Mbu
JF-Expert Member
- Jan 11, 2007
- 12,753
- 7,844
- Thread starter
- #21
Mbu..nataka kubadili msimamo wangu wa awali kuwa wazazi wasilaumiwe.
Kama tunazungumzia ndoa..kwenye ndoa si kuna kiongozi? Tena kiongozi huyu hapigiwi kura wala nini.Uongozi wake ukiwa bora basi tunatarajia familia/ndoa yake itakuwa na mafanikio na hata matatizo yatakuwa yale ya kawaida kabisa ya kibinadamu.
Tatizo ni kuwa wengi wa hawa viongozi wamekithiri kwa uongozi mbovu, ufisadi, ubabe, kukosa mwelekeo, kutokuwajibika, kutokuwa na uwazi, kutokuwa na ukweli na uadilifu.Matokeo yake ni kukosa mwelekeo familia nzima.MAADILI YAKIKOSEKANA KATIKA FAMILIA ambapo watoto wanaona wazazi wanavyoishi kwa ubabe, visa,ukatili,utovu wa adabu na nidhamu, vitendo vya ukengeufu wa maadili usitarajie nao wakikuwa watakuwa wanandoa bora.
...pheeeeeeewwww, WoS kwa mtizamo huo unamlaumu Baba mwenye nyumba ama?...
Nilidhani jukumu la malezi kwa watoto ni la baba na mama. Halafu una habari watoto (naturally) wanajifunza/kufuata yale wanayoelekezwa na mama zao kuliko baba? Hii haswa inatokea tangu mtoto kuzaliwa mpaka umri wa baleghe/kuvunja ungo.
Ndio kusema Mama ana influence kubwa kwenye 'foundation' ya maadili ya mtoto kuliko baba. By the time huyo kijana/binti amefikia kwenye 'teens', jamii inayomzunguka, i.e walimu, wanafunzi wenzake, majirani, ndugu jamaa na marafiki ndio wanaochangia tabia nyingine mpya.
Hapo ndio mara nyingi utaona baba mtu anaingilia kati kusimamia nidhamu, kwani kina mama wengi wakati huo utawasikia..."..muonye mwanao, mie ananishinda!"...
Kibaya zaidi unakuta mwanamke na mwanaume wanakutana ukubwani kila mtu na background tofauti kwa maana ya kwamba mwingine kalelewa kwa maadili na upendo wa hali ya juu wa wazazi na hakujua kabisa tabia chafu za kukosa maadili.Anakutana na mwenzake aliyelelewa kwenye malezi mabovu ambapo wazazi hawana maadili.Sasa niambie hiyo ndoa itakuwa ya namna gani? Most likely yule aliyetoka kwenye background mbovu atakuja na vitabia vyake vibaya kwenye ndoa na kumkwaza yule aliyekuja na maadili mema- uchafuzi tu!
...Bado nataka kuamini mama mwenye maadili mema huko alikotokea hata kama mumewe atakuwa 'mkware' vipi, heshima na adabu vitaendelea kuwepo nyumbani kwao. Kishindo ni pale huyo mama ni 'manjilinji' tangu asili yake (alishindikana kwao), na mume hakieleweki,...!