Kuota nyama

Jomse

JF-Expert Member
Jan 19, 2011
275
92
Nawasalimu wote.Jamani binti yangu wa miaka mitatu na nusu ana kanyama kametokea sehemu ya haja kubwa.

Wenye utaalamu au kujua naomba mnieleweshe kwamba je kina madhara yoyote ?na kama ni tatizo hili tatizo linasababishwa na nini? Na je tiba yake ni nini?

Asante sana.
 
huwo ni ugonjwa mbaya sana, na kikiendelea kukuwa kitamsumbua sana kwani maumivu yake ni makali sana,, muwahishe hospital, kikiwahiwa kinapona.
 
Nimeogopa kumpeleka sasa kwani katika wiki tatu zilizopita alipata homa kali na alipofanya vipimo alionekana ana infection daktari alimwandikia sindano nne za kristapeni .Juzi jumamosi alikuwa na homa kali na vipele ikabidi nimpeleke hosptali ingne,ambapo ameonekana ana surua na kwa sasa anatumia dawa.Ni siku mbili tangu aanze matibabu ya surua,Je itakuwa vema kumpeleka mda huu?
 
the time is now, ngoja ngoja yaumiza matumbo...mpeleke mtoto hospitali usisubiri kesho.
 
Kipo juu ya sehemu ya haja kubwa.Kimekuwa kama kipele hapo juu.Wala haarishi.Na hata nimemuuliza kinauma akaniambia hapana(kwani anaweza kuongea).
 
Kipo juu ya sehemu ya haja kubwa.Kimekuwa kama kipele hapo juu.Wala haarishi.Na hata nimemuuliza kinauma akaniambia hapana(kwani anaweza kuongea).

Issue si kumpeleka kwa Daktari tu, ila Dakatari wa watoto atakusaidia zaidi.
 
Nawashukuru wote kwa ushauri wenu.Nilimpeleka kwa daktari na amemwandikia dawa ya kunywa na za kupaka.Pia amenishauri kumpa mapapai mara kwa mara.
Ameniambia uvimbe ungekuwa na madhara zaidi kama ungekuwa kwa ndani.
 
Magonjwa mengine needs prayer too wakati unaenda hospitali. Ni kibaya hicho kinyama, nimeona kikitibiwa kwa mitishamba ila sikuwahi kujua ni mchanganyiko wa miti gani.

Give yourself hope. Kitapona.
 
Magonjwa mengine needs prayer too wakati unaenda hospitali. Ni kibaya hicho kinyama, nimeona kikitibiwa kwa mitishamba ila sikuwahi kujua ni mchanganyiko wa miti gani.

Give yourself hope. Kitapona.

Asante sana naamin Mungu atasaidia na kitapona
 
Nawashukuru wote kwa ushauri wenu.Nilimpeleka kwa daktari na amemwandikia dawa ya kunywa na za kupaka.Pia amenishauri kumpa mapapai mara kwa mara.
Ameniambia uvimbe ungekuwa na madhara zaidi kama ungekuwa kwa ndani.

Chunguza km kinakua(kinaongezeka kimo)kuna rafk yangu aliwahi kuwa na tatizo hilo wakat anaeleza alikuwa na umri wa miaka 14 na kilirefuka hadi 1/4 mita hivi.Jaribu kuwasiliana na madaktar wengine wakupe ushauri,hivyo vinyama vinasumbua na vikikomaa kukatwa huwa vigumu.
 
Nawasalimu wote.Jamani binti yangu wa miaka mitatu na nusu ana kanyama kametokea sehemu ya haja kubwa.Wenye utaalamu au kujua naomba mnieleweshe kwamba je kina madhara yoyote ?na kama ni tatizo hili tatizo linasababishwa na nini?na je tiba yake ni nini?
Asante sana.

hiyo ni ishu ya muhimbili au kcmc, mwanzo haiumi ila kunasiku ataumwa gafla utashangaa. some times huwa inarudi yenyewe sometimes not. ukitoboa atatoka damu mfululizo bila kufunga. ni hatari sana.
 
Hata mimi napenda kukutoa hofu. Ugonjwa huo unatibika na kupona, kuna jamaa yangu alikuwa anaumwa hivyo hivyo alitibiwa akapona. Hiyo dawa ya kupaka itafanya kinyama kinywee na dawa ya kunywa itauwa vidudu kwa ndani
 
Wanyumbani tutajie hiyo dawa ili tuiatfute kuna mdogo wangu naye anasumbuliwa na hii kitu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom