Membensamba
Senior Member
- Nov 4, 2010
- 157
- 10
Hivi karibuni nimesikia kuwa baadhi ya wabunge wa CCM waliopita bila kupingwa walitumia mbinu ya kuwanunua wagombea wa upinzani ili wajiengue katika hatua ya mwisho kwa lengo la wao kubakia kama wabunge waliopita bila kupingwa. Vile vile nimesikia kuwa hata baadhi ya wabunge wengine walioshindwa ubunge walikuwa awali wameshinda, lakini wakarubuniwa wakauza ushindi wao kwa wabunge wa CCM. Nachelea kutoa mifano nisije nikawapa baadhi ya watu ugonjwa wa mshtuko wa moyo.
Kama hili ni kweli, basi Tz, tumeingia mahali pa hatari kubwa. Kuuza demokrasia au kujaribu kuinunua ni kosa kuu kuliko uhaini kwa mtazamo wangu.
WanaJF, naomba niambieni, kwanza hili ninyi mmelisikia? Ni kweli? Kama ni kweli, mnadhani nini kifanyike kuzuia hali hii? Kumbukeni kama ni kweli, basi nafasi za uongozi katika chaguzi zijazo, na hata Uspika wa bunge zitanunuliwa na hawa mafisadi ambao kwao mamilioni ni vijisenti tu.