Kura ya Maoni: Je, unaiamini Taarifa ya Kova Kuhusiana na Mkenya wa Dr Ulimboka?

Je, unaiamini taarifa ya Kova kuhusu mkenya aliyekamatwa?

  • Ndio

    Votes: 1 1.2%
  • Hapana

    Votes: 83 98.8%

  • Total voters
    84
Huu mchezo wa polisi kuwa wanasiasa utatufikisha pabaya. Tupige kura kuwaonyesha kama kweli sehemu hii muhimu ya watanzania inaiamini taarifa ya kova au la.

tengeneza ukurasa wa kupigia kura! Kura za kutokuiamini hiyo report naamini zitafika 99.9% Ritz pekee ndiye atapiga upande ule mwingine.
Nasubiri ukurasa.
tafadhali, Mods, Invisible help!!!!!!
 
Last edited by a moderator:
Katika hali ya kawaida wange-retrive numba za simu zilizowasilaiana na Ulimboka mpaka anatekwa wangeshamkamata mtu aliyetengeneza huu mkakati lakini kwa makusudi kabisa wameamua kufanya mambo ya kihuni ili kuwahadaa watanzania. Hakuna kitu hapo hayo ni maigizo tu.
 
ni Ritz na Kupeng'e ndo watavote kuiamini japo hawaiamini
 
Binafsi sishangai, maana maigizo kama haya TZ mbona nimesha yazoea.SIRI TUNASEMA ....BAYANA TUNAFICHA
 
Sina imani maana ripoti yenyewe ni kama uwendawazimu fulani. Tangu lini watekaji wasifahamiane wao kwa wao na kwa wametumwa na mtu wasiyemfahamu??? Ripoti gani hiyo kama siyo ukichaa. Mtanzania anayekubali ripoti hii ni sawa na kusema hana akili timamu pia! I am sorry, Pasco, Ritz
 
haina chembechembe hata moja ya ukwel kikwete na serikal yake watambue kwamba maovu,dhuluma,ubabe,chuki,kiburi kinapozid kwenye jamii ajue kwamba ukomboz umekaribia.
 
ahmed.png
 
Back
Top Bottom