BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,007
Kuna hili swala la Wanaume na Wanawake ambao wako kwenye mapenzi mazito ndani ya ndoa au katika uBF na uGF wanampenda sana mwenzi wao katika mapenzi kwa kupindukia lakini hawako tayari kumwambia hivyo muhusika ili ajue anapendwa kupindukia badala yake wapo radhi wawaambie ndugu, jamaa na hata marafiki wa muhusika au ndugu, jamaa na marafiki zao. Wengine hudai kwamba muhusika akitamkiwa hivyo kwamba anapendwa kupindukia basi ataanza kuleta za kuleta. Hili Waungwana limekaaje? Kwanini kusiwe na uwazi wa kumwambia mpenzi wako kwamba unampenda kupindukia na penzi lake kwako linakufanya ujisike na furaha kupita kiasi? Kwanini akayasikie maneno haya kwamba Mumeo/Mkeo au BF/GF anakupenda kupindukia kutoka midomoni kwa ndugu, jamaa na marafiki badala ya wewe muhusika mkuu!? Kulikoni?