Kupanda kwa ghafla kwa bei za bidhaa mbali mbali baada ya uchaguzi

Kwa kuwaudhi zaidi...
Duh! kumbe kilimo sasa hivi kinalipa hivi kwani nini msichukue jembe mkalime?
 
mijitu ilijifanya inajua kuliko ukweli walokuwa wanaambiwa sasa acha wakomeee...... Chama cha kijani oyeeeeee......
 
Bila kusahau ka mkweche kangu nilikokuwa nalipia 100000/= kwa mwaka ghafla kamekuwa 150000/= tra mpaka nilishikwa na kigugumizi isee!!!!!!:nono:
 
watu waichukie ccm mara ngapi? walioipa kura ccm ni wanachama wa ccm
Hili nalo neno, ila kwa ajili ya kuweka kumbukumbu sahihi ongezea kidogo hivi kama hapa chini...
....walioipa kura ccm ni wanachama wa ccm na zilizobaki (neutrals na vyama vingine) ziliwekwa mafungu matatu - chache alipewa my Prez Dr Slaa, kiduchu zaidi aligewa Lipumba na fungu lililobaki (again za Mr Prez Dr Slaa) zilichakachuliwa!!
 
naongezea kidogo (maeneo ya - sinza)

chumvi gm 250 toka 150 baada ya uchaguzi 300
always za kina dada 1300 baada ya uchaguzi 2000
petrol 1500 baada ya uchaguzi 1800
samaki fresh 4500 kgbaada ya uchaguzi 5500


naongezea mafuta ya kupikia lita 5 toka shs14000 hadi 17000.nilichoka sana nilipokwenda kuyanunua dukani.
 
Wanarudisha pesa zao walizotumia kwenye uchaguzi...mmesahau kwani!? Wameichangia sisiemu sana! Hapo wanapewa na tax holiday. Hebu fuatilieni TRA mtashangaa mapato kushuka!!!!!!1
 
Yote nakubaliana nayo, tutawalaumu sana wakulima na wote wa mikoa ambayo imetajwa. kwanza kabisa matokeo ya hiyo mikoa siamini kama yalikuwa hivyo, kwa mwamko niliouona binafsi ktk nchi naamini hao walikuwa ni victim zaidi kwa kuchakachuliwa, All and all hapaswi kulaumiwa mtu au kundi fulani sababu hatima ya yote TUME NDIO YA KULAUMIWA kwa sababu ili present sivyooooo! sasa tusitwist. Watu walisafiri kutoka mikoa waliokuwako kwa ajiri ya kupiga kura...mabasi stand zote hayakufanya kazi kwa sababu movement za wasafiri haikuwepo.... wapiga kura waliwahi sana asubuhi kwa mwamko......kwa ?????????? ulidhani wanaenda kufanya?
 
safiiiiiii kabisa hii ndo sawa. Ni namna ya kuzirudisha zile za kofia, vilemba, kanga fulana na 5000/=. walifikri za bure na walibeza sana cementi kuuzwa 5000/= kwa mfuko.
 
Kwa maoni yangu, nadhani sababu kubwa ni kushuka kwa thamani ya shilingi. Nina imani kuwa CCJm ilimwaga pesa nyingi sana kwenye mzunguko bila kujali tija. Shahada za kura ilikuwa ni mali, kuweka bendera ya CCM kwenye daladala ilikuwa ni mali, kuvisha gazeti kava ya CCM ilikuwa ni mali, kuandika vizuri kuhsu CCM ni mali, kuimba bongofalva kusifia CCM mali. Tena mali zote hizo zilikuwa za pesa nyingi. Uksihajaza hela ya madafu kwenye mzunguko kuliko tija ya nchi basi basi shilingi hiyo inakuwa haina thamani. Hapo ndipo majirani wanapofurahi kuona uchumi wetu ni kama kichwa cha mwendawazimu. Tangu uchaguzi wa kura ya maoni ndani ya CCm unanze, shilling iliporomoka, na sasa hivi iko kwenye steep slope kuelekea bondeni.

Shilingi.JPG
attachment.php

Sifa pekee ya Mkapa ambayo ndiyo ninayomheshimu ni kuwa alidhibiti sana usambazaji wa shilingi hovyo hadi watu wakawa wanaita ukosefu wa shilingi kuwa ni Ukapa.
 
Wafanya biashara wakubwa ndio waliokichangia chama cha ccm, mabilioni waliyotoa mnadhani watayarudishaje? wanakamuliwa wananchi ili fedha irudi, so indirect, walala hoi ndio waliokichangia chama cha ccm.
 
kuna siku (kabla ya uchaguzi)nilikuwa navuka naelekea Kigamboni,
Wakati nakata tiketi nikamwuliza makataji tiket mbona gharama ya kuvuka kwa gari ni kubwa.
Akasema na bado kwani baada ya uchaguzi gharama itapanda zaidi.
Nikashangaa kwanini ipande baada ya uchaguzi, nami sikupata jibu.

Ndibalema umenigusa sana-Miezi michache kabla ya uchaguzi nilikuwa bongo hapo wakati petrol ina-range btn 1600-1650) Ewura wakatoa tangazo kuwa bei ya mafuta inatakiwa ishuke kwa asilimia kati ya 3%-4...% kwani imeshuka katika soko la dunia, siku mbili baadaye nikapita katika petrol station moja ambayo ilikuwa ikiuza petrol 1630, bei ikawa 1650; nikamuuliza muuzaji vipi bei imepanda wakati inatakiwa ishuke akajibu kwa dharau kama ilivyo kawaida yao dada zetu hawa walio katika hizi petrol station utadhani kama na wao wana share humo "Bei Ishuke!? na bado itapanda sanaa!!? si mnajifanya mnataka kwenda ikulu nyie?" Hajui kwamba mafuta yale yakipanda na yeye na yy inakula kwake pia na yeye akibakiwa na kimshahara chake cha 50,000/. Nikaachana naye nikaweka wese langu huuyooo nikatoweka. Yes, ni kweli kutoka 1650 ikapanda 1680, then 1720 then 1750,I do no kama sasa ishafikia 2000/ au 3000/

Niliwahi kusoma kitabu kimoja maarufu sana kinasema "M/Mungu haondoshi neema kwa watu hadi wanadamu wenyewe waikatae neema hiyo it means haileti neema hadi waitake neema hiyo wanadamu wenyewe. Sasa si tumeikataaa! atailetajeee!
 
Ishu hapa ni kuwa naamini kushuka thamani kwa shilingi ya Tanzania kulitokana na serikali kuchapisha fedha nyingi kwa ajili ya 'gharama' za uchaguzi.
 
NAWASHUKURU WOTE KWA MICHANGO YA MAANA NA YENYE TIJA. NINA IMANI KUWA HATA WABUNGE WETU WA CHADEMA AMBAO WANASOMA MICHANGO KAMA HII WATAPATA KITU CHA MAANA CHA KUONGEA BUNGENI KWA MAANA HAPA TUNAWAKILISHA MAONI YA WANANCHI WA TANZANIA. KWA HAKIKA NIMEGUSWA KIPEKEE ZAIDI NA MCHANGIAJI LUKOLO ALIYESEMA KUWA "Juzi naongea na watu wa bush kwangu wanalalamika kwamba wanashindwa kuuza mahindi kwa kuwa bei ipo chini mno. Sasa bei za mazao ya wakulima zimeshuka halafu bei za bidhaa nyingine ambazo wakulima wanazihitaji zimepanda" NAOMBA UTUFAFANULIE KIDOGO KWA UNDANI ILI UTUWEZE KUANZISHA MJADALA MPANA KUHUSU HALI HIYO KWA FAIDI YA WABUNGE WETU KUPATA HALI HALISI YA WATANZANIA VIJIJINI.


AIDHA NIMEGUSWA KIPEKEE PIA NA KICHUNGUU KUHUSU MATUMIZI MAKUBWA YA FEDHA KATIKA UCHAGUZI YANAVYOSABABISHA MFUMUKO WA BEI MARA TU BAADA YA UCHAGUZI, KIELELEZO ALICHOTUWEKEA KIMESAIDIA SANA KUTUONYESHA HALI HALISI YA KUPOROMOAKA KWA SHILINGI YATU SAMABAMBA NA CCM KUFANYA MATUMIZI YA MAKUBWA YA FEDHA KATIKA KIPINDI CHA KUELEKEA UCHAGUZI KUU HADI SIKU YA UPIGAJI KURA. NAOMABA NA YEYE PIA ATUANZISHIE MJADALA MPANA ULIOSHEHENI TAKWIMU NA TAARIFA MBALI MBALI ILI TUJIELEIMISHE ZAIDI.


NI MATEGEMEO YANGU KUWA BADALA YA KUANZISHA THREAD ZA KUWASEMA SEMA WATU NI VYEMA TUKAANZISHA THREAD ZENYE KUJADILI MATATIZO YA WANANCHI POPOTE TULIPO ILI KUWAHABARISHA WABUGE WETU HALI HALISI INAYOWAKABILI WANANCHI.
 
mimi sikushtukia suala hili kwa sababu nimehamia sehemu nyingine, nikajua kuwa ni bei za huku nilikohamia. Hio kali but Hakuna mwalimu mzuri duniani kama Maisha. Acha maisha yatufundishe kutoichagua CCM.
 
Back
Top Bottom