Kuongeza ukubwa wa mauno na maziwa: Tunazuia au tunatangaza?

Rugas

JF-Expert Member
Jan 8, 2009
1,048
196

Siku za karibuni watanzania tumeanza kusikia kuwa sasa dada zetu wanaweza kuongeza makario,maziwa na kubadili mionekano yao kwa kutumia madawa yanayopatikana kwenye maduka ya vipodozi.Swala hili limezua mjadala hasa pale Mamlaka za umma km vile MAMLAKA YA CHAKULA NA DAWA kuanza kuzuia madawa hayo na kusema yana madhara kwa binadamu.

Hapo ndipo yanapozuka maswali mengi miongoni mwa watanzania;

1.Je hapo mamlaka na vyombo vya habari vinazuia au vinawafahamisha
wadau kuwa sasa mnaweza kujibadilisha na kupendeza?

2.Je mbona hizi mamlaka hazijazuia madawa ya kuongeza ukubwa wa
uume,ambayo pia yanasemekana kuwa na madhara na yanatangazwa
mpaka kwenye maTV? Huku si kupendelea upande mmoja na kuacha upande
mwingine uangamie?

3.Je madawa haya yanapita wapi,mpaka yasambae nchi nzima?Kuna udhibiti
hapo kweli?

4.Njia hizi si zinatumika pia kuzuia madawa ya kulevya na vingine
haramu,mbona hakuna mafanikio?

5.'UVUTAJI WA SIGARA UNAZURU AFYA YAKO' basi pia tuandike UTUMIAJI WA CREAM HII UNAZURU AFYA YAKO,turuhusu watu watumie km tulivyoruhusu sigara huku tukijua zina madhara makubwa..

6........................

7.........................

8.......................

Maswali ni mengi,yakijibiwa tutakuwa tumefanikiwa katika hili..
 
Nafikiri wanahitaji Brain Transplant kabla ya kuanza kuongeza maziwa, makalio n.k

Wajiadhari na madawa ambayo yako kwenye majaribio bado lol!
 
Mimi ninafikiri ni sahihi kwa serikali kutangaza madhara yake kwani bila kutangaza watu wengi wanawezakuangamia kwa kuwa hawakujua madhara. Ndiyo kwa namna nyingine ni kama kuzitangaza zaidi dawa hizi lakini mtu akiamua kutumia baada ya kutangaziwa madhara yake basi hatalaumu yeyote zaidi ya nafsi yake.

Ila sasa serikali isiishie kutangaza madhara tu bali ijizatiti katika kudhibiti uingizaji wake ili kuokoa wananchi wake.
 
Pamoja na kuwa TDFA wanajaribu kunusuru jamii na madhara ya madawa inakuwaje madawa ya kubadilisha ngozi hayakufanyiwa jitihada za namna hii? akina dada wengine wamekuwa weupe kama karatasi. Jitihada zifanywe kuzuia uingizaji wa dawa hizo. Bandarini na airport kuwe na xtra uangalizi.
 
Unajua hii inachangia sana na sisi wanaume kupenda vitu flani flani kama mimi mpenzi wa mawowowo sasa anatokea shori kimiss au portable ananipenda sana lakini kwangu mimi naona hana kiwango na vigezo nampiga chini atakacho fanya anatafuta dawa hizo za mchina baada ya miezi 2 anakuja kwa mzee fidel dah mazee teh teh teh si mchezo lazima anipagawishe na kunirusha roho unashangaa unatoa 70,000 kwa wiki kwa ku-retouch nywele.
 
jamaa yangu f angependa awe AUTHORIZED AGENT/SIPPLIER wa haya madawa ya makalio!hahahahahahah
 
Unajua hii inachangia sana na sisi wanaume kupenda vitu flani flani kama mimi mpenzi wa mawowowo sasa anatokea shori kimiss au portable ananipenda sana lakini kwangu mimi naona hana kiwango na vigezo nampiga chini atakacho fanya anatafuta dawa hizo za mchina baada ya miezi 2 anakuja kwa mzee fidel dah mazee teh teh teh si mchezo lazima anipagawishe na kunirusha roho unashangaa unatoa 70,000 kwa wiki kwa ku-retouch nywele.
Kaaaaaaazi kwelikweli
 
Kama kuna anayefahamu wapi yapo ya kupunguza makalio , mm natafuta maana yamezidi. na mm nataka kuwa Miss. Pls Fidel nasikia wewe ni supplier wa dawa za kuongeza mm nitafutie ya kupunguza . ni oder maalumu.Hahahaahahaahah!
 
Hivi kumbe watu huko bongo wanataka kuzidisha mauno sio kupunguza kama wanawake wengine.... I wish I could think that way....
 
Back
Top Bottom