Kuondolewa kwa Lowassa, Chenge na RA - CCM na hatima yake na yao

Another attemp from Membe and allies! NMbopo na Sangara watafuata

teh....teh.....teh! Mbona wewe ni muoga wa mapambano! Unaogopa nini kama unaamini katika unachokisimamia? Nyie ni watu who have all along been giving asinine advice to the big man that he has a mammoth following in his ill motivated ascent to power. Those of us who were against his deeds have been vindicated by this historic event of cloughing and we are telling them that woe betide for any the evil spirits that think that they can manipulate this country as if it is "shamba la bibi".

Since good has triumphed over evil, we cannot help but rejoice. But since we know that this snake has only been rattled, we are now bracing ourselves for the fight that will eventually have it killed. Now whether what has won is what Membe stood for, is a subject for another day but what is important is that mafisadi have been stripped naked and the public is enjoying watching these gbagbos of our country facing a mushroom embarassment remiscent of an adulterer who has been caught infragrante delicto! Mr. NSSF Damu and other syconphants such as Bashe and his Habari Corporation crew should better read the signs of the times!

We will not relent in our quest for justice and Mr. NSSF Damu should better know that we are here to stay!
 
Haahahahahaaa! Wana jamiii nyie wabaya.

Mnanikumbusha enzi za utoto mnaweza kupigana ngumi kwa uchonganishi kama huu.
Msitari unachorwa na ngumi zinapigwa...........

Sasa tutaona kama walikutana barabarani au waligongana kwenye korido za guest house.
 
Tiote
inaoneka wewe ndio kilaza usio na uwezo wa kutafakari na kuelewa nachoandika
siyo lazima uoneshe ujinga wako hadharani

Kaka matusi hayajengi. Ukiona wanafunzi wako darasani wanasinzia au kupiga stori wakati wewe unafundisha darasani basi ujue hueleweki na kuwachapa hakutasaidia wao kuelewa somo. Kama ni ligi ya matusi wenzio tumekulia uswahili. Tunayajua kuliko wewe lakini hapa siyo mahali pake. Tujadili tu yaliyomkumba swahiba wako Lowassa na siyo matusi!
 
Katika CCM wanakojidai ni kujivua gamba (ambalo kimsingi hawawezi as its too late kwa gamba kuvulika) Makamba and his co-pilot members in CCM wametoswa nafasi zao........ Utamkumbuka kwa lipi Makamba, Membe, Makalla, Chiligati etc?

Binafsi japo wote walikua uozo, nitamakumbuka zaidi Makamba, uteuzi wake kwangu ulikua ni kipimo cha umakini wa kiongozi husika. Huyu mzee alikua mpayukaji zaidi ya utendaji........... Hata kwenye speech yake ya kuondoka alimwomba JK asimsahau, kukiwa na kuwajibu wapinzani matusi, yuko tayari kuwajibu kwa matusi........

Nitamkumbuka pia, akiwa RC Dar Es Salaam, alianzisha operation kamata dada zetu wajasiriamali wa miili yao......... Wale madada walieneza rumours (si mnajua Dar rumourville) kwamba Mhe. Makamba anawataka na wao hawamtaki, hivyo kamata kamata ina-hidden agenda. Kwenye press conference, Makamba alivyopigwa hilo swali, akasema, "Jamani, hivi vibinti vidogo vinasema navitaka, hivi mimi Makamba na uzee wangu wote, nitavipeleka wapi? KWA MAMA JANUARI KWENYEWE NATUMIA UZOEFU".

Huyu Mzee nitamkumbuka kwa pumba zake na kipimo cha umakini wa waliokuwa wanamchagua. No wonder ataendelea kuchaguliwa...........
 
Lowasa usitishiwe kuvuliwa gamba, coz meno yako bado yana sumu, wanajua we ni kiboko kwenye dili. hivi kweli ni mmsai? No, no sidhani. Tena ukivuliwa gamba unakuwa kijana, kama noma na iwe noma sanua na wewe magamba yao. hasa la mkuu, hata zile dili za .......???

Ambacho hamjui ni kwamba huyu siyo nyoka. Ni gamba la nyoka ambalo lina michubuko na harufu kali sana. Sasa nyoka mwenyewe kagundua kwamba kumbe linamfanya akimbiwe ndo alkalimwaga na sasa linakauka tu porini kusubiri moto wa jangani (NEC ijayo) uliteketeze ligeuke majivu. Sasa atasanua nini anachokijua? Msimponze mwenzenu akakutana na ghadhabu za watanzania.
 
Nguvu ya CCM ni wenye fedha tena fedha chafu. Wanapokomaa na Mafiga matatu ya fedha ndani ya chama chao na kutaka kuharibu, maana yake nini?

Ushindi wao utatoka wapi? Watapewa fedha na nani?

Naona CCM bila Rostam, Lowassa na Chenge ni sawa na chai bila sukari.
 
Mimi sikutaka aachie ukatibu mkuu
Pumba zake zilisaidia sana kuidhoofisha ccm na serikali kwa ujumla ikawa rahisi kwa upinzani kukubalika
 
Lowassa usikubali lazima mzame wote haiwezekani umbebee mizigo yake ya ufisadi leo ukuaibishe.
Kama vipi itisha mkutano na waandishi wa habari haraka.

Wote mlikuwa kwenye list of shame kivipi leo wewe na rostam tu.?

Mkapa anafanya nini KK

Kingunge asiongee kabisa maovu yake yapo wazi

Lowassa bora ufe naye usikubali mulikula wote
 
Lowassa usikubali lazima mzame wote haiwezekani umbebee mizigo yake ya ufisadi leo ukuaibishe.
Kama vipi itisha mkutano na waandishi wa habari haraka.

Gamba linalotakiwa kuvuliwa halimfanyi mtu kubadilika hubakia mtu huyo huyo hii ni sawa na kuoga na kutumia taulo na kisha taulo kuchafuka wakati linasafisha mwili uliooga. Hata hivyo gambaz lazima zimalizwe zote bila kupendeleana. Sasa tuene wenye ubavu
 
Usikubali kugeuzwa gamba. Gamba mana yake nini? Yaani wewe ni gamba? Leo hii umegeuka gamba? dili zote ulizopiga naye, leo anakugeuza gamba? Anakutosa? Anakutishia nyau?

Usikubali!

Ukikubali ujue umekwisha mjomba. Watakufilisi hadi mali zako ulizochuma kihalali.

Watu wengine? Mwenzie ni Rais wa JMT!!! DO U KNOW WHAT IT MEANS?
 
Namsikitikia mbunge wangu Peter Sherukamba, yeye ni mtoto wa EL na alitegemea uwaziri 2015. Kwa kumtosa EL nampa shamvu JK; sasa mahela ya Dowans yataliwa kwa mtindo gani kwani yalikusudiwa kutumiwa kuhonga wajjumbe 2015. JK kaona mchezo wao anategemea wajumbe wa NEC watokee wilayani hivyo watakuwa wengi ambao kwa kiasi fulani itakuwa vigumu kuwahonga wote. Sasa CDM ije na mbinu mpya za kupambana na mgombea CCM 2015, kwa vile makombora yaliyoandaaliwa ya UFISADI majibu yamepatikana
 
Hana jipya na mwenzake kamwaga mboga sidhan kama ana ugali wa kuumwaga akiharibu tuu watampoteza kwani system bado anayo JK

Hana ugali wala mboga huyo. Arobaini yake imefika na sasa aende huko TBC akafanye usanii wake, au arudi Monduli akaandae maandamano kama yale aliyoyafanya 2008 pale alipojitemesha mzigo, maana huyu jamaa staili yake in kama ile ya watuhumiwa wa Ocampo kule Kenya, ambao kila siku wao ni kulalama tu kwamba wanaonewa na ku-retreat kwenye makabila yao as if walipoua au wanapoiba wanakula na makabila yao.

Mara zote amekuwa akichangia kumdhoofisha rais kwa hila mbalimbali huku akijisifu kwamba hawakukutana barabarani, kumbe watu walishamchoka na sasa hata wale waliokuwa wajikalia kimya kama akina mzee Mwinyi, Msekwa, Megji, makongoro Nyerere na hata Kinana wamepaza sauti kwa staili ya bubu kusema mambo yanapomzidia. Akaanzishe chama huku na atapata wafuasi wa aina yake kama vile Serukamba, Nchimbi, Mgeja, Mahanga, Sophia Simba na huyu NSSF Damu. lakini wenye CCM yao na watanzania hawamtaki jamani!
 
Gamba linalotakiwa kuvuliwa halimfanyi mtu kubadilika hubakia mtu huyo huyo hii ni sawa na kuoga na kutumia taulo na kisha taulo kuchafuka wakati linasafisha mwili uliooga. Hata hivyo gambaz lazima zimalizwe zote bila kupendeleana. Sasa tuene wenye ubavu
Namshauri Lowassa asijiuzulu manake ccm haina cha kumfanya (Mkapa na Meghi nikashfa kibao wataongea nini?)
Lowassa akomae kama hawezi basi atengeneze mtandao ili JK atakapoondoka tu amchafue vilivyo kwani JK atakuwa hana meno.
Walikula wote hawa mabwana kivipi kutapishana?
 
Natamani nimpatie Lowassa 'benefit of doubt', ila nataka afanye yafuatayo:

  1. Akubali makosa waliyoyafanya serikalini wakati wa Richmond scandal na kwamba alijiuzulu kwa hilo. Awaombe Watanzania msamaha.
  2. Akubali ufisadi walioufanya wakati wa mchakato wa kumtafuta mgombea urais kwa tiketi ya CCM mwaka 2005. Awaombe Watanzania msamaha.
  3. Awatake wenzie, pamoja na Rais Kikwete, wakiri makosa na waombe msamaha. Awatake wale wote ambao bado hawajajiuzulu nafasi zao za kiuongozi, wafanye hivyo ili kuwajibika.
  4. Akubali kuwa kutokukiri makosa haya mapema na kuomba msamaha ni udhaifu wa kibinadamu tu.
Akifanya hivi Lowassa nitampatia 'benefit of doubt'. Baada ya kukiri makosa na kuomba msamaha itakuwa juu ya Watanzania wenyewe kusamehe ama vinginevyo.
 
Ukweli Lowassa komaa mwanangu! Kamwaga mboga mwaga ugali, la sivyo omba hifadhi ya kisiasa nchi nyingine kwani kifuatayo itakuwa mbaya kwako.
 
Usikubali kugeuzwa gamba. Gamba mana yake nini? Yaani wewe ni gamba? Leo hii umegeuka gamba? dili zote ulizopiga naye, leo anakugeuza gamba? Anakutosa? Anakutishia nyau?

Usikubali!

Ukikubali ujue umekwisha mjomba. Watakufilisi hadi mali zako ulizochuma kihalali.

Nimefurahia post yako!!! content yake kubwa sana, you can produce volume of books and poems!!
 
Hivi kuna lolote la kushangilia usanii unaoendelea CCM? Hivi hawa Ra,El na Chenge wapo serikalini siku hizi? Ndio wameshindwa mshauri rais na maisha ya watanzania kuwa magumu kiasi hiki? Ndio wameleta rasimu mbovu ya Katiba bungeni? Hivi hawa wakifukuzwa CCM, Tanzania itakua nchi ya maziwa na asali?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom