Kuondoka ccm na kuingia chadema SIO mwisho wa matatizo. Bali ni mwanzo wa maangamizo mapya

Malaria Sugu

JF-Expert Member
Jul 7, 2009
2,653
264
Wakati wa Kenya wanamuondosha kwa furaha Rais mstaafu Daniel arap Moi na kudhani ndio kikwazo cha maisha yao. vumbi la machafuko liliikumba baada mpinzani wake ambae ni rais wa sasa Kuvuruga amani na kukataa kuondoka madarakani hadi kusababisha vita.

Lkn pia kwa upande wa Zambia baada ya kumuondosha Keneth kaunda na kuja mpinzani Fedrik Chiluba hali ya maisha imezidi kuwa ngumu, na mpizani huyo wa Dk Kaunda amefikishwa mahakamani kwa rushwa.
Malawi nako hali sio shwari.

Lkn nako znz baada ya Cuf kuingizwa ktk madaraka, waznz wanalalamikia hali mbaya ya maisha.
kwa mfano mchele mbovu uliokuwa unalalamikiwa na CUF kabla ya kuingia madarakani sasa unauzwa kwa bei ya juu huku waziri wa Cuf wa biashara hajui nini afanye.ile ahadi ya kuigeuza zenj kuwa kisiwa cha biasha imekuwa kama hadithi ya kuku na watoto
hali ya wizara ya afya chini ya Mh Juma duni imezidi kuwa mbaya kuliko hata utawala wa ccm pekee.
 
Tatizo watu wakishashika madaraka wanajisahau sana mtu umeomba kura kwa sera watu wakakukubali, wakakupigia kura "umepita" lakini ukishafika huko tu basi unasahau kabisa vilio vya wananchi na matakwa ya wananchi hii inakera sana. Haya sasa cuf iliingia kwa mbwembwe za michele mibovu itadhibiti lakini leo yale yale mchele bado upo madukani na isitoshe unauzwa kwa bei kubwa hii mbaya sana. Basi tunapowaweka madarakani wasibweteke jamani!!! saidia wananchi hacha kusaka maslahi yako binafsi.
 
In fact ningekushauri ubadili hata jina kwa sababu hoja sijaiona hapa bali nimeona maneno ya kuwatisha watanzania ili wasikubali mabadiliko bali waridhike na walicho nacho japo hakifai. Usitudanganye, Moi hakuondolewa.

Katika uchaguzi wa mwaka 2002, Moi hakung'olewa madarakani kwa sababu hakugombea. Aliyegombea kwa ticket ya TANU wakati ule alikuwa uhuru Kenyata na hata baada ya uchaguzi vurugu hazikutokea.

Vurugu zilitokea baada ya uchaguzi wa mwaka 2007. Hali ya maisha kuwa ngumu Zambia imesababishwa na kupungua kwa matumizi ya shaba.

By the way, Kaunda is responsible kwa sababu hakuweka mazingira ya uchumi mbadala pale ambapo shaba ingekuwa haina thamani. Pia mabadiliko ya hali ya hewa yalichangia kuporomoka kwa uchumi wa Zambia. Mimi nadhani kwa resources walizo nazo malawi ukilinganisha na zile tulizo nazo sisi, Malawi wanafanya vizuri.

Hata timu yao ya mpira wa miguu iko juu. Mikoa ya kusini hasa Songea na mbeya wananunua sukari ya malawi, japo sisi tuna eneo zuri lenye rutubwa na kubwa la kulima miwa kuliko wao.

Tatizo kubwa la Serekali ya CCM ni kuwa, haina wabunifu, nadhani baada ya miaka kumi hivi Dar es Salaam itakuwa the biggest slum in Africa. Hata nchi masikini kama Ethiopia wanajenga apartments sisi bado tunajenga kwenye viwanja vya 20*20m.

Wamejijengea mtindo wa kulindana. Mtu hata serekalini anapata ajira kwa sababu ya kujuana na wala si kwa vile ana uwezo. Kwa hiyo tukiendelea na CCM, tusitegemee jipya.
 
Ndugu CUF haiongozi zanzibar bali ccm na Rais wao mbovu,mada yako nzuri sisi tunataka watu watakao itumikia nchi kwa uaminifu hata chadema wakishindwa tutawatoa kama ambavyo tunaitoa ccm 2015
 
Acha kutupumbaza na Hoja Yako isiyo na Mashiko!! Justification ya Hoja yako ni Kuwa waafrika Hatuwezi Chochote kitu ambacho Si kweli!! We need change, Acha Blaablaa hapa, Hukuna research ambayo inaonyesha waafrika Tumeshindwa ila watawala ndio wameshindwa!!
 
Mambo bado ,mbona mna halaka,hivi ni nani mtawala huko Zanzibar ? Sasa mnalaumu anaelipa mshahara wakati hela anazuia tajiri,nyie vipi ?
 
Ndio nakubali, lakini ni mwanzo wa kutatua matatizo. Ni kweli watayakuta maana ccm haina jipya mpaka itakapoondoka.:yield:
 
Kwa Tanzania dawa ni kuibadilisha CCM, si kuwajaribu cdm ambao taalum zao ni hasi...
 
Asante mwanaforum kwa kuliona hilo. Nadhani huyu bwana anataka kufananisha kifo na usingizi which is not valid. lkn hayo ndo mawazo ya mafisadi. Nitamshangaa sana, hadi kuzirai kama mtoa hoja atakuwa kijana.
 
in fact ningekushauri ubadili hata jina kwa sababu hoja sijaiona hapa bali nimeona maneno ya kuwatisha watanzania ili wasikubali mabadiliko bali waridhike na walicho nacho japo hakifai. Usitudanganye, moi hakuondolewa.

Katika uchaguzi wa mwaka 2002, moi hakung'olewa madarakani kwa sababu hakugombea. Aliyegombea kwa ticket ya tanu wakati ule alikuwa uhuru kenyata na hata baada ya uchaguzi vurugu hazikutokea.

Vurugu zilitokea baada ya uchaguzi wa mwaka 2007. Hali ya maisha kuwa ngumu zambia imesababishwa na kupungua kwa matumizi ya shaba.

By the way, kaunda is responsible kwa sababu hakuweka mazingira ya uchumi mbadala pale ambapo shaba ingekuwa haina thamani. Pia mabadiliko ya hali ya hewa yalichangia kuporomoka kwa uchumi wa zambia. Mimi nadhani kwa resources walizo nazo malawi ukilinganisha na zile tulizo nazo sisi, malawi wanafanya vizuri.

Hata timu yao ya mpira wa miguu iko juu. Mikoa ya kusini hasa songea na mbeya wananunua sukari ya malawi, japo sisi tuna eneo zuri lenye rutubwa na kubwa la kulima miwa kuliko wao.

Tatizo kubwa la serekali ya ccm ni kuwa, haina wabunifu, nadhani baada ya miaka kumi hivi dar es salaam itakuwa the biggest slum in africa. Hata nchi masikini kama ethiopia wanajenga apartments sisi bado tunajenga kwenye viwanja vya 20*20m.

Wamejijengea mtindo wa kulindana. Mtu hata serekalini anapata ajira kwa sababu ya kujuana na wala si kwa vile ana uwezo. Kwa hiyo tukiendelea na ccm, tusitegemee jipya.

kweli nahavache huyo kada wa magamba anataka kuturudisha nyuma. Hampati mtu, watz wanauelewa sana siku hizi. Tz ni tajiri sana ukiuondoa ufisadi TU na na nchi iwe na uongozi bora chini ya katiba mpya utamalaki.
 
Tatizo watu wakishashika madaraka wanajisahau sana mtu umeomba kura kwa sera watu wakakukubali, wakakupigia kura "umepita" lakini ukishafika huko tu basi unasahau kabisa vilio vya wananchi na matakwa ya wananchi hii inakera sana. Haya sasa cuf iliingia kwa mbwembwe za michele mibovu itadhibiti lakini leo yale yale mchele bado upo madukani na isitoshe unauzwa kwa bei kubwa hii mbaya sana. Basi tunapowaweka madarakani wasibweteke jamani!!! saidia wananchi hacha kusaka maslahi yako binafsi.

[/People change when they become presidents - Gerald Ford]

It is about systems in place and not people.
 
Wakati wa Kenya wanamuondosha kwa furaha Rais mstaafu Daniel arap Moi na kudhani ndio kikwazo cha maisha yao. vumbi la machafuko liliikumba baada mpinzani wake ambae ni rais wa sasa Kuvuruga amani na kukataa kuondoka madarakani hadi kusababisha vita.

Lkn pia kwa upande wa Zambia baada ya kumuondosha Keneth kaunda na kuja mpinzani Fedrik Chiluba hali ya maisha imezidi kuwa ngumu, na mpizani huyo wa Dk Kaunda amefikishwa mahakamani kwa rushwa.
Malawi nako hali sio shwari.

Lkn nako znz baada ya Cuf kuingizwa ktk madