macho_mdiliko
JF-Expert Member
- Mar 10, 2008
- 21,791
- 39,584
soma hapa kwa kirefuNdugu zangu wana JF, naomba kuelemishwa ni nin hatima ya mbunge anayepita bila kupingwa hapa nchini. Nafahamu kuwa, kila chama kina mchakato wake wa kuteua mgombea wa ubunge wa jimbo, hii ikiwa ni pamoja na kuitisha kura za maoni, na baadaye kuchakachua matokeo na kumpitisha aliyeshinda au yule ambaye chama kiinampenda (si lazima awe mshindi). Sasa, pale inapotokea huyo mshindi wa chama kimoja anakuwa ndiye mgombea pekee, baada ya vyama vingine kupata mgombea au wagombea waliojitokeza na kupita kuamua kujitoa kwa njia yoyote ile, au wagombea kuwekewa pingamizi na kutolewa; ni nini hatima ya huyu mtarajiwa aliyepita bila kupingwa na hivyo hakuna uhakika kama anapendwa jimboni mwake:
(1) JAnaweza kuteuliwa kuwa waziri?
(2) Anaweza kuteuliwa kuwa waziri mkuu?
(3) Je anaweza kugombea Uspika?
Naomba nisilaumiwe, bali nielimishwe!! Huwezi jua, inawezekana tuko wengi tu tusioelewa suala hilli!! Nawasilisha.
https://www.jamiiforums.com/uchaguz...-mwenyekiti-wa-tume-ya-taifa-ya-uchaguzi.html