Kupinga wagombea huru, ni uamuzi wa "Kipumbavu"

Hivi nani anasomaga haya maandiko ya Mwanakijiji.....nani anamuda wa kusoma haya?

Kwa taarifa yako, siku ya jumatano Tz Daima hugombaniwa kama njugu, kisa makala moto moto zikiwemo za Mkijiji!

Kwa kifupi ni kwamba husomwa sana, na zinapendwa mno kuliko unavo dhani, Upekee wake ni jinsi anavo anza habari zake na kuzileta kama simulizi.. humvuta msomaji hadi mwisho akivutiwa kuendelea kujua kulikoni? Lakini pia jinsi anavo mkoma nyani giledi live live!
 
Ukitaka kujua nguvu ya wananchi wapi inahitajika.....ni katika jambo kama hili......hivyo basi kazi kwetu kuwaamsha wananchi, tuwaelimishe kuwa ni wajibu wao na haki yao kuhakikisha "wanakula ile kitu wao wanapenda"....na sio kulazimishwa kuchagua CCM/CUF/CHADEMA........etc
 
basi seriikali ndiyo mpumbavu! kwani ndiyo iliyofanya uamuzi huo. Naomba radhi kwa mtu yeyote ambaye anadhania kuwa yeye ni sehemu ya serikali iliyofanya uamuzi wa kipumbavu. Ningesema kuwa na maoni ya kupinga ugombea binafsi ni upumbavu basi ningekuwa nimemtukana mtu mwenye maoni hayo.

Hii lugha ninaifahamu vizuri, na nikitaka kusema kitu ambacho nataka kumaanisha sina tatizo hilo. Labda tatizo langu ni kuwa baadhi ya wasomaji wangu wanasoma zaidi ya nilichoandika na kuniwekea maneno kinywani.

Nachagua maneno ninayotumia vizuri sana kama Mwalimu.

Kwikwikwikwikwiiiii.......
 
Mimi huyasoma, tena wakati mwingine zaidi ya mara moja. Unasemaje Nyani Ngabu

Taratibu jamani mnapowagusa pabaya basi muwapulizie kidogo kwani na wao wanakiona mbali, ingawa Mwalimu alisemea upumbafu huo lakini waliamua wawe hivyo mpaka leo bila kujali kwa nini?
 
...basi seriikali ndiyo mpumbavu! kwani ndiyo iliyofanya uamuzi huo. Naomba radhi kwa mtu yeyote....

Nilijua wewe ni better kuliko Nyerere inapokuja kwenye Demokrasia na uwazi wa mawazo. Nyerere asingekuja kujadili vitu openly hapa na kuvumilia kubanana mbavu kiume.

Kuanzia leo ninakuheshimu kwa taadhima kuu.

Only with unambiguous disclaimer. Kwamba tutaendelea kuwa na wide open mind isiyo tetea tetea arguments au figures fulani bila ku appreciate other possible interpretations of events, arguments and facts.

Nashukuru sana.
 
Nilijua wewe ni better kuliko Nyerere inapokuja kwenye Demokrasia na uwazi wa mawazo. Nyerere asingekuja kujadili vitu openly hapa na kuvumilia kubanana mbavu kiume.

Kuanzia leo ninakuheshimu kwa taadhima kuu.

Only with unambiguous disclaimer. Kwamba tutaendelea kuwa na wide open mind isiyo tetea tetea arguments au figures fulani bila ku appreciate other possible interpretations of events, arguments and facts.

Nashukuru sana.

It has been a pleasure...!
 
kupinga wagombea huru ni kudidimiza demokrasia. wananchi wa karatu walishathibitisha hili hata kabla ya uhuru. demokrasia ni kama bustani ya mboga. inapandwa, inapaliliwa na inamwagiliwa maji pale mvua zinapokosekana! vile vile inapuliziwa dawa kuua wadudu waharibifu (CCM). kuna sababu nyingi za kisiasa ambazo zilitolewa tanzania kupinga wagombea huru sababu ambazo ni mwendawazimu tu anayeweza kuzitoa!

tunapopima maendeleo ya demokrasia katika tanzania (trends) kuanzia 'uhuru ' hadi sasa basi angalau tuone kuna improvement in the quality of democracy. hii ya kupinga wagombea huru ni kurudi nyuma! mfumo wa sasa wa vyama vingi nao umeonyesha kasoro kubwa katika utekelezaji wake. wanasiasa wamevuruga mfumo huo kama jinsi inavyojidhihirisha katika bunge letu la 'ndio mzee' ( sikubaliani na maelezo ya waziri lakini naunga hoja mia kwa mia ). kama huu sio ufisadi ni nini? halafu tumeona jinsi utaratibu ulivyowekwa kudhibiti hoja binafsi...hii ikiwa ni katika kuhakikisha kwamba chama kinawafunga kabali wabunge wake kisawasawa.

kwa hiyo sambamba na hili la wagombea huru, ni lazima bunge lipitie na kufanya marekebisho ya kanuni zake ili kuondoa vikwazo vilivyopo kwa watoa hoja binafsi na si hilo tu kuwakomboa wabunge wetu kutoka makucha ya nidhamu ya woga ambayo inawadhalilisha wabunge wetu na kuliingizia taifa hasara ya mabilioni na kurudisha nyuma maendeleo. you see it is all tied in the quality of our democracy!
 
Mzee Mwanakijiji nimekuwa naheshimu sana hoja zako ambazo umekuwa unazitoa siku zote zimekuwa za msingi. lakini hapa mmmhh

Pamoja na kueleza kuwa unaifahamu sana hii lugha nikweli lakini waswahili husema kuwa ulimi hauna mfupa kutamka neno mpumbavu kwa kweli siyo kauli nzuri ,Na kukubali kukosolewa ni uungwana wala siyo ujinga kwa sababu nilizosema hapo juu kwamba ulimi hauna mfupa
 
Mzee mwanakijiji,
Bila samahani mkuu tuendelee kuelimishana.. Mkuu ni muhimu sana tuelewe kitu gani tunazungumzia hapa na sio kuvuta haki pale zisipostahiri...na vizuri sana tukielewa madaraka ya Diwani kama mwanasiasa...Kumbuka tu kwamba diwani, mbunge na rais ni mwakilishi wa wananchi iwe hata kundi dogo hivyo ni muhimu kutanguliza unawalisha nani kabla hujatazama haki ya mtu asiyewakilisha Watu..Hiyo haki itakuja tu baada kutambua kisheria haki za watu anaowawakilisha na sio jinsi watu mnavyoitazama haki hii.
Watu wote humu tungependa sana hili neno siasa na hawa Piliticians wasiongoze nchi lipatikane jina jingine ama hata kurudi kwa Watemi Ma chief wetu lakini pia huko kuna taratibu zake ambazo hazikubaliki leo na ndio haswa sababu ya kuwepo muundo wa demokrasia.
Huwezi kutaka haki ya Kutangaza dini wakati wewe mwenyewe hufahamu unaamini na kuabudu kitu gani! Vile vile huwezi kuongoza misa ya sala kanisani kama wewe sii muumini ya dini na pengine utahitaji kwanza kukubaliwa na chombo cha kanisa hilo kama unaweza kuongoza misa hiyo hata kama wananchi wanazipenda sana longolongo zako huko mtaani..
Hivyo hutuwezi kufanya maamuzi kwa sababu ya jinsi tunavyoitaka haki ya mtu mmoja.

Pengine itafika muda haki hii ya wagombea binafsi inaweza kusimamishwa lakini kwa sasa hivi nadhani tutazidi kujichanganya zaidi. Tanzania tuna matatizo mengi mazito ambayo hayahitaji kuvurugwa akili zetu wananchi..Ufisadi wenyewe umesha tuchanganya akili tunapoona mafisadi wakipokelewa kwa shangwe na vifijo huko makwao, kesho wakachukue Udiwani na Ubunge kuzidi kutuchezea akili. At least ndani ya vyama unayo nafasi na kutazama nani wa kumyooshea kidole!

Binafsi nimechoka na hawa wagombea ambao kila siku huja na upuuzi wa kuwajaza wananchi Utajiri, kesho tutaona hata waganga wa kienyeji na wachawi wakigombea Udiwani kuwajaza wananchi ujinga wa utajiri kwani hakuna haja tena ya biblia na msahafu..
Ndugu yangu nchi yetu maskini na kila mnapoitaka haki inayohusiana na jasho (kodi) za wananchi ni muhimu sana kuwepo na taratibu zinazotambulika na kukubalika. Na kama kuna mtu anafikiria anataka kufungua kanisa lake basi ni lazima kusajili kanisa hilo na ktk kusajiri kuna vipengele ambavyo vinaweza kukubali usajili huo ama kukataliwa ili mradi dini hiyo haipotoshi wananchi..Kisha kitakacho tambulika ni chombo yaani kanisa na sio kiongozi huyo kuwa dhamana ya dini ama dhehebu lenyewe. kwa hiyo kisheria inakuwa rahisi kuweza kutenganisha kanisa na Mhusika panapotokea swala la kisheria. Huamini dini yoyote why bother kutafuta Uongozi..

Mgombea binafsi mimi namwona kama ni mtu asiye abudu Mungu na anataka kuingia uongozi kuongoza waumini bila kitabu cheke kitakatifu. hata wagombea binafsi tunaowaona nchi za magharibi wana mrengo wao na huwezi kuamini kabisa kwamba Ulaya unaweza kumkuta mgombea binafsi akipigania haki za Wasenge, Mazingira na hata wengine haki ya Utaifa against wahamiaji..Kwa hiyo hawa huenda na mkoba wao wa imani kusajili imani hiyo na kuorodhesha Ki/viongozi wake, na pindi wanapokataliwa ndipo haki ya kundi ama watu hawa kisiasa hutazamwama na wanasheria, sio mtu mmoja kalala jana kawazia Utajiri akaona mwanya akajiandikisha Udiwani basi ni haki yake kugombea.Huyu mtu anawakilisha watu gani?.. ama kundi gani hatujui!, hivyo ni haki ya mtu mmoja tu hapa inazungumziwa.
Kwa kutazama mbali (upeo mkubwa) naogopa ikija fikia mtu kuruhusiwa kunadi anachofikiria yeyey kama vile haki ya Wakerewe kujitenga na Mwanza au Tanzania na akapewa support ya mahakama kwa sababu huyu mgombea binafsi hafungwi na sheria za usajili wa vyama...We have to be very careful na hizi haki!
Mkuu tunapo kubali na kuipokea Demokrasia ambayo inatafsirika tu kwa kuwepo Vyama zaidi ya kimoja ktk kugombea kuongoza nchi na sio kuwepo kwa Wagombea -WATU tofauti.. Demokrasia ya vyama ndio msingi wa amani na haki ya wananchi kuchagua mfumo wa Kiutawala na sio sura za watu hivyo muhimu na lazima tukubali taratibu zinazoambatana na ujio wa demokrasia.
Binafsi nazidi kusimama pale pale kuwa kanisa hili halitambui haki ya ndoa za wasenge pamoja na kwamba wao na wengine wengi mnaona ni haki yao. Na kama kweli wanautaka Usenege huo wajitokeze hadharani watoke ndani ya makabati yao na kusherehekea usenge bila aibu kwani hawa wagombea binafsi wote wanaotaka sana sheria hii wamejificha ndani ya vyama vyetu..
Na nadiriki kusema kama kweli Salim, Warioba, na hao wengine wote wanaojificha ndani ya chama cha CCM hali wao wanapingana sana na itikadi za chama hicho basi hawa ni wananfiki.. Watoke CCM watangaze sera zao kama ni Usenge ijulikane mapema na wapo kina Antii watakaojiunga kudai haki za wasenge. Sikubaliani na kiongozi yeyote ambaye hana vision ama mrengo wa kile anachokipigania iwe Diwani, Mbunge au rais wote hawa ni Wanasiasa hivyo ni lazima wawe wazi kwa wananchi wote bila kuogopa..hizi nafasi watu wamezifanya sehemu za AJIRA badala ya kuwa wawakilishi wa wananchi..wanachotanguliza ni matumbo yao.
Nadhani mkuu nimejieleza vya kutosha, CCM washinde wasishinde hiyo rufaa lakini binafsi nipoo nao kwa hili pengine tunachotofautina ni sababu za kutokubali wagombea binafsi.
 
Mzee Mkandara nimekusoma vizuri.

Zipo haki za aina nyingi lakini katika hili nitatofautisha haki mbili ambazo ni za msingi nazo ni haki za binadamu na haki za raia.

Haki za binadamu

Haki za binadamu ni haki ambazo mwanadamu yeyote yule anazo na anazo kwa sababu moja tu, ni mwanadamu. Haki ya kwanza ya mwanadamu ni haki ya kuishi. Haki ya pili ni haki ya kujitapatia maisha yake hifadhi na usalama. Na nyingine ni haki ya kujipatia mahitaji yake yatakayomwezesha kuishi. Sasa karibu mataifa yote yanatambua haki za binadamu na mataifa hayo yameridhia mkataba wa Kimataifa na wanatambua kile kinachoitwa Azimio la Umoja wa Mataifa Juu ya Haki za Binadamu. Unaweza kusoma Azimio hilo HAPA

Sasa ukiangalia haki ambazo zinatambuliwa (haziundwi au kuwekwa na Umoja wa Mataifa) ni pamoja na:

Article 20.

(1) Everyone has the right to freedom of peaceful assembly and association.

(2) No one may be compelled to belong to an association.


Article 21.

(1) Everyone has the right to take part in the government of his country, directly or through freely chosen representatives.

(2) Everyone has the right of equal access to public service in his country.

(3) The will of the people shall be the basis of the authority of government; this will shall be expressed in periodic and genuine elections which shall be by universal and equal suffrage and shall be held by secret vote or by equivalent free voting procedures.

Sasa hizo ni haki za binadamu.

b. Haki za Raia.

Hata hivyo zipo haki za raia ambazo mara nyingi zinatokana na haki za binadamu. Lakini hizi ni haki ambazo zinatambuliwa na nchi fulani kwa raia wake. Kwamba ukiwa raia wa Tanzania una haki hizi na hizi na zile. Sasa hizi haki za raia ni haki ambazo huwezi kumfanya mgeni aziifurahie nazo. Miongoni mwa haki hizo ni pamoja na haki ya kupiga kura, kupata ajira, kuchagua kiongozi wake, n.k n.k Sasa haki za raia huwezi kumpa raia mmoja halafu ukamnyima mwingine. Ukitoa haki fulani kwa raia mmoja ni lazima raia mwingine naye awe na access ile ile.

Haki ya kuchagua unayetaka akuongoze:

Sasa haki ya kumchagua mtu unayetaka akuongoze ni haki ya kila raia na tumesema ataweza kutumia haki hiyo akiwa na miaka 18, na akili timamu na ambaye ndani ya muda fulani hakuwa mtu aliyekutwa na hatia ya kosa kubwa. Mtu mwenye kutimiza masharti hiyo basi anaweza kushiriki katika uchaguzi wa kumchagua, diwani, mbunge, Rais, n.k n.k Hivyo huwezi kusema upande huu wa Tanzania nyinyi mnaweza kumchagua mkiwa na miaka 18 halafu upande ule wa TAnzania wao waanze kupiga kura wakiwa na miaka 16. Raia wote wana haki sawa.

Haki ya kuchaguliwa kuongoza.

Katika hili tunasema kuwa raia wote wenye kutimiza masharti fulani basi wana haki ya kuchaguliwa kuongoza. Katika nchi yetu tumeweka mipaka; kwa upande wa wabunge tumesema kila raia mwenye akili timamu, na ambaye ametimiza miaka 18 na hajashtakiwa uhalifu ana haki ya kuchaguliwa kuongoza. Kwa upande wa Rais tumeongeza awe na angalau miaka 40 na awe hajachaguliwa Rais vipindi viwili huko nyuma.

Lakini kwa namna ya kushangaza tukasema lakini mtu huyo lazima awe mwanachama wa chama cha kisiasa. Hapo ndipo penye tatizo.

