Kupingana kwa Wapinzani Maendeleo TZ ndoto

Sakijoli

Member
Oct 4, 2010
71
7
Uchaguzi ulipomalizika na matokeo kutangazwa wapendamaendeleo wote tulipata hamasa baada ya kuona hatua kubwa iliyopigwa na vyama vya upinzani kwa kuweza kufumbua macho ya Watanzania mjini na vijiji, bara na visiwani.

Cha kushangaza ni kwamba baada ya kuingia bungeni hawa tunaodhania kuwa ni wakombozi wetu (UPINZANI) waliotupa matumaini mapya kwa kuwa na idadi kubwa bungeni tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma, WANATENGENEZA UPINZANI WA KUPINGANA WAPINZANI. Mfano mzuri tazama matokeo ya spika na kura alizopata mwakilishi wa upinzani aliyegombea. Au kuwepo na makundi mawili ya upinzani (Majority opposition & Minority Opposition)

Ndugu zangu wapinzani hatutaki kujutia kupigia kura upinzani, lakini kwa dalili hizi za mwanzoni mtakuja kusababisha kutowaamini tena.
 
Hivi maana ya upinzani mdogo ni nini? Inaonekanna hawaelewi wanachokifanya.Chama tawala kinachekelea ambacho tangu mwanzo hakina dhamira ya kuwa na upinzani nchi hii kinafurahia sana; hapa kuna divide and rule! Je hakuna sheria kuwa Bungeni kunakuwa na pande ngapi si tawala na upinzani?
 
Back
Top Bottom