliza kama kweli tuna viongozi wenye nia ya kutuongoza na kutufikisha katika neema ya angalau milo mitatu kwa siku! Nimeshindwa kuelewa ni kwa sababu zipi kila siku inabidi mtu uondoke nyumbani saa kumi alfajiri ili kuwahi kazini na ukifika huko kazi zenyewe hazileti tija bali ni kukaa, kusoma magazeti ya udaku na kujaribu kuganga njaa kwa kutafuta semina na mikutano ili angalau uambulie posho itakayopelekea familia yako ipate mlo kwani mshahara hautoshi hata kidogo. Ni nchi ambayo hata zinaponyesha mvua umeme ni wa mgao na bei ya mafuta na gesi haishikiki! Nikajiuliza kama kweli Watanzania ambao kila siku ndugu zao wanauwawa na askari polisi, majambazi na ajali za barabarani bila kujali mabomu ya kijeshi wanaweza kuwapatia kura viongozi ambao aghalabu hawajali hali zao bali matumbo yao na ya vimada wao! Ndiyo maana nakuuliza, hivi kweli kura yako ilihesabika Desemba mwaka jana? Nipeni jibu labda akili yangu itatulia kidogo!
 
Hata mtu ungeruhusiwa kupiga mara3 kwa mtu1 bado NEC isingeruhusu kura zako kubadilisha matokeo,kimsingi kura zetu hazikuhesabiwa,kura ziliwekwa kando wakatoa walichokikusudia wao na ndo maana mpaka leo NEC imeshindwa kutoa jumla ya matokeo ya kura zetu...it was like voting for leisure,the cursed nec!
 
Hata mtu ungeruhusiwa kupiga mara3 kwa mtu1 bado NEC isingeruhusu kura zako kubadilisha matokeo,kimsingi kura zetu hazikuhesabiwa,kura ziliwekwa kando wakatoa walichokikusudia wao na ndo maana mpaka leo NEC imeshindwa kutoa jumla ya matokeo ya kura zetu...it was like voting for leisure,the cursed nec!

Sad isnt it? Na watanzania wamekaa kimya kama vile kilichotangazwa ni halali! Siku zote huwa najiuliza, hivi mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi hana kikomo? Kuna jamaa aliniambia kuwa wakati wa uchaguzi Katibu na Mwenyekiti wa Tume walikuwa wamemaliza muda wao! Hivyo uwepo wao ulikuwa batili na yamkini walibakizwa kwa shughuli ya kuchakachua
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom