Kupanda Ndege tatu Kigoma - Dar, Dr. Mwakembe Tusaidie.

Ambiente Guru

JF-Expert Member
May 21, 2012
2,596
1,071
Narejea hotuba ya Mhesh. Rais J. Kikwete kwenye shughuli za Precision Air juz juz kuwa mashirika ya ndege yazingatie sheria. Tarehe 1 August 2012 nilipanda ndege TATU tofauti za Precision Air kutoka Kigoma hadi Dar es Salaam katika kipindi cha masaa SABA na kutua Mwanza na Kilimanjaro. Hili linawezekana sehemu nyingine duniani au ni Tanzania tuu?. Tuliondoka Kigoma saa nne hivi na kufika Dsm saa 11.30 jioni. Hawakutupatia Chakula kamili (lunch) isipokuwa kuambulia vitafuni (sandwitch na korosho) tu wakati wote tukiwa angani na transit. Jamani lioneni hili.
 
hawezi kukusaidia yuko busy na watu wanaokunya njiani wakiwa kwenye mabasi.

Ndiyo maana napenda JF. Yaaani huwezi shindwa kucheka hata kama una stress za kufa mtu. Kigogo, yaani nimecheka sana baada ya kusoma bandiko lako.
Telo.
 
Dk Mwakyembe jana amenukuliwa humu, hawezi kuitegemea JF kama source ya habari. Nachelea kilio chako huenda kisimfikie.
 
...Hivi, kabla hata ya kumtafuta Mwakyembe, tatizo kama hili hakuna mahali popote unapoweza kushitaki kudai fidia ya kupotezewa muda wako?? Mimi nadhani sisi Watanzania wenyewe pia tuna matatizo. Wakati umefika wa ukifanyiwa unachoona io haki unaanza vurugu mwenyewe kwanza hata kabla hujaomba kusaidiwa na mamlaka zinazohusika! Ifike mahali tuanze kuyapa haya makampuni yanayotoa huduma hafizu a run for their money ndio labda wataanza ku-sit up na ku-take note!!
 
hii nayo ni aina mpya ya Kuchimba Dawa Sasa! Ndege tatu! safari Moja... au Pengine walikuwa on test ndege zao... Poleni Sana... hii ndio asiyotaka Ulimbok.. ops Dr.Mwaikembe
 
Back
Top Bottom