Kupatwa kwa Mwezi kesho: Tegemea Haya

Danniair

JF-Expert Member
Feb 18, 2011
360
66
tarehe 14/6/2011 niliweka thread hii "
Kesho tarehe 15/6/2011 mwezi utapatwa katika nyota Mshale katika nyuzi 24[SUP]o[/SUP]23[SUP]'[/SUP]. Sakata hili litaanza hapa kwetu saa 2:24:34 usiku na kuisha saa 8:00:45 usiku wa manane. Ifikapo saa 4:22:30 mwezi utaanza kugeuka rangi kuwa mwekundu na ifikapo saa 5:12:37 usiku basi kuna mawili au utakuwa hauonekani kabisa (ukizingatia volcano iliyolipuka hivi karibuni na kutupa vumbi jingi sana angani), ama utageuka na kuwa kama damu iliyoganda. Ukiangalia tutakuwa na masaa 3:30 ya mwezi mwekundu na jumla ya masaa 7 ya tendo zima la kupatwa.

Tutegemee nini basi, kwa wale waliozaliwa kati ya tarehe 13 juni hadi 20, na desemba 13 hadi 20 wakae chonjo kwani wana miaka saba ya machungu. Pia kwa wale wenye sayari ktk nyuzi hizi 20-28 Mapacha na Mshale (ikiwemo nchi yetu). Kubwa zaidi kutakuwa na ugunduzi mkubwa wa habari za uongo ambazo zilikuwa zikijulika kama za kweli, hii inaweza kuleta mtafaruku. Kwa kuwa Mars ndiye atakuwa bwana wa kupatwa huku ambako nako kunatokea ktk nyota ya moto - mshale, machafuko, vifo vya jumla, mioto, vitegemewe sana. Uzuri mmoja ni kuwa Mars akiwa ndiye bwana wa kupatwa ataonyesha na njia ya kutokea pia ktk matatizo hayo.

Usiku wa kupatwa tunashauriwa kufanya haya; kuoga wakati wa kupatwa, kusali (andika sara yako kwenye karatasi safi kisha ichome moto, hapa nini maanisha unacho taka kitendeke ktk maisha yako, na usichotaka kitende kiandikwe kwa AMRI ya neno naachilia jambo hili na hili. mf. naachilia tabia yangu ya ulevi iende ilikotoka isirudi kwangu tena). Kula kabla ya saa 2:24:34.

Katika usiku huu unashauriwa usifanye haya: tendo la ndoa, usigombane, usiseme uongo, usile.

Mambo ni mengi sana kwa leo nakomea hapa.

Najua majumbani magomvi sasa yameisha anza, lakini chukulieni magonvi hayo kama chachu ya kusonga mbele. Na magomvi haya hasa ni kuhusu watoto, majirani, elimu, n.k. Kwa wale walioharibikiwa na magari simu, computer msihofu ndo nyota ya mapacha inavyoliwa ambayo iko mkabara na Mshale.

Siku njema.''

hapo penye red!! inatupa picha kamili jinsi ambavyo bajeti zetu zimekuwa zikipitishwa na wabunge wetu kwa mtindo wa bahasha!
Pia hapo penye red panatudhihirishia unafiki wa wamiliki na waadishi wa magazeti ya The Sun na news International.
 
Back
Top Bottom