Kupeana faraja na furaha.

Nzuri sana...
Nimeikubali...
kuna watu wana mioyo mikuu, na wanajua kutoa na kujitoa kwa ajili ya wengine...
Tupo wachache lol
 
mkuu hiyo mioyo wamejaliwa wachache sana

Na tunapata shida sana wenye hiyo mioyo wala usitamani coz kila mda unajifeel kubeba mizigo ya watu,
Na unajali sana... sasa kwenye dunia ya sasa tunaonekana ni watata...
ila ndio hivyo ni kama karama toka kwa Mola
 
Wagonjwa wawili walikutana hospitalini,moja alikuwa amepata ajali ya miguu na mwingine alikuwa amepooza mwili.
Wagonjwa hao walizoeana,walielezana na kuambiana mambo mengi ya kimaisha,kutiana moyo katika hali zao
ngumu walizonazo.Aliyekuwa amepooza mwili kitanda chake kilikuwa karibu na ukuta na aliweza kuangalia nje kupitia dirishani,ila aliyepata ajali ya miguu kitanda chake kilikuwa upande ambao haukuwa na dirisha.Walikuwa wakikesha ndani bila kutoka nje kutoka na hali zao mbaya.Aliyepata ajali ya miguu alikuwa anamwuliza mwenzake kila siku kuhusu hali ya hewa huko nje na kila kitu kinachofanyika kwasababu mwenzake alikuwa analala karibu na dirisha.
Ambaye alikuwa amepooza kila akihadithia hali ya hewa jinsi ilivyo huko nje mwenzake alikuwa akifunga macho huku akifanya imagination ya hali ya hewa na mambo mazuri aliyokuwa akihadithiwa.
Aliyepooza huwa akiulizwa kuhusu huko nje alikuwa anaeleza ''Sasa hivi nimeangalia nje kupitia dirishani,nimeona bahari nzuri,bata wa kila rangi wanaogelea,naona familia nyingi zikifurahia maisha mazuri,naona wachumba wakiogelea na kupeana maua meupe na mekundu na kila aina ya rangi,wanafurahia upepo wa ufukweni,usijali mi na wewe ipo siku tutapona na tutafurahia kama wao'''
Wakawa wanafurahia maisha ingali wagonjwa.Aliyekuwa amepooza akafariki,siku nesi alipokuja kuchukua mwili wa aliyefariki yule mwenye matatizo ya miguu akamwambia nesi naomba nipeleke kwenye kitanda cha mwenzangu,mana yeye alikuwa akinihadithia hali ya hewa nilikuwa nafurahi,mimi nataka niwe naangalia nje kupitia dirishani.Nesi akampeleka kwenye kitanda cha mwingine,cha kushangaa alipofungua dirisha na kuangalia nje zaidi ya kuona ukuta mkubwa mbele ya dirisha na hakuweza kuona kwingine.Akamwuliza nesi,inakwaje mwenzangu kila siku ananihadithia hali ya hewa nzuri na watu wakicheza ufukweni wakati mbele ya dirisha kuna ukuta wa jengo lingine kwa nje?Nesi akamwambia,mwenzako alikuwa kipofu na hakuweza kuona kabisa,kwa hiyo alikuwa anafanya hivo ili uwe na furaha.



Ujumbe.........wengi wetu tuna matatizo ila sisi tulio na mioyo ya uvumilivu na matumaini tuwe na mioyo ya kuwapa faraja na kuwafurahisha ambao wana mioyo laini na dhaifu kuliko sisi.
Mkuu, this is really nice

and just to let you know that i usually like your posts very much... real life, indeed
 
Mkuu, this is really nice

and just to let you know that i usually like your posts very much... real life, indeed

Thanks much mkuu.....ila wakati mwingine mtu kuwa na moyo kama huu inakuwa kama kipaji mana wengi wetu tunajali zaidi nafsi zetu
 
Ujumbe.........wengi wetu
tuna matatizo ila sisi tulio na mioyo ya uvumilivu na
matumaini tuwe na mioyo
ya kuwapa faraja na
kuwafurahisha ambao
wana mioyo laini na dhaifu
kuliko sisi.

Safi sana mkuu.
Nimeipenda.
Sababu sitoagi like wewe nakupa leo.
"Like".
 
DUUUUUUUHHH, Inapendeza unapoweza kumfanya mwenzako mwenye Matatizo ajisikie Furaha

Japo na wewe una matatizo, Tena Makubwa na Magumu kuliko

Tuamini kwamba kila linalotokea MUNGU anampango kamali ktk hilo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom