Kuongeza unene

Adm

Senior Member
Sep 19, 2010
149
45
mara nyingi nakutana na maelezo ya namna ya kupunguza unene ama msisitizo wa matumizi ya aina fulani ya vyakula vinavyosaidia kupunguza unene. Swali langu ni je hakuna namna ambayo mtu mwembamba anaweza kufanya ili aongeze unene?
 
hii mbona rahisi sana. fakamia mivyakula kila ukipata nafasi unakula......machipsi, makuku, mapilao, makeki nk wewe wakati wote unakuwa mtu wa kutafuna tafuna:A S wink:
halafu pia unajifunza kunywa beer na vya kusindikizia kibao...supusupu, kiti moto nk. Kama huwezi beer kwako ni chungu basi kunywa mvinyo wa dodoma.
halafu uwe mama/baba lao la uvivu, kazi yako iwe moja tu kula & kunywa sana sana na safari za msalani, zaidi ya hapo unakuwa mtu wa kupumzika tu kwenye kitanda/mkeka/kochi unajipweteka LOL
 
Duh,hiyo dozi ya ukweli lakini kuna mtu alinambia kwamba wembamba ni genetic aspect hata ule vp if you are constituted with such genes huwezi kunenepa
 
Hakuna ati genes za unene au wembamba.
Mnene aweza kukonda, mkondefu naye aweza kunenepa.
Jaribu kutumia dose niliyotoa hapo juu uone, hata kama wewe ni kimbaumbau minofu itakuja tu LOL

Duh,hiyo dozi ya ukweli lakini kuna mtu alinambia kwamba wembamba ni genetic aspect hata ule vp if you are constituted with such genes huwezi kunenepa
 
Adm Ukitaka kunenepa kula kwa wingi Ufuta changanya kidogo na sukari au pia waweza kupika huo ufuta ikawa ndio chakula chako utanenepa mwili wako.
 
Last edited by a moderator:
mara nyingi nakutana na maelezo ya namna ya kupunguza unene ama msisitizo wa matumizi ya aina fulani ya vyakula vinavyosaidia kupunguza unene. Swali langu ni je hakuna namna ambayo mtu mwembamba anaweza kufanya ili aongeze unene?

...Ongeza idadi ya milo kwa siku labda kila baada ya masaa manne unakula portion ndogo ndogo ambazo zitakufanya usisikie njaa hata siku moja baada ya wiki mbili utaanza kuona unajazajaza na kakitambi kwa mbali kanachomoza...Kila la heri katika kusudio lako la kuutafuta unene.
 
Back
Top Bottom