Kura ya kutokuwa na Imani na Waziri Mkuu ni kura dhidi ya Rais na Chama tawala!

DO! Inaonekana kweli hujanielewa, kama ambavyo na mimi sijakuelewa. Mimi nina maanisha kuwa kilichotamukwa katika ibara ya 52 ni kazi za kufanywa na PM siyo madaraka ya kuzitekeleza. Nikaongeza kusema kuwa ktk kutekeleza kazi zake PM anategemea huruma ya RAIS, kwani RAIS ndiye mwenye mamlaka juu ya watu ambao PM anapaswa kuwasimamia ili kutekeleza kazi za serikali: WATU HAO (1) wanateuliwa na RAIS, na (2) kama ni swala la kuwajibika, wanawajibika kwa RAIS siyo kwa PM. Sasa kama hakuna kitu cha maana kinafanywa na serikali mimi ninaami kuwa wakushughulikia, muundo huu wa kwetu ambapo RAIS ndiye mwenye mamlaka, ni RAIS siyo PM.


UNASEMA SOKOINE alifanya makubwa, ni kwa sababu moja, RAIS mwenye mamlaka alikubali SOKOINE atumie mamlaka yake. KAMA NYERERE angekatalia mamlaka yake basi, SOKOINE naye angekuwa mtu wa kucheza MAKIDAMAKIDA. PM wetu anafanya kazi kwa mtindo wa kushitaki, that is a fact, yaani kama kuna mtu anamuona anatenda visivyo anachoweza kufanya ni kumshtaki kwa RAIS. SASA Rais kama atakuwa mtu wa kuchukua hatua, PM ataonekana anafanya kazi, vinginevyo, ndo mambo yanakuwa kama tunavyoyaona sasa...
.

Eeeh naona mbwilambwila tu mkuu tizama red unakubalina na kisha unakataa kitu kile kile mkuu hata maandishi ya katiba kuyasoma nayo shida mkuu,manake katiba hiko wazi unasema kilichotamkwa kwenye katiba ni kazi za Waziri Mkuu na sio madaraka!!!

Du unanishangaza yani hata pasipo aibu nawe unamwagika tu waaaaaaah ebu nakuwekea tena maelekezo ya katiba vifungu na ibara zake bado usomi unakurupuka haya narudia tena kukopia ibara hiyo yako ya 52 omba wakusaidie kusoma inasema nini nimetumia rangi ya blue kuweka msisitizo mkuu!!!

Kazi na mamlaka ya Waziri Mkuu Sheria ya 1984 Na.15 ib.9
52.-(1)
Waziri Mkuu atakuwa na madaraka juu ya udhibiti, usimamiaji, utekelezaji wa siku hata siku wa kazi na shughuli za Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
(2) Waziri Mkuu atakuwa Kiongozi wa Shughuli za Serikali Bungeni.
(3) Katika
utekelezaji wa madaraka yake, Waziri Mkuu atatekeleza au kusababisha utekelezaji wa jambo lolote au mambo yoyote ambayo Rais ataagiza kwamba yatekelezwe.

Haya tetete tuone huo mbuyu unaozunguka nao kama sio woga!!!Labda mwenzetu katiba unayosoma wewe ni ya mwaka upi?,manake mimi natumia e-electronic ya mwaka 1977 chapisho la mwaka 2005.

NB:
Umetumia neno madaraka ambayo kwa tafsiri ya kamusi ya Kiswahili Kiingereza maana yake
Madaraka nm [ya-] responsibility, power, control:

Katiba imetumia maneno yote mamlaka na madaraka:Hivyo imejitosheleza kwenye hilo unalopingana nalo.
Mamlaka nm [ya-] authority, jurisdiction, mandate.

Maneno hayo madaraka [Responsibility] na mamlaka [Authority] kwa tafsiri ya kiingereza ni kama ifuatavyo:
Responsibility=Madaraka:
1: If you have responsibility for something or someone, or if they are your responsibility, it is your job or duty to deal with them and to take decisions relating to them.
2: If you accept responsibility for something that has happened, you agree that you were to blame for it or you caused it.
3: Your responsibilities are the duties that you have because of your job or position.
4: If someone is given responsibility, they are given the right or opportunity to make important decisions or to take action without having to get permission from anyone else.
5: If you think that you have a responsibility/duty to do something, you feel that you ought to do it because it is morally right to do it.
6: If you think that you have a responsibility to someone, you feel that it is your duty to take action that will protect their interests.

Authority=Mamlaka:
1: The authorities are the people who have the power to make decisions and to make sure that laws are obeyed.
2: An authority is an official organization or government department that has the power to make decisions.
3: Authority is the right to command and control other people.
4: If someone has authority, they have a quality which makes other people take notice of what they say.
5: Authority is official permission to do something./Authorization.
6: Someone who is an authority on a particular subject knows a lot about it.
7: If you say you have it on good authority that something is true, you mean that you believe it is true because you trust the person who told you about it.

Jipange upya au ndio hivyo contradictory unashindwa kupambanua!!!
 
Wakubwa wa nchi wanachotaka ni AUTHORITY na POWER sio RESPONSIBILITY na ACCOUNTABILITY. Waziri Mkuu wetu hana authority wala power. Kumwambia ajiuzulu au awe accountable kwa makosa ya mawaziri wenzake ni kumwonea sana tu. Yeye WM tumtake ajiuzulu pengine kwa kuwa TAMISEMI iko chini ya ofisi yake na ina madudu mengi mno.
 
Wakubwa wa nchi wanachotaka ni AUTHORITY na POWER sio RESPONSIBILITY na ACCOUNTABILITY. Waziri Mkuu wetu hana authority wala power. Kumwambia ajiuzulu au awe accountable kwa makosa ya mawaziri wenzake ni kumwonea sana tu. Yeye WM tumtake ajiuzulu pengine kwa kuwa TAMISEMI iko chini ya ofisi yake na ina madudu mengi mno.


Mkuu WildCard hii hapa chini nini jamani mbona tunazungumza mambo tuliyonayo mikononi jamani,nashindwa kujua ulikuwa unamaanisha nini HANA au ANA.Kwa kuwa unasema HANA ukimaanisha HAKUPEWA nguvu hiyo ya kikatiba na sheria,eb tizama hapo chini hiyo ni kwa mujibu wa sheria na katiba ya Taifa lako.Hivyo kusema HANA ni kuwa ukusoma katiba na hata thread hii ukusoma pia kujua.

Kazi na mamlaka ya Waziri Mkuu Sheria ya 1984 Na.15 ib.9
52.-(1)
Waziri Mkuu atakuwa na madaraka juu ya udhibiti, usimamiaji, utekelezaji wa siku hata siku wa kazi na shughuli za Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
(2) Waziri Mkuu atakuwa Kiongozi wa Shughuli za Serikali Bungeni.
(3) Katika
utekelezaji wa madaraka yake, Waziri Mkuu atatekeleza au kusababisha utekelezaji wa jambo lolote au mambo yoyote ambayo Rais ataagiza kwamba yatekelezwe
 
Back
Top Bottom