Ibara ya 20 (2) ya UDHR niliyoweeka hapo juu inasema mtu yeyote hatoshurutishwa kujiunga na chama chochote kile. Sasa kwa kusema anayetaka kugombea uongozi "lazima" awe mwanachama wa chama cha siasa tunavunja hiyo ibara. Kinachosemwa hapo ni kama kusema "mtu hatoingia kanisani hadi awe ni muumini wa parokia fulani" au kusema "mtu hatoingia msikitini hadi awe muumini wa msikiti fulani". Ukifanya hivyo ina maana unamlazimisha mtu ambaye hataki kuwa muumini katika msikiti wowote ule ajiunge na msikiti ili aweze kuingia msikiti mwingine.

Inakuwaje kama mtu anamuamini Mnyezi Mungu na Mtume wake na anataka aende kuswali anakopenda bila kuulizwa anatoka msikiti gani? Itakuwaje kama mtu anataka kwenye kusali Jumapili tu na anaamini Biblia nk lakini hataki kuwa chini ya mchungaji yoyote?

Sasa tatizo hili siyo la hiyo Ibara ya Umoja wa Mataifa tu bali pia tunaliona kwenye Katiba yetu kwani Katiba yetu na yenyewe inapigisha mwangwi kipengele hicho hicho. Inasema hivi: Ibara 20(4)

Bila ya kuathiri sheria za nchi zinazohusika ni marufuku
kwa mtu yeyote kulazimishwa kujiunga na chama chochote au
shirika lolote,

Sasa, ninachojengea hoja ni kanuni ya haki na sijagusia hata kidogo jinsi haki hiyo inavyoweza kufanya kazi katika Tanzania. On principle, serikali haina uwezo wa kufuta haki ya mtu kuchaguliwa kwa sababu hataki kujiunga na chama cha kisiasa.

Je twaweza kuwa na wagombea huru?


Ndiyo. Tukikaa chini tunaweza kufikiria ni jinsi gani mgombea huru katika Tanzania anaweza kugombea. Tunaweza kufanya kwa kuangalia levels za uongozi na hivyo kuona kuwa kizingiti cha kugombea kama mtu binafsi kinakuwa kikubwa zaidi unapopanda ngazi za juu lakini bila kufanya kiwe kikubwa hadi kigeuke kuwa kizuizi.

Pia tukumbuke kuwa tunaposema mgombea huru hatuna maana asiye na chama bali hata mwenye chama ambaye hataki kugombea kupitia chama chake au chama chake hakikumpa nafasi ya kugombea lakini anaamini wananchi wanamtaka.

Hebu tuangalie kwenye level mbalimbali. Pamoja na mtu kutimiza masharti ya mpiga kura, mgombea huru katika nafasi zifuatazo afanyiwe hivi:

a. Udiwani:


- Awe ni mkazi wa eneo hilo kwa angalau miaka mitatu mfululizo
- Apate wadhamini angalau asilimia 30 ya wakazi wa eneo hilo
- Kila mdhamini awe amewahi kuwa mkazi eneo hilo angalau miaka 2
- Awe na Ilani yake (platform) na ilani hiyo isiwe kinyume na Katiba ya nchi au sheria.
- Ilani yake iwe na wadhamini angalau wa tano ambao watatia sahihi kuwa haipingani na sheria.
- Aunde timu ya timu ya watu wasiozidi 20 kusimamia kampeni yake na hakuna mipaka kwa wale watakaofanya hivyo kwa kujitolea. Wale ishirini lazima wajulikane kwa tume.
- Afungue mfuko wa mgombea ambao utaonesha wachangiaji na matumizi ni nini. Kwa mgombea atakayepoteza nafasi yake, fedha hizo anaweza kuzitumia kuanzisha mfuko wa jamii wa eneo analotoka au kuziweka dhamana kwa ajili ya mfuko wa kampeni ya mgombea atakayemuunga mkono.

b. Ubunge:


- Awe ni mkazi wa jimbo husika kwa angalau miaka mitatu
- Awe na wadhamini angalau asilimia 20 ya kura za maoni
- Wadhamini hao wawe ni wa kazi wa eneo hilo kwa angalau miaka miwili mfululizo
- Awe na timu isiyozidi watu 50 kusimamia kampeni yake na wajulikane kwa NEC. Kwa wale wanaojitolea hana mipaka.
- Awe na Ilani yake inayofafanua agenda yake kwa wapiga kura wake na Ilani hiyo isipingane na Katiba au Sheria za nchi. Ilani hiyo lazima ipitishwe na Mahakama ya Wilaya Ilani hiyo idhaminiwe na angalau watu 20 wa Jimbo lake hilo kwa kuweka sahihi zao kuwa wanakubaliana nayo.
- Kama ni mwanachama wa chama cha siasa akichaguliwa hatotakiwa kuwa chini ya nidhamu ya chama chake.

c. Urais


- Apate udhamini wa watu 150 na kutoka kila mkoa angalau wananchi wasiopungua wasiopungua 5 kutoka kila mkoa.
- Awe na timu ya watu wasioziidi 50 kusimamia kampeni yake na hana mipaka katika wale wanaoijitolea
- Awe na Ilani yake ya mgombea ambayo itapitiwa na Jaji yeyote wa Mahakam Kuu.
- Lazima awe na mgombea mwenza ambaye atatoka upande mwingine wa Muungano.
- Kama ni mwanachama wa chama cha siasa akichaguliwa hatotakiwa kuwa chini ya nidhamu ya chama chake.


Well.. kuna ubaya gani kufikiri vitu kama hivi badala ya kuamua kufuta tu haki ya mtu? Ndio maana nakubaliana na kauli kuwa serikali kuamka na kufuta haki ya mtu kwa vile haiipendi haki hiyo ni uamuzi wa kipumbavu.
 
Karibu sana Prof Kaiyurankuba.........mchango wako hapa unahitajika sana......
 
Watu siku zote tumekuwa tukiwalaumu vyama vya siasa kwamba vimeshindwa kuwafikia wananchi. Sasa hili ni jambo la kila mtu na zaidi ya yote haliwahusu sana vyama vya siasa kwa sababu kwao linawaathiri, positively or negatively, moja kwa moja. Sasa hapa ndipo mahala pa wale wasioabudu siasa za vyama akina Mkama na wengine kuongoza haya mapambano. Kinachotakiwa sasa ni kuwaelimisha wananchi waelewa umuhimu wa mgombea huru (mimi sipendi kuita mgombea binafsi maana inaharibu maana) na kisha kuwa-moblise kwa maandamano kuelekea katika bunge la bajeti huko Dodoma kuanzia next month. Huku bungeni tuendelee kuandamana kila siku hadi pale siku ambapo bunge litatunga sheria ya kuwa na mgombea binafsi. It is time for actions.

Mkandara, nimekusoma sana lakini ni vigumu mno kukubaliana na sababu zako za kukataa mgombea binafsi! Anyway, ndio uhuru wenyewe huo. Ambacho hutaki kukubaliana nacho ni kwamba kama vile ambavyo tunavumiliana hapa kwa mawazo tofauti, tena kuna wengine humu wana mawazo ya ajabu kabisa na ni very minority, lakini tunaendelea kuwaheshimu na kulinda uhuru wao wa kutoa maoni yao. Vivyo hivyo, pamoja na kwamba wengi tunaamini katika nguvu ya umoja, lazima tuheshimu na kulinda uhuru wa kila mtu kugombea uongozi kupitia chama au yeye mwenyewe.

Hiyo ya kung'ang'ania watu kugombea kupitia kwenye vyama ndiyo inayosababisha hata wabunge wetu wakienda bungeni wasiweze kujenga hoja kwa uhuru na kujitegemea. Matokeo yake wanasubiri kwanza kujua msimamo wa chama chao ndio waongee bungeni. Isitoshe, sisi demokrasia yetu na hata dini tumeiga kutoka kwa wenzetu wa magharibi ambao wanaruhusu mtu kugombea kupitia kwenye vyama au bila chama. Tena hata ukishakuwa mbunge unaweza kuachana na chama chako bila kuathiri ubunge wako. Sasa kwa nini tunapenda kuiga mambo nusunusu?
 
Mkuu Mwanakijiji,
Safi sana nimekusoma na nitakueleza wapi ulipochanganya...
Haki zilizotajwa ktk Ibara ya 20 ni haki za kila mwananchi ambazo haziruhusu mtu kulazimishwa kujiunga na chama - kuwa Mwanachama.. Mathlan wewe hapo leo hii huna chama na huwezi kulazimishwa na mtu ama serikali kujiunga na chama chochote ili upate kazi ama mahitaji yako ya msingi (Haki za kibinadamu) ama hii haki ya kupiga kura kuchagua kiongozi..Hivyo wanaozungumziwa hapa ni wananchi, nje ya mtu mmoja anapotaka kugombea nafasi ndani ya siasa (Mwanasiasa) hapo utalazimika kujieleza..
Tena basi tuna bahati sana Afrika utakuta vyama karibu vyote vinajiita Blaa blaa Demokratic party lakini vyote vina mrengo mmoja. Nchi nyingine utaambia biashara hiyo imeshachukuliwa, sema tofauti yako na chama kilichotangulia upate kusajiliwa..Huwezi kuwa na vyama vitano vyote vinazungumzia kitu kile kile tofauiti yake eti ni wagombea. hapa mkuu hawa wote walitakiwa kugombea ndani ya chama kimoja chenye mrengo sawa kisha ndio waingie ktk uchaguzi mkuu. (Kina Obama na mama Clinton tunawaona)
Na Lau kama kina Salim wameshindwa ndani ya CCM basi watoke nje na kusajili chama kinachopingana na CCM, hata kama wakianzisha chama cha UJAMAA (kikomunist) atapata nafasi ya kugombea kama anavyotaka kuwa mgombea binafsi..
Mimi sioni tatizo lao nini hasa! Unapotaka kushindana ni lazima ujiandikishe na chama ni mhuri wa uwakilishi kama vile Olimpiki inakuja ni lazima uwe na nchi (watu) ya kuiwakilisha, huwezi kuingia tu na kusema huu ni ubaguzi kwa nini iwe lazima niwe na nchi ya kuwakilisha kama nikitaka kujiwakilisha mwenyewe?..Then huyo mtu nia yake ni binafsi pia ameshindwa kuona nini maana ya Olimpic na taratibu zake. Court iotakayo ruhusu watu binafsi kuingia basi hiyo Olimpic iapotosha manaa yake na kuwa kitu kingine kabisa.
Kwa hiyo ni muhimu sana kuweka mwongozo unaohusiana na Wanasiasa,
Kwa maana hiyo labda nishereheshe mfano wako hapo juu 20 (2) ni kwamba Hakuna mtu anayelazimishwa kuingia dini yoyote ni haki ya kila mtu kuchagua dini ama kutoabudu kabisa, lakini kama utapenda kushiriki ktk uchaguzi wa Ma Padre ama Ma - Sheikh hapo mkuu utakumbana na sheria za dini.. pamoja na kwamba haki yako ya kuabudu unachotaka haiondoki itabakia pale pale.. kanisa ama msikiti watakupima uwezo wako kuongoza sala na utaratibu huu haupotoshi ile haki ya kila mtu kuabudu dini anayoitaka..Kesho yake tu unaweza kuchomoa na ukasema toka leo mimi ni naabudu Mizuka hivyo najikata na hakuna sheria itakayo kufunga kutokana na haki ile ya 20 (2).

Kumbuka kama nilivyosema hapo awali kuwa hatuzungumzii haki ya binadamu kuishi na kadhalika ila tunazungumzia haki inayoambatana na uchaguzi wa Demokrasia... Unahusu Wananchi mbali na viongozi kwa sababu haki zote zilizoandikwa huwa ni msahafu wetu sisi wananchi kama kinga dhidi ya hao viongozi wanaotaka kutawala pamoja na kwamba wao pia wanayo ile haki ya msingi inayotangulia.. 20 (2)..Akisha kuwa kiongozi (Bihind the wheel - Mungu mtu) basi yeye ndiye anatakiwa kuhakikisha haki hiyo inapewa wananchi..
Hivyo basi mfumo huu wa uchaguzi wa viongozi umetanguliza haki za wananchi kumchagua yeye kiongozi atakaye waongoza na inahusu watu wote ikiwa ni pamoja na kiongozi mwenyewe ndio hata yeye hupiga kura..Lakini kinachoendelea Bongo ni haki ya mtu mmoja ama wawili kuingia ktk uchaguzi bila kupitia sheria za usajiri ambazo ni lazima ziambatane na chama kwa sababu mgombea yeyote ni lazima awe anawakilisha haki za WATU ambao sio lazima wawe wananchama.
Hivyo basi hata kama Mtikila anataka kugombea kwa sababu ya kulitangaza jina la bwana Yesu kisiasa, anaruhusiwa kisheria na atatakiwa kusajili jina la chama hicho kuwakilisha wale wanaoamini imani hiyo... Only what we want he must come open na sio kusuasua migongoni mwa watu kuwapumulia!
Hivyo basi sipendi kuzungusha sana hii issue isipokuwa ni muhimu tufahamu kwamba hakuna haki yeyote iwe toka UN ama ya Kidunia inayomhusu mtu mmoja mmoja pindi anapojisikia...Na huwezi hata kusema kwamba hawa jamaa zetu wanabaguliwa kwani Ubaguzi huonekana pale mtu anapotimiza masharti yote lakini bado atakataliwa bila sababu ya msingi..
Wagombea binafsi Tanzania wanataka kupewa nafasi hiyo bila masharti wakati hawana ujumbe unaowakilisha kundi la watu..isipokuwa wanachotazama ni nafsi zao wao.
 
Mheshimiwa Mkandara, katika hoja yako kuna mapungufu kadhaa ambayo nitayaangalisha:

a. Haki ya mtu mmoja mmoja na haki ya kikundi

Katika jamii haki ya wengi hulindwa kwa kulinda haki ya mtu mmoja mmoja. Haki ya kuishi kwa mfano ni haki ya binadamu wote, lakini ulinzi wake unaanzia kwa kuhakikisha kuwa haki ya mtu mmoja mmoja ya kuishi inalindwa kwanza. Haki ya jamii kufanya kazi hulindwa kwa kuhakikisha kuwa haki ya mtu mmoja mmoja kufanya kazi inalindwa; vivyo hivyo haki ya watu wengi kuchaguliwa (kwenye chama) kuongoza inalindwa pale ambapo haki ya mtu mmoja mmoja kuchaguliwa inapolindwa.

Hivyo, huwezi kutenganisha haki ya mtu mmoja mmoja (individual right) kutoka katika haki ya watu wengi (communal right) kwani haki ya wengi hutoka kwa haki ya mtu mmoja (the communal rights of a society proceed from the individual rights of that society).

Kwa maneno mengi, hatuwezi kusema jumuiya ina haki ya kusema lakini mtu mmoja mmoja hawezi kusema hadi awe kwenye jumuiya hiyo. Hivyo, unaposema kuwa mtu ana haki ya kuchaguliwa pale tu atakapojiunga kwenye chama lakini akiwa nje ya chama hana haki hiyo unachezea dhana nzima ya haki (you are trivilizing the whole concept of rights). Hilo la kwanza.

b. Kama anayechagua halazimishwi kuwa kwenye chama kwanini anayechaguliwa alazimishwe.

Binafsi ningeona wana hoja kama wangesema kuwa kila mpiga kura (mwenye kuchagua) lazima awe mwanachama wa chama cha kisiasa na hivyo basi yule anayechaguliwa naye lazima awe mwanachama. Lakini hawafanyi hivyo, wanasema anayechagua anaweza awe kwenye chama au la lakini haki yake ya kuchagua haihusishwi na kujiunga na chama.

Sasa hapa ndipo penye tatizo; unasema kumchagua mtu huru asiye na chama ni kuwa atatumia maslahi yake binafsi au kutowakilisha maslahi ya jumuiya kubwa ni kosa. Hivi wale wapiga kura huru wasio na chama wanapopiga kura wanapiga kura kuwakilisha maslahi ya nani kama siyo ya kwayo? Mtu asiiye na chama akimchagua mtu mwenye chama anaharibu kura yake? La hasha.

Kama sivyo kwanini basi anayetaka kuongoza na jamii inamkubali kuwaongoza kwanini na yeye asitambuliwe kuwa anayo haki ya kuchaguliwa bila kulazimishwa kujiunga kwenye chama?

Nimekuonesha mifano hapo juu ya mapendekezo ya jinsi gani mfumo wa wagombea huru (wawe kutoka kwenye vyama au nje ya vyama) yanaweza kufanyika hujanionesha matatizo yake ni nini?

Kwangu la msingi ni kutengeneza mfumo mzuri wa kuhakikisha wagombea huru wanakuwepo na wanaruhusiwa.

c. Kukataza wagombea huru ni kuwanyima watu haki ya kuchagua na kuchaguliwa.

Kwenye kijiji ambacho chama chenye tawi ni CCM na wanasimamisha mgombea wao aliyepitishwa na chama hicho lakini wananchi wengi (wanachama na wasionachama) hawamuungi mkono itakuwaje atakapotokea mwanachama mwingine wa CCM hapo hapo ambaye anataka kugombea lakini nafasi iliyopitishwa na CCM ni moja? Huyo mgombea hataki kujiunga na chama kingine kwani havipendi na anazipenda sera za CCM na anakubalika zaidi kwanini tumkataze kusimama kama mgombea huru ambaye anaapa kuwa hata akichaguliwa kuwa kiongozi atatelekeza sera za CCM?

Kama wananchi wanamtaka mgombea huyo na hawamtaki huyo "aliyepitishwa" na chama cha kisiasa kwanini tuwanyang'anye wananchi haki ya kumchagua wanayemtaka kama kweli ndiyo demokrasia? Si demokrasia kiini chake ni utawala wa watu?

Nikupe mfano mwingine; kwenye kijiji kingine vyama vyote vya kisiasa vimesimamisha wagombea wake lakini hakuna hata mmoja anayekubalika au kuonesha kuvutia wananchi au kuonesha uadilifu. Mara wanakijiji wanamuomba mzee X agombee. Lakini tatizo hakuna chama ambacho kiko tayari kumuondoa mgombea wake ili wampishe mzee huyo.

Hata hivyo mzee wetu huyo anasema kuwa yuko tayari kuwatumikia wananchi na katika nafasi yake atatelekeza sera za maendeleo na kuhakikisha shule, kliniki n.k zinakuwepo n.k n.k Na anasema kuwa wananchi wakimpa nafasi ya kuwatumikia atahakikisha kuwa ubadhirifu wa fedha unakoma kwenye shule ya msingi na anawaonesha rekodi yake ya kazi na utumishi na wananchi wakatokea kumkubali. Tatizo ni kuwa anakubali siku moja kabla siku ya mwisho kwa nec kupokea majina ya wagombea.

Je, mtu huyo anyimwe nafasi ya kugombea kwa sababu hakupata nafasi ya kupitshwa na chama cha kisiasa? Je wananchi wanyimwe haki ya kumpata mgombea muadilifu kwenye kinyang'anyiro na matokeo yake wapewe wasiomtaka.

Ikitokea chama cha NLD kikaamkua kumuondoa mgombea wake na mzee wetu akapata nafasi ya kugombea na baadaye kuchaguliwa kwa kura nyingi na kuwa mwakilishi wao na akafanya kazi nzuri kabisa je tutasema alichaguliwa kwa vile ni mwanachama wa NLD na anawakilisha sera za NLD au alichaguliwa kwa sababu alikuwa anakubalika na mwenye uwezo na angeweza kugombea kwenye chama chochote na kushinda?

Kama ni hivyo kwanini asigombee kama mtu huru bila kumlazimisha afanye unafiki, au umamluki wa kisiasa? Kwanini tumlazimishe ajiunge na chama?

Itakuwa vizuri kama anajiunga na chama anachokubaliana nacho kama alivyofanya Dr. Slaa. Mwaka 1995 Dr. Slaa alikuwa anakubalika sana kule Mbule kumshinda Patrick Qorro. Ninafahamu hili vizuri kwani nilikuwa kona hizo. Patrick Qorro akapitishwa na CCM kugombea na Dr. Slaa akaamua kwenda CCM na wananchi wa Karatu since then wameionesha Tanzania kuwa CCM walifanya makosa.

Nakuhakikishia hata angegombea kama mtu huru Dr. Slaa bado angeshinda.

Kwanini tuwanyime watu haki ya kumchagua wamtakaye bila kulazimisha kukichagua chama chake kama hawazipendi sera zake?
 
Hoja ya kimsingi ni kuwa kila Mtanzania ana haki ya kuchagua na kuchaguliwa kuwa kiongozi wa ngazi yoyote ya uongozi wa nchi yake bila kuwekewa zengwe la kuwa mwanachama wa chama chochote kile kiwacho cha kisiasa. Hivi ndio katiba ya nchi yetu inavyotupa hki sawa raia zake wote.

CCM na serikali yao, siku zote, imekuwa ikivunja katiba katika suala hili. Hii ni jitihada ya mwamba ngoma. Lakini siku za mwizi ni arubaini. Hapa tulipofika, suala la mgombea binafsi halina tena mjadala. Ni utekelezaji tu, kinyume chake ni ufisadi. Viongozi wanaapa kuilinda na kuitetea katiba, huku wakijua wanaivunja kwa faida yao binafsi au ile ya chama chao au vyote viwili.

Hili la kusema kwamba Nyerere kasema hili au hakusema lile, halina maana yoyote katika zoezi hili. Nyerere mwenyewe aliivunja katiba hii. Ni lini aliruhusu wagombea binafsi katika enzi yake? Hata yeye mwenyewe alikuwa akigombea urais na kivuli tu. Yeye anapiga kampeni na kivuli je, kilikuwa kinaendesha kampeni?
 
Mzee Mwanakijiji,
Mkuu huwezi kutenganisha haki ya mtu mmoja mmoja toka haki wa jamii ni kwa sababu haki nzima inahusu jamii hiyo na kwamba matendo hufanywa na mtu mmoja mmoja lakini hiyo right huandikwa kwa ajili ya jamii nzima..
Mfano chukulia haki ya kuishi, inahusu jamii yote lakini wapo baadhi ya watu ambao hukutana na matatizo (individuals) na ndipo tunapotumia kifungu cha sheria hiyo inayohusu jamii..
Nachosema mimi hakuna haki inayoandikwa kwa ajili ya mtu mmoja hivyo jamii nzima waikubali haki ya mtu huyo..Utaratibu huu ndio uliopigwa vita na ujio wa Demokrasia kwa sababu zamani Masultan ndio walikuwa na haki ya kutawala kisheria na kati yao waligombea vile vile within royal family hizo lakini wananchi hawakupewa nafasi ya kumchagua kiongozi. Wakafuatia Madikteta ambao kwa kutumia nguvu ya chama au Jeshi waliteua ama kuchagua kiongozi bila wananchi kuhusishwa pia..

Hat ukitazama huko kwenye utawala uliokuja pingwa na Demokrasia utakuta kilichotangulia ni ile executive power kuwa chini ya royal prerogative au tuseme Jeshi na sio individual ambao hawana nguvu ya kutawala kama hawana executive power vested in.
Power zote zinakuwa possessed by the Title na sio individuals pamoja na kwamba ni individuals watakao tawala. Bila shaka kwa mtazamo finyu unaweza kushindwa kuona nachojaribu kusema hapa, lakini mkuu ni rahisi kabisa.. ndio maana nikasema ni haki ya kila mtu kuabudu dini unayotaka ndiyo sheria imetungwa kwa kuitazama jamii nzima ya binadamu lakini individuals ndio wanakutwa na majanga haya kila siku sheria ipo kuwa protect.
Tukirudi ktk uchaguzi nitarudia kusema kwamba haki ya mtu binafsi bado kabisa wakati wake Kantazania kwa sababu hadi sasa hivi siasa zetu zinatupotosha zaidi. Siku tutakapo weza kusimamisha Demokrasia na vyama vikawa vinatazamwa kwa mrengo na sera zake na akachaguliwa kiongozi anayeonekana kuwa mbora ktk kuwasilisha sera hizo kwa wananchi hapo naweza kukubali watu binafsi wanaokuja na hoja tofauti kabisa na vyama hivi..Not now hasa nikiwaona wagombea wenyewe wanaotafuta ULAJI na hawana mpya kisiasa zaidi ya ahadi za kutupa Utajiri!

Mkuu bila kubisha sana ebu turudi nyuma kwenye shina la hii issue.. Nini maana ya KIONGOZI?..
Nauliza hivyo kwa sababu huwezi kujijengea jina la Mheshimiwa (Hon) kuongoza wananchi kwa utaratibu unaoutaka wewe..sheria na utaratibu hutazama the mass population ama title kisha huijengea sheria kuipa kinga ya kutoingia wasiokuwa na haki. Kwa maana hii Diwani , Mbunge na rais hawa wote ni Wa - Heshimiwa, hivyo utaratibu unatakiwa kulinda heshima hii kutolewa ovyo kwa mafisadi...

Kisha bado hujanijibu swali langu mkuu hawa wanaotafuta haki ya individuals kugombea Uheshimiwa wanashindwa kitu gani kujiunga na Upinzani ikiwa matokeo ya matunda ya kujiandikisha kwao hakutakuwa na tofauti kama wakiwa individuals.. Kama hawakubaliani na vyama vilivyopo then kwa nini wasituambie kwanza kile wanacho amini wao tofauti na vyama hivi..
Imean hii ndiyo inayomkuta Field Marshall Es na hata wewe wakati fulani yaani watu wanakupinga kitu lakini wao hawana jibu wala solution isipokuwa wanapinga tu ulichoamdika. Why? ati haikukaa sawa!
Sema basi usawa ni Upi? watu wanazunguka tuuuu, kumbe hata ukweli wa issue nzima hawana isipokuwa wanajaribu kudadisi zaidi upate kuingiwa hasira zaidi..
 
Kwaminchi,
Hoja ya kimsingi ni kuwa kila Mtanzania ana haki ya kuchagua na kuchaguliwa kuwa kiongozi wa ngazi yoyote ya uongozi wa nchi yake bila kuwekewa zengwe la kuwa mwanachama wa chama chochote kile kiwacho cha kisiasa. Hivi ndio katiba ya nchi yetu inavyotupa hki sawa raia zake wote.

Mkuu kwanza kumbuka kuwa hapa tunahoji sheria zetu iwe for or against.. ni mawazo ya kila mtu kutokana na utaratibu uliopo au utakao kuja. Kwa hiyo sheria tunaiweka nje kwanza na kutazama kile kinachotokea/kitatokea kwa kujenga hoja zetu..
Hata hivyo naomba kifungu hicho cha sheria (Katiba) kinachosema hivyo..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom