Kuondolewa kwa Lowassa, Chenge na RA - CCM na hatima yake na yao

SON OF DAVID

Member
Apr 1, 2011
42
3
Kuna wale wanajf wanaotoa thread kibao za kuonesha kuwa LOWASA ni Rais wa TZ 2015 mmeingia mtini? Naona swahiba wake jk kamfungia vioo Dodoma. Kapewa siku 90 kujiondoa kwenye NEC. Yeye na Rostam na Chenge nk.
Maneno yalikuwa mengi sana. Mara fedha zimekusanywa, ooh mtandao tayari, ooh zitto wa Chadema atawaunga mkono kwa kujiunga NCCR kupunguza kura za Chadema, nk. Hebu njooni na thread zenu tuwasikie tena safari hii. Au mmefyata mkia sasa?
Au mfahamukuwa watanzania sasa mmeamka?
 
Kikwete amtakasa Rostam, ASEMA NI MTU SAFI ALIYEENEA KAMA TIMU YA MPIRA

Saturday, 02 October 2010 07:11

jkrostam.jpg


Ibrahim Bakari, Igunga
MGOMBEA urais kwa tiketi ya CCM, Jakaya Kikwete amemsifu mweka hazina wa zamani wa chama hicho, Rostam Aziz kuwa ni mtu safi na aliyeenea kila sehemu.Kikwete alisemna hayo wakati akimtambulisha Rostam, ambaye anatetea kiti chake kwenye Jimbo la Igunga ambako amekuwa mbunge tangu mwaka 1995.



Kikwete: Lowassa ni msafi, alisingiziwa!

Baada ya kumpigia kampeni BAsil Mramba Rombo, JK saa Katika kampeni zake za mkoani Arusha anaelekea Monduli atakapomnadi na kufanya mazungumzo ya faragha na Lowassa

wtcoj.jpg







Lowassa: Hakuna wa kunivuruga na Kikwete
• "Hatukukutana barabarani, na watu hawawezi kutuvuruga barabarani."

na Mwandishi Wetu



WAZIRI Mkuu mstaafu na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, amesema uhusiano imara wa kisiasa na kikazi alioujenga kwa miaka mingi na Rais Jakaya Kikwete, hauwezi kuvurugwa na jitihada za kikundi kidogo cha watu wenye nia mbaya.

Lowassa alitoa kauli hiyo ofisini kwake jijini Dar es Salaam jana wakati alipofanya mahojiano ya ana kwa ana na Tanzania Daima Jumatano.

‘‘Huyu bwana mkubwa (Rais Kikwete), hatukukutana barabarani, na watu hawawezi kutuvuruga barabarani,” alisisitiza Lowassa, wakati alipotakiwa kueleza iwapo ni kweli amejipanga kusaka urais wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwakani.

SOurce:Lowassa: Hakuna wa kunivuruga na Kikwete
.
 
Kuna wale wanajf wanaotoa thread kibao za kuonesha kuwa LOWASA ni Rais wa TZ 2015 mmeingia mtini? Naona swahiba wake jk kamfungia vioo Dodoma. Kapewa siku 90 kujiondoa kwenye NEC. Yeye na Rostam na Chenge nk.
Maneno yalikuwa mengi sana. Mara fedha zimekusanywa, ooh mtandao tayari, ooh zitto wa Chadema atawaunga mkono kwa kujiunga NCCR kupunguza kura za Chadema, nk. Hebu njooni na thread zenu tuwasikie tena safari hii. Au mmefyata mkia sasa?
Au mfahamukuwa watanzania sasa mmeamka?

Another attemp from Membe and allies! NMbopo na Sangara watafuata
 
Kuna wale wanajf wanaotoa thread kibao za kuonesha kuwa LOWASA ni Rais wa TZ 2015 mmeingia mtini? Naona swahiba wake jk kamfungia vioo Dodoma. Kapewa siku 90 kujiondoa kwenye NEC. Yeye na Rostam na Chenge nk.
Maneno yalikuwa mengi sana. Mara fedha zimekusanywa, ooh mtandao tayari, ooh zitto wa Chadema atawaunga mkono kwa kujiunga NCCR kupunguza kura za Chadema, nk. Hebu njooni na thread zenu tuwasikie tena safari hii. Au mmefyata mkia sasa?
Au mfahamukuwa watanzania sasa mmeamka?


another idiot from Membe,uvccm crual
 




*Wengine wadai yalichelewa, uchafu umeganda
*Baadhi wasema ni ndio mwarobani wa ufisadi
*Yusuf Makamba afurahia kuondoka na wengi


Na John Daniel na Chales Masyeba

SIKU moja baada ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kutangaza rasmi mabadiliko makubwa katika safu yake ya uongozi, kwa kujiuzulu sekretarieti na Kamati Kuu yake, wananchi wametoa maoni tofauti huku wengi wakitaka mabadiliko hayo yaendelee hadi serikalini.

Wakizungumza na Majira kwa nyakati tofauti jana, wananchi hao walisema licha ya mabadiliko hayo kulenga kuleta mabadiliko ndani ya CCM lakini hatua hiyo imechelewa kuchukuliwa, hadi kukifanya chama hicho kukosa mvuta kwa wananchi.

Miongoni mwa walitoa maoni ni aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Bw. Yusuph Makamba ambaye amewataka Watanzania na wanachama wa CCM wasifadhaike kwa kujiuzulu kwao kwani 'wanarudi kwa baba ambaye amewaletea mtume mwingine'.

Mbali na hilo, Bw. Makamba alionesha furaha yake kwa kutowajibika peke yape, bali ukawa ni mkumbo wa wengi.

“Nashukuru tumetoka wote, kama tulivyoingia pamoja na tunatoka pamoja tukiwa wamoja. Haiwezekani mmoja anyoshewe kidole. Hata baadhi ya wajumbe wa mkutano huu walisema atoke Makamba, mimi nikasema tutoke wote”.

Bw. Makamba aliyasema hayo alipopewa fulsa ya kuaga kwa niaba ya wajumbe wenzake wa sekretarieti iliyojiuzulu majuzi, huku akishangiliwa na wajumbe wa halmashauri kuu ya taifa katika ukumbi wa NEC maarufu mjini Dodoma.

Kutokana hatua hiyo, Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho imewateau Bw. Wilson Mukama amechaguliwa kuwa Katibu Mkuu, nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Bw. Makamba, akisaidiwa na Naibu Makatibu Wakuu (Bara na Visiwani), Bw. John Chiligati na Bw. Vuai Ali Vuai. Katibu mpya wa Itikadi na Uenezi ni Bw. Nape Nnauye, huku, Bw. Mwigulu Mchemba akichaguliwa kuongoza Idara ya Fedha na Uchumi. Mkuu wa Oganaizesheni ni Bi. Asha Abdallah Juma na Katibu wa Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Bw. Januari Makamba.

Kwa kutumia misemo ya biblia, Bw. Makamba alisema wanarudi kwa baba yao kutayarisha makao mapya na hata wenzao waliokuja na kukalia viti walivyoviacha watawakuta huko.

"Baba ameleta mfariji mwingine ambaye ni Wilson Mukama na wajumbe wengine. Wanachama tuendelee kuvumiliana na kujipanga ili kupata ushindi mkubwa mwaka 2015.

"Tulipoteuliwa tuliaminiwa kufanya kazi za chama na tukafanya kazi hizo kikamilifu na chama kikapata ushindi. Ndiyo, tulishinda hata kama ni kwa namna gani, lakini tulishinda, alisema.

Alisema wao wamekubali kumwaga damu kuokoa chama, kwani hawana tofauti sana na waliobaki na kwamba amefurahi kuona wengine nao wakichukua nafasi zao na kuwaasa kwamba wakitaka kutumia fagio la zamani wao wako tayari wakati wote, lakini wasipolihitaji wakiharibu watawasema.

Akizungumzia hulka ya yake ya kauli za kuudhi, alisema kwa mifano na kusisitiza kuwa kama unatukanwa na mtu mdogo aliyetumwa na mtu mzima ili kuweka mambo sawa, na yeye anamtukana kwa lengo la kusawazisha ili iwe sare.

Mkazi mwingine wa Dar es Salaam alisema, "Chama ni watu na watu ndio wanakuwa na mapungufu, kama mapungufu yao yameonekana ni vizuri waondoke kabisa, alisema akifurahia uamuzi huo wa CCM.

Aliongeza: "Suala la ufisadi upo na siyo siri, fisadi si lazima yeye achukue hela, lakini anaweza kumsaidia mtu mwingine kupata hizo hela, huo pia ni ufiasadi, kama wamepewa muda wa kuondoka wenyewe wafanye haraka wasije wakaahibishwa," alisema Bw, Ashrif Khan, aliyejitaja kama kada wa CCM.

Alisema kumekuwepo na malalamiko mbalimbali ndani ya chama hicho na kwamba hatua ya kuwaondoa watendaji hao na kupanga upya safu ni moja kati ya taratibu za CCM.

"Hatua iliyochukuliwa ni sawa kabisa na kuheshimu maoni ya wananchi, kama chama kikiona kinakwenda vibaya ni lazima irudi kwenye kati na kanuni zake," alisema.

Alisema hatu hiyo inatoa nafasi kwa walioteuliwa kuwa makini na kutothubutu kurudia makosa huku akisisitiza umuhimu wa wana-CCM kurejea itikadi za chama hicho.

Kwa upande wake Bw. Raymond Talawa, mkazi wa Kinyerezi Dar es Salaam licha ya kupongeza mabadiliko hayo alisema yamechelewa kufanywa kwa kuwa mapungufu ya kiutenaji ndani ya CCM yalianza mapema mwaka 20067/2008

"Kama hao akina Makamba wameondolewa na mafisadi wengine wamepewa muda kujiondoa wenyewe, basi hata wale wafanyakazi wazembe serikalini nao waondolewe haraka," alisma.

Alisema kumekuwa na wizi wa fedha za umma zinazotolewa na serikali kwa ajili ya miradi mbalimbali lakini wahusika wanahamishwa badala ya kuondolewa kama ilivyofanywa na CCM.

Naye Bi. Rehema Abdala, wa Kimara alisema amefarijika kwa mabadiliko hayo japo hatua hiyo imechelewa kufikiwa na kusababisha madhara makubwa kwa CCM.

"Itabidi CCM ifanye kazi kubwa kurudisha imani iliyopotea, lakini wamefanya vizuri," alisema Bi. Abdallah bila kutoa ufafanuzi wa kina.

Wananchi wengi walionyesha wazi kufurahishwa na hatu ya mabadiliko hayo huku wakisisitiza umuhimu wa Rais Jakaya Kikwete, kuelekeza nguvu kama hizo kwa baadhi ya watendaji wa serikali wazembe na wala rushwa badala ya kuishia kwenye chama.

"Ujenzi wa shule, barabara na huduma za wananchi zinaishia njiani kutokana na watendaji wa serikali wala rushwa na wazembe, rais angefanya kama alivyofanya kwa CCM kuwaondoa,"alisema mmoja wa walimu wa Chuo cha Uongozi wa Fedha IFM na kuomba jina lake kutotajwa.
 
Hawa wanayo pesa ya kuweza kuwanunua 2/3 ya wajumbe wa mkutano mkuu wa chama chao. 2012 Dodoma hapatatosha!
 
another idiot from Membe,uvccm crual

Whatever that means (in red). It tells how confused you Lowassa disciples are lost and dejected and I can really feel for you. But whether these are Membe's ****** or whoever else's ******, your man has been dealt a severe blow and it confirms what people have been saying about how sunken in dirt your 'god' finds himself and your laundry mission is all but a wasted effort. People's jubilation of what has just happened in Dodoma only confirms that no amount of ill gotten fortune will make his realise his burning desire for ascending to the helm.

Kwa ufupi jamaa amekuwa-caught pants down na recovery is almost an impossibility.
 
Aaaah! Wapi, wapambe wenyewe njaa kali, sasahv wameanza kuusoma mchezo watatoka nduki muda c mrefu, ukiwauliza mmoja mmoja utasikia wanasema hata mi simpendi ila basi tu nina kiu na njaa na msha ndo ananiweka hewani.
 
MAGAMBA mengine ya wana CCM ni ngozi ya mnyama aitwae FISADI anayepatikana kwenye Hifadhi itwayo CCM hivyo hayo magamba hayavuuki ovyo lazima yatatoa harufu mbaya maana hayo MAGAMBA huvalishwa mwana CCM gamba likiwa bado bichi. Haaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa! Lo! Patamu sana hapo. Naona MAFISADI PEMBE ZAO ZIMEANZA KUYEYUKA.
 
Usikubali kugeuzwa gamba. Gamba mana yake nini? Yaani wewe ni gamba? Leo hii umegeuka gamba? dili zote ulizopiga naye, leo anakugeuza gamba? Anakutosa? Anakutishia nyau?

Usikubali!

Ukikubali ujue umekwisha mjomba. Watakufilisi hadi mali zako ulizochuma kihalali.
 
Hivi mimi najiuliza kwani kuna dhambi gani kuunga mkono harakati za Membe kama ambavyo wengine wana uhuru wa kuunga mkono watarajiwa wengine? Bahati mbaya ni kwamba Membe ameshakanusha kwamba hagombei lakini kama anavyovisimamia vinavutia watu basi ni haki yao kuunga mkono. Lakini awepo au asiwepo kwenye harakati hizo, ukweli unabaki kwamba wako wanaofurahishwa na kuchukizwa na mwenendo wa Lowassa na wala siyo dhambi kwa mtu kueleza hisia au maoni yake, kama huyo NSSF Damu, ambaye tunajua naye amekuwa akijivua gamba kila siku toka kuitwa Game Theory au GT na majina mengine kibao. Why should one take support for Membe as something treasonable or highly offensive.

Mwanzilishi wa thread ameeleza yale aliyofikiria kwamba ndiyo consequences au predicaments zinazomkabili Lowassa baada ya maamuzi ya CC na NEC then waumini wake wanaanza kumwaga matusi. Mlionywa humu ndani kwamba utakaso wenu kwa huyu bwana ni kuvuna maji kwa pakacha mkadhani ni utani kumbe sasa arobaini yenu inakaribia na hayo matusi kwa Mbopo au Sangara na last kicks of the dying horse.
 
Kikwete amtakasa Rostam, ASEMA NI MTU SAFI ALIYEENEA KAMA TIMU YA MPIRA

Saturday, 02 October 2010 07:11

jkrostam.jpg


Ibrahim Bakari, Igunga
MGOMBEA urais kwa tiketi ya CCM, Jakaya Kikwete amemsifu mweka hazina wa zamani wa chama hicho, Rostam Aziz kuwa ni mtu safi na aliyeenea kila sehemu.Kikwete alisemna hayo wakati akimtambulisha Rostam, ambaye anatetea kiti chake kwenye Jimbo la Igunga ambako amekuwa mbunge tangu mwaka 1995.



Kikwete: Lowassa ni msafi, alisingiziwa!









Lowassa: Hakuna wa kunivuruga na Kikwete
• "Hatukukutana barabarani, na watu hawawezi kutuvuruga barabarani."

na Mwandishi Wetu



WAZIRI Mkuu mstaafu na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, amesema uhusiano imara wa kisiasa na kikazi alioujenga kwa miaka mingi na Rais Jakaya Kikwete, hauwezi kuvurugwa na jitihada za kikundi kidogo cha watu wenye nia mbaya.

Lowassa alitoa kauli hiyo ofisini kwake jijini Dar es Salaam jana wakati alipofanya mahojiano ya ana kwa ana na Tanzania Daima Jumatano.

'‘Huyu bwana mkubwa (Rais Kikwete), hatukukutana barabarani, na watu hawawezi kutuvuruga barabarani," alisisitiza Lowassa, wakati alipotakiwa kueleza iwapo ni kweli amejipanga kusaka urais wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwakani.

SOurce:Lowassa: Hakuna wa kunivuruga na Kikwete
.

hapo kwenye nyekundu alijibuje?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom