Kuporwa Adam Malima, Watu Wasiokuwa na Hatia Bado Wanashikiliwa na Polisi

Muke Ya Muzungu

JF-Expert Member
Jun 17, 2009
3,444
264
Humu Tanznaia tumezoea kuwaona masikini wakinyanyaswa kwa mambo ambayo hayaeleweki huku Mafisadi wakubwa ndio wanalindwa na dola. Namuomba Adam Malima awaangalie hawa vijana na huyu mwanamke WALIVYOPIGWA, ajiulize moyoni kama kweli walimwibia.

Uislamu unatufundisha haki, ukristo nao vilevile...........Zaidi ya yote, huu ni mwezi mtukufu...... Ndugu yangu Adam, hawa raia wema ambao hawakuusika na wizi wa mali zako bado wanasumbuliwa sana na polisi, tunakuomba uwaonee huruma. waambie polisi wawaachie huru. hawana hatia kamwe.Naomba uangalie hizi picha kwa umakini, ukiona ukweli ndani yake naomba ukwel ukuguse moyoni mwako kwani sote dunia ni mapito yetu ila hakuna sababu ya kuwapa watu wasio na hatia mateso.

Wewe na serikali yako mmekuwa watawala waonevu. Mungu Akupe Nguvu. Wasamee kama kweli walikuibia, kama hawakukuibia basi uwaangalie usoni na maumivu wanayoyapata na wanayoendelea kuyapata kisha uwaombe radhi Amina................!!!!

Huu ni mwezi wa TOBA !
IMG_7297.jpg

IMG_7300.jpg

malima11.jpg
 
Ill-trained policemen kazi yao ni kupiga suspects tu. Kaz zingine laana kwel kwel.
 
Usikute yule changu yupo mtaani anapeta ama kweli nimekumbuka wimbo wa Inspector " wanaokwenda jela sio wote wana hatia wengine wanakwenda kwa kesi za kusingiziwa"
Mhusika atoe order hawa watu waachiwe tuu!
 
Shukrani Lumato kwa kuleta hii taarifa. Nimekuwa najiuliza sana kuhusu hatma ya 'wahanga' wa utalii wa Adam Malima. Nimetumia neno 'wahanga' kwa sababu naamini watu waliokamatwa hawahusiki kabisa na mkasa wa Adam, na ni jambo la kuhuzunisha sana kumuona Adam Malima anavaa kanzu kila Ijumaa huku akijuwa fika watanzania hawa wanasumbulia bila ya hatia.
 
Hela kawaachia mahawara zake, wakukamatwa ni wengine... Mungu amwone.... asisahau kuwa malipo ni hapa hapa duniani.. Mbinguni ni hesabu tu.. ipo siku...yaja siku hiyo ambapo uovu wote wa mwanadamu utafunuliwa na kuadhibiwa...
 
Nilitumia muda jana jioni kuangalia majumuisho ya Wizara ya Elimu yaliyofanywa na Dr. Shukuru Kwanmbwa. Nilichokiona kwenye TV ndio kimenifanya nijiulize maswali juu ya Adam Malima na vigezo vilivyotumika kumzawadia Ubunge na Uwaziri.

Yaani wakati Dr. Kawambwa anaongea yeye yuko row ya nyuma naye anapiga story tena kwa sauti kubwa na anamchosha mpaka anayeongea naye na kuamia kweye column nyingine yaani mradi apige to hadithi. Na jana haikuwa mara ya kwanza bali karibia siku zote anakuwa hivyo.

Haya yanatokea wakati kuna Watanzania wenzetu wanaumia kwa upuuzi wa watu kama hawa na magenge yao.

Serikali iwahukumu hawa vijana au iwape haki yao ya kuwaachia huru kwa maana suala lao liko wazi!
 
Hakuna kazi ya ki.pumba.vu kama upolisi,badala ya kufanya kazi kama sheria inavyotaka we unakuwa mtumwa wa wanaume wenzako na kutesa maskini wenzako kwa amri za matumbo yaliyojaa maziwa na mayai. Inauma kusikia mwana ndoa alilala na mchangudoa wakamuibia alafu kuficha kashfa kaenda kushika vijana maskini wakiwa kwenye mihangaiko yao. Hii laana.
 
Unashangaa nini? Hujui bongo mawaziri ni miungu? Aliyekuwa waziri wa nishati na madini bwana Ngeleja alifanya zengwe hadi mlinzi wa Ultimate security akafukuzwa kazi. Kisa, ATM machine
 
Usikute yule changu yupo mtaani anapeta ama kweli nimekumbuka wimbo wa Inspector " wanaokwenda jela sio wote wana hatia wengine wanakwenda kwa kesi za kusingiziwa"
Mhusika atoe order hawa watu waachiwe tuu!

Chechela segedansi nondo geleza inside ndete lupango kunapoteketeza wanaokwenda jela sio wote watuhumiwaaaaa!!
 
Shukrani Lumato kwa kuleta hii taarifa. Nimekuwa najiuliza sana kuhusu hatma ya 'wahanga' wa utalii wa Adam Malima. Nimetumia neno 'wahanga' kwa sababu naamini watu waliokamatwa hawahusiki kabisa na mkasa wa Adam, na ni jambo la kuhuzunisha sana kumuona Adam Malima anavaa kanzu kila Ijumaa huku akijuwa fika watanzania hawa wanasumbulia bila ya hatia.

Huyu Adam malima hana uislam wowote ni ubishoo tu na kuvuta bangi; kama ni muislam wa kweli huu mwezi wa TOBA atahakikisha kuwa hawa jamaa waliobambikiwa kesi wanaachiwa huru kwani changu wake aliomuibia yeye mwenyewe anamjua!!
 
mbona unaanza kunishawishi mkuu!!
 
Back
Top Bottom