Kupinga wagombea huru, ni uamuzi wa "Kipumbavu"

Serikali haijui kitu kinaitwa contingency plan.Nililifikiria hili hata kabla ya kulisikia kutoka mdomoni mwa Mwanakijiji, nilivyomsikia Mwanakijiji katumia maneno hayohayo nikaona we are on the same page.

Mwanakijiji kambana vizuri sana kwa mifano ya Nguza.

Hapa either waahirishe uchaguzi, au wakubali mgombea binafsi.Mahakama ikishaamua kwamba kuanzia sasa mgombea binafsi ruksa, maana yake huwezi kuweka uchaguzi bila mgombea binafsi.

Ukiitishwa uchaguzi bila ya mgombea binafsi, CCM wanajiweka katika position ya watu baadaye kukata rufaa, halafu mashauri yarudi mahakamani kule kule.

Kifupi Marmo kaonekana kapwaya, kachoka, hana jipya zaidi ya kutumia ubabe wa kiserikali tu. Mwanakijiji ameonekana kuwa informed and engaging.

CCM wanahaha.
 
Marmo haeleweki! Anadai anaheshimu uamuzi wa Mahakama, lakini Mahakama ilipotoa umamuzi kwamba RUFAA SIO AUTOMATIC STAY kwa maana kwamba uamuzi wa mwaka 2006 wa Mahakama Kuu uko pale pale, anadai kuwa Mwanasheria Mkuu na yeye AMETOA UFAFANUZI. Sasa chombo cha mwisho cha utoaji haki ni MWANASHERIA MKUU au ni MAHAKAMA? Uanasheria wa Phillip Marmo [LL.M (Legislative Drafting)] sina imani nao tena. I am so disappointed in Him!
 
Marmo haeleweki! Anadai anaheshimu uamuzi wa Mahakama, lakini Mahakama ilipotoa umamuzi kwamba RUFAA SIO AUTOMATIC STAY kwa maana kwamba uamuzi wa mwaka 2006 wa Mahakama Kuu uko pale pale, anadai kuwa Mwanasheria Mkuu na yeye AMETOA UFAFANUZI. Sasa chombo cha mwisho cha utoaji haki ni MWANASHERIA MKUU au ni MAHAKAMA? Uanasheria wa Phillip Marmo [LL.M (Legislative Drafting)] imani nao tena. I am so disappointed in Him!

Yaani jamaa anajichanganya left, right and center.Maraa siwezi kuongelea hili swala kwa sababu liko mahakamani, wakatai huo huo analiongele.

Halafu anaonekana kutoelewa - au kujitia kutoelewa- maana ya rufaa.Ukikata rufaa unataka kutengua maamuzi yaliyopitishwa na mahakama, haina maana kuwa kukata rufaa tu kunatosha kutengua au ku suspend maamuzi ya mahakama.

Kama wanasheria wenyewe ndio hawa sishangai tuna mikataba mibovu.

Halafu Marmo hajui kujieleza. Swala la mgombea binafsi ana li belittle kama "ni dogo sana". Hili swala linahusika kabisa na civil/ human rights za watu yeye analiita dogo?
 
Halafu Marmo hajui kujieleza. Swala la mgombea binafsi ana li belittle kama "ni dogo sana". Hili swala linahusika kabisa na civil/ human rights za watu yeye analiita dogo?

Hili suala lingekuwa dogo Serikali ingesubiri hukumu ya Mahakama ya Rufaa kupinga uamuzi wa Jaji Lugakingira (1993?) wa kuruhusu mgombea binafsi, lakini badala yake, hata kabla ya kusikiliza wananchi wanasemaje wakaimbilia Bungeni kubadilisha Katiba. Mwaka 2006 Mahakama Kuu ilipobadilisha vifungu vile vile vya Katiba wanaanza kudai eti Bunge halina uwezo wa kubadili Katiba! Ikumbukwe kwamba Katiba ilibadilishwa wakati Rufaa ikiwa pending, kwa hiyo mabadiliko hayo ni questionable! Kwa ujumla tuache utani, Serikali haitaki mgombea binafsi! Hizi mbwembwe za Marmo ni danganya toto tu!
 
Nafikiri hapa suala si kubadilisha katiba suala ni kuilinda CCM na mpasuko uliopo. Wanajua fika kuwa mfumo wa sasa unaotaka wagombea wawekwe na Chama ni mfumo unaoimarisha uwepo wa CCM zaidi. Kwani wanajua kuwa mtu akifukuzwa kwenye Chama au kujitoa basi anapoteza na nafasi yake ya Ubunge na hilo linawasaidia kuwatisha wabunge makini wanaotetea maslahi ya Taifa badala ya CCM.

Ukweli ni kwamba CCM kama Chama wanaogopa sana mgombea binafsi kuliko hata vyama vya upinzani. Ila wajue kuwa wanapong'ang'ania msimamo wao huo wanavunja katiba ya nchi kwani imeweka wazi kuwa "Kila mtanzania mwenye umri wa miaka 18 au zaidi na akili timamu anayo haki ya kuchagua kiongozi au kuchaguliwa kuwa kiongozi kwa mujibu wa sheria za nchi"- Hii ni part ya katiba ambayo mpaka leo ipo kichwani mwangu toka enzi zile za elimu ya siasa mashuleni. Ni matarajio yangu kuwa hawajabadili maana kama Marmo anavyosema kubadili katiba ni mchakato mrefu sana, na katika umri huu wote sijawahi kusikia mchakato wowote mrefu uliwahi kufanyika wa kubadili katiba. Ila nina jua kuwa haya yafuatayo yamewahi kufanyika bila ya huo mchakato mrefu

1. Kutoka katika mfumo wa Chama kimoja kwenda vyama vingi, Japo white paper ilisema 20% ndiyo wanataka vyama vingi ila walikubaliwa matakwa yao kwa mujibu wa tume ya Nyalali.

2. Kutoa muundo wa makamu wa kwanza na wa pili wa raisi wa Jamhuri.

3. Kuongeza mikoa na wilaya za nchi, kuongeza majimbo ya uchaguzi n.k

4. Muswada wa kumpunguzia rais madaraka ambayo yapo katika katiba, umepita very simple.

Philip Marmo na Genge lake la wanaojiita Serikali hawana hoja katika kuzuia mgombea binafsi zaidi ya ubabe wa kuilinza CCM. Ila Mvua huwa haizuiwi kunyesha japo unaweza kuikimbiza kwa kukata miti kuwe na jangwa lakini siku ikifika itanyesha tu. Kwani hata jangwani hata mvua hunyesha pia.
 
Exuper Kachenje

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), Philip Marmo amesema kuwa kutekeleza suala la mgombea binafsi litawezekana tu endapo uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu utaahirishwa.

Akizungumza na gazeti hili jana, Marmo alisisitiza kuwa ugumu wa kutekelezwa kwa suala hilo unatokana na muda mfupi uliopo kati ya sasa na uchaguzi mkuu ujao iwapo mahakama itatoa hukumu kama ile ya awali kabla ya Oktoba.

Waziri Marmo alisema hayo jana katika mahojiano na gazeti hili kwamba, suala la mgombea binafsi linahitaji muda wa kutosha ili liweze kuingizwa kwenye sheria na taratibu za nchi.

"..Ninachosema mchakato wa kubadili katiba ni mrefu na muda uliopo sasa hautatosha. Jambo hilo la mgombea binafsi litawezekana tu iwapo itatokea uchaguzi ukaahirishwa," alisema Marmo.

Alisema kuwa kimsingi mbali na uwezo wa kutoa uamuzi wa kuruhusu kuwepo kwa mgombea binafsi, mahakama haina uwezo wa kufanya mabadiliko ya sheria ili kuwezesha suala hilo.

"Mahakama haina uwezo wa kufanya mabadiliko ya sheria, uamuzi wake kwa mujibu wa taratibu zilizopo, hata ikiamua kuwepo kwa suala hilo basi, kimsingi lazima upitie kwenye mchakato wa kuutekeleza ambao ni kubadili katiba," alisema Marmo.

Marmo ambaye pia ni Mbunge wa Mbulu, mkoani Manyara alifafanua kuwa hata ikiwa uamuzi huo utatolewa na mahakama, lazima suala hilo lipitie katika mchakato ambao ni kubadili katiba ya nchi, taratibu na sheria za uchaguzi.

Waziri Marmo alisema kutokana na hali hiyo ni wazi kuwa mchakato huo unahitaji muda mrefu na maandalizi ili kuwezesha mabadiliko hayo kufanyika.

"Haitoshi mahakama kutoa uamuzi, lazima uamuzi wake upitie kwenye mchakato, nao ni mabadiliko ya katiba, yanahitaji muda mrefu mchakato wake kukamilika," alisema waziri huyo wa serikali ya awamu nne.

Alisisitiza akisema: "Mgombea binafsi ni suala la kikatiba na kwa mujibu wa utaratibu siyo tu mahakama ikiamua inatekelezwa mara moja, katika hilo lazima mchakato wa kubadili katiba ufanyike nalo linahitaji muda mrefu. Kwa sasa hilo la mgombea binafsi kuwezekana labda uchaguzi mkuu uahirishwe."

Hivi jopo la majaji wa Mahakama ya Rufaa nchini wakiongozwa na Jaji Mkuu, Augustine Ramadhani waliamua kwamba hukumu iliyotolewa na Mahakama Kuu ya kuruhusu mgombea huru ndiyo inayotambuliwa wakati wa uchaguzi mkuu wa Oktoba hadi hapo itakapoamuliwa vinginevyo.

Mahakama Kuu iliruhusu mgombea binafsi baada ya mwenyekiti wa chama cha siasa cha DP, Mchungaji Christopher Mtikila kufungua kesi akidai kuwa sheria za nchi kuhusu haki ya kupiga kura na kupigiwa kura inapingana na katiba ya nchi kutokana na kutamka kuwa mgombea ni lazima apitishwe na chama.

Lakini tangu hukumu hiyo ilipotolewa mwezi Juni, 2006 ikitaka mchakato wa kutunga sheria ya kuruhusu mgombea binafsi ufanyike katika kipindi cha miezi sita, hakuna kilichofanyika na badala yake serikali ilikata rufaa ikipinga mamlaka ya Mahakama Kuu kutafsiri katiba.

Rufaa hiyo ilitarajiwa kusikilizwa jana mbele ya jopo la majaji hao saba wa Mahakama ya Rufaa, lakini serikali iliomba suala hilo liahirishwe kwa muda wa miezi minne ili ijipange kikamilifu.

Akiwasilisha maombi hayo, Naibu Mwanasheria Mkuu (DAG), George Masaju alisema sababu za maombi yao ni kutokuwepo kwa wakili mwenza anayeshirikiana naye ambaye anaifahamu vizuri kesi hiyo na ambaye anauguliwa na mgonjwa.
Alidai kuwa yeye (DAG) hakupata muda wa kuipitia orodha ya kesi zitakazotumiwa na upande wa utetezi kwa kuwa walichelewa kuipata, akidai kuwa waliipata Jumamosi ambayo ni siku ya mapumziko.

“Mheshimiwa Jaji, kama utaridhia naomba shauri hili liahirishwe ili tupate muda wa kuzipitia hoja za upande wa pili ili tuweze kuisaidia mahakama kwa kuwa tuliwapelekea wenzetu List of ‘Authorities’ (orodha ya kesi za rejea wakati wa usikilizwaji kesi husika) Ijumaa na wenzetu walituletea list of authorities zao Jumamosi,” alisema Masaju. Maelezo hayo yalionekana kumshangaza Jaji Ramadhani na akamuuliza maswali mengi kutokana na kitendo cha serikali ambayo ni mrufani kuchelewa kupeleka orodha hiyo ili nao wapewe orodha ya upande wa pili mapema wakati suala hilo lilikuwa likijulikana kwa muda mrefu.
 
Kazi nzuri kwa mahojiano na ubunifu wa kaka yetu M. Mwanakijiji. Hata hivyo, hata siku moja sijaridhisha na juhuzi za serikali kujaribu kubana hadi hukumu iliyotolewa isitekelezwe. Kwa mfano, serikali ilikuwa wapi kuandaa rufaa yake mapema tu baada ya hukumu? Mbona wamesubiri mwaka wa uchaguzi mkuu uliolengwa na hukumu iliyotolewa mwaka 2006, ndiyo kasi ya rufaa yao ikawa kubwa? Kwa nini isingefanyika 2006, 2007, 2008 ama mapema 2009?
Katika maelezo ya mahakama wakati inaongeza muda wa serikali kupeleka rufaa, ilisema - as it stands now mgombea binafsi anaruhusiwa kwani hakuna maamuzi tofauti yaliyokwisha tolewa tangu mahakama iseme wagombea binafsi wanaruhusiwa.
Inabidi mtu anayetaka kugombea kibnafsi muda ukifika akachukue form na Tume ya uchaguzi ikimnyima apeleke suala hilo mahakamani, akiishtaki tume kwa kumnyima haki yake ya kikatiba na kuitaka mahakama isimamishe uchaguzi hadi atakapopewa form. Vinginevyo tutafika mahali watasema - mliomba form mkanyimwa (mlijitokeza kugombea mkakataliwa?)
 
Nilichoelewa toka kwake ni kuwa;
  1. Serikali ya JK hawayathamini, hawayaogopi na wala hawayaheshimu maamuzi ya Mahakama
  2. Watafanya uchaguzi kwa jinsi wanavyotaka wao
Serikali inafanya/itafanya hivyo kutokana na udhaifu wa mahakama. Ikumbukwe kuwa baada ya uchaguzi jaji ndiye huwapisha rais na rais hawezi kuingia madarakani bila kuapishwa. Kwa nini basi majaji wasikatae kumwapisha rais ambaye serikali yake haiheshimu wala haiko tayari kutekeleza maamuzi ya mahakama?
 
Nafikiri hapa suala si kubadilisha katiba suala ni kuilinda CCM na mpasuko uliopo. Wanajua fika kuwa mfumo wa sasa unaotaka wagombea wawekwe na Chama ni mfumo unaoimarisha uwepo wa CCM zaidi. Kwani wanajua kuwa mtu akifukuzwa kwenye Chama au kujitoa basi anapoteza na nafasi yake ya Ubunge na hilo linawasaidia kuwatisha wabunge makini wanaotetea maslahi ya Taifa badala ya CCM.

Ukweli ni kwamba CCM kama Chama wanaogopa sana mgombea binafsi kuliko hata vyama vya upinzani. Ila wajue kuwa wanapong'ang'ania msimamo wao huo wanavunja katiba ya nchi kwani imeweka wazi kuwa "Kila mtanzania mwenye umri wa miaka 18 au zaidi na akili timamu anayo haki ya kuchagua kiongozi au kuchaguliwa kuwa kiongozi kwa mujibu wa sheria za nchi"- Hii ni part ya katiba ambayo mpaka leo ipo kichwani mwangu toka enzi zile za elimu ya siasa mashuleni. Ni matarajio yangu kuwa hawajabadili maana kama Marmo anavyosema kubadili katiba ni mchakato mrefu sana, na katika umri huu wote sijawahi kusikia mchakato wowote mrefu uliwahi kufanyika wa kubadili katiba. Ila nina jua kuwa haya yafuatayo yamewahi kufanyika bila ya huo mchakato mrefu

1. Kutoka katika mfumo wa Chama kimoja kwenda vyama vingi, Japo white paper ilisema 20% ndiyo wanataka vyama vingi ila walikubaliwa matakwa yao kwa mujibu wa tume ya Nyalali.

2. Kutoa muundo wa makamu wa kwanza na wa pili wa raisi wa Jamhuri.

3. Kuongeza mikoa na wilaya za nchi, kuongeza majimbo ya uchaguzi n.k

4. Muswada wa kumpunguzia rais madaraka ambayo yapo katika katiba, umepita very simple.

Philip Marmo na Genge lake la wanaojiita Serikali hawana hoja katika kuzuia mgombea binafsi zaidi ya ubabe wa kuilinza CCM. Ila Mvua huwa haizuiwi kunyesha japo unaweza kuikimbiza kwa kukata miti kuwe na jangwa lakini siku ikifika itanyesha tu. Kwani hata jangwani hata mvua hunyesha pia.

Hata ya kufuta mgombea binafsi haikuwa na mchakato mrefu - haikupelekwa kwa wananchi. Kama ni kupeleka kwa wananchi basi isiwe viraka vya katiba bali itungwe katiba mpya ambayo pamoja na mambo yanayozungumzwa sana, itamke yafuatayo:
-Wizara na idadi yake,
-wabunge wasiwe mawaziri (akiwa waziri ajiuzuru ubunge)
- wabunge wafanyabiashara waache biashara kama vile mfanyakazi anavyosimaa kazi (Katiba iunde chombo cha kusimamia biashara zao)
-Wananchi ndiyo wenye maamuzi ya mwisho katika jambo lolote na sio rais
-Hakuna aliye juu ya sheria - hata rais akifanya makosa kama mtu binafsi ashtakiwe (mfano Mkapa alipotumia urais wake kujipatia kibinafsi mgodi wa kiwira)
 
Lakini mara zote walipobadilisha Katiba hakuna wakati waliona umuhimu wa kuja kuwauliza wananchi. Iweje leo ndio waone umuhimu huo?
 
Lakini mara zote walipobadilisha Katiba hakuna wakati waliona umuhimu wa kuja kuwauliza wananchi. Iweje leo ndio waone umuhimu huo?
Ukiona waziri anaongea ameshika mikono, kama Marmo alivyo kwenye hiyo picha ya hapo juu, muangalie mara mbili mbili. Amekaa kama anamsujudia mungu kumbe Ni usanii mtupu unaoendelea.Anajaribu kuonyesha kwamba lile analolisema ni jambo zito kweli kweli. Hivi kuna jambo zito kama kuheshimu utawala wa haki na sheria? Yeye Marmo nguvu za kupinga mahakama mbona hajaomba ridhaa ya wananchi amejiamulia tu! Huku ndo kuzeeka vibaya tunakosema.
Watu wa aina yake sio wa kutulia maana hata kidogo. Time will come when the rubish they have made will be flushed out of the system.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom