Kuorodhesha ukabila wako kwenye kitabu cha wageni Guest/Hotel

Rutunga M

JF-Expert Member
Mar 16, 2009
1,769
1,382
Wakuu
Naomba kupata ufafanuzi,hivi kuorodhesha ukabila wako kwenye vitabu vya wageni kwenye hotel na Guest house hapa Bongo ni kwa ajili ya kazi gani.

Kwa sababu ukitazama history ya vita vya wenyewe wenyewe kwa baadhi ya nchi,maandalizi yake yalianzia kwenye mambo ya watu kutambuliwa kwa ukabila.

Mimi nimetazama kwa muda mrefu umuhimu wa kujiorodhesha kwa kabila langu sioni mantiki,kwa kuwa kama mtu unaandika jina,uraia,unatoka,ulikosazaliwa nk kwa nini pia tuulizwe ukabila.

Mimi naona utaratibu huu ungefutwa kabisa
 
Mimi sidhani kama utaratibu huu una ubaya wowote kwa kuwa ni taarifa (documentation) ya mteja ukizingatia kuwa, mara kadhaa matukio ya watu kupata matatizo ikiwema vifo yanatokea ndani ya nyumba hizo. Kwa mantiki hiyo taarifa hizo zitaisaidia dola kama tukio lolote likitokea.

Kwako wewe uliyemhudhuriaji mzuri wa maeneo hayo unahisi kama unajichoresha huko, usiogope bro ni kawaida tu!
 
Kama ukabila ni wa maana kwa nini wakati wa sensa hatuulizwi kabila? Kama serikali inapenda kujua kabila langu nikiwa guest house kwa nini isipende kujua kabila langu wakati wa sensa? Sioni kitu cha msingi kwenye kutaka kujua kabila la mtu. isitoshe watu siku hizi wamechanganyikana sana kwa kuoana kiasi kwamba ni vigumu hata mtu kujipambanua na kabila fulani. Naamini partculars tunazozitoa mbali na ile ya kabila zinajitosheleza kabisa kumtambulisha mtu.
 
Nakubaliana na Babuyao,Isitoshe hata ukabila ungekuwa na maana iwapo tungeulizwa wakati wa sensa.
 
Kama ukabila ni wa maana kwa nini wakati wa sensa hatuulizwi kabila? Kama serikali inapenda kujua kabila langu nikiwa guest house kwa nini isipende kujua kabila langu wakati wa sensa? Sioni kitu cha msingi kwenye kutaka kujua kabila la mtu. isitoshe watu siku hizi wamechanganyikana sana kwa kuoana kiasi kwamba ni vigumu hata mtu kujipambanua na kabila fulani. Naamini partculars tunazozitoa mbali na ile ya kabila zinajitosheleza kabisa kumtambulisha mtu.
Ni kweli kabisa, maana zamani ulikuwa ukimuona mtu ni mweupe...basi kama si MRANGI, MCHAGA NA HASA PALE KWENYE MENO................. NA UKIMWONA NI MWEUSI BASI LAZIMA UTAPELEKA HISIA ZAKO KUWA HUYO NI 'MURA'.......... hayo kwa sasa hayapo .......... HAIFAI........KABILA LIKUSAIDIE NINI.....??? HATA KAMA KUNA MATUKIO YA VIFO ..........HUKO GESTI.........KABILA LA NINI........??? cha muhimu jina na unatoka wapi.............. kwanza majina yetu yalivyo yanajieleza................ kwa mfano wote tunajuwa Joyce Masawe wa kabila gani................. Rwechungura Rutabanziba wa kabila gani.............. Tuntufye Mwakalindile wa kabila gani.................Chacha Mwita Marwa wa kabila gani........... John Komba............. Chilewa Mazengo................... Humfrey Mwakalinga.................. John Shekinyashi Shetani..................Okereyan Olesendeka................
 
Hapo patamu Ngali..

Je Serikali ina lengo gani kuendeleza utaratibu huu,kwa sababu baadhi ya wilaya vitabu hivyo vinachapishwa kabisa vikiwa na kipengele cha mtu kunadika ukabila
 
Hiyo inakusumbua? Kwenye kabila weka MSWAHILI tu, au weka dash kama mdau hapo juu, ukiona mtu anakulazimisha kumwambia ukabila wako muogope kama UKIMWI.
 
Back
Top Bottom