Nguvu ya CCM ni wenye fedha tena fedha chafu. Wanapokomaa na Mafiga matatu ya fedha ndani ya chama chao na kutaka kuharibu, maana yake nini?
Ushindi wao utatoka wapi? Watapewa fedha na nani?
Naona CCM bila Rostam, Lowassa na Chenge ni sawa na chai bila sukari.
Hii thread imekaa kiuchokozi!
Suala la "kuvua gamba" ndani ya CCM ni suala nyeti na muhimu ili kurejesha heshima ya Chama hiki kikongwe. Hata hivyo watu waliotuhumiwa kuwa "vitimbakwiri" (mafisadi) si hao tu waliotuhumiwa wapo wengi. Kwa hiyo, kwa mtazamo wangu bado Chama tawala kina kazi kubwa ya kujivua gamba. Mbali na ukitimbakwiri yapo magamba mengi ambayo viongozi wengi wa CCM wanahitaji kuyavua kisha wavae mavazi mapya kama wana nia thabiti ya kuwaongoza Watanzania. Magamba wanayohitaji kuyavua ni pamoja na ukitimbakwiri wenyewe, kutokuwa na uwezo wa kuongoza, fitina, chuki binafsi, uwongo, wivu, ushirikina, uvivu wa kufikiri na ubinafsi uliojaa ndani ya fikra na mioyo yao. Wakiweza kujigambua hayo magamba niliyoyataja na kuuvaa mavazi ya uzalendo, utu wema, upendo kwa Watanzania kuliko nafsi na familia zao pekee, kumtegemea Mungu badala ya waganga, taaluma na utaalamu, weledi badala ya uwongo, ujanja ujanja na hila katika kuwaongoza Watanzania basi watakuwa wamejivua gamba na dhana nzima ya Mwenyekiti wa Taifa wa CCM, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete itakuwa na maana na tija kwa Watanzania. Tatizo la baadhi ya viongozi wa nchi hii ni kuvaa barakoa (kinyago) cha kondoo huku ndani ni mbwa mwitu wenye nia ya kuirarua Tanzania na tasilimali zake na Watanzania na rasilimali zao kwa faida yao na watoto wao bila kujali walio wengi. Viongozi wa namna hii wanafikiria nini? Au hawajui hawakuja na kitu duniani na hawatoka na kitu? Inakuwaje hata wanapohudhuria maziko ya rafiki na ndugu zao hawagundui kwamba "sanda" haina mfuko! Unajua sanda haishonewi mfuko kwa sababu mtu anapokufa hatahitaji TZS 500/= za kununulia soda njiani kuelekea ahera! Huko hakuna kiu wala njaa ni ama motoni milele ama paradiso milele! Hivi hawa hawajui haya na kama hawawezi kujua haya watawezaje kutuongoza? Mtu msafi akichafuka hatangoja kuambiwa kaoge!
anatakiwa kuvitema vyeo vyote hivyo.
Nguvu ya CCM ni wenye fedha tena fedha chafu. Wanapokomaa na Mafiga matatu ya fedha ndani ya chama chao na kutaka kuharibu, maana yake nini?
Ushindi wao utatoka wapi? Watapewa fedha na nani?
Naona CCM bila Rostam, Lowassa na Chenge ni sawa na chai bila sukari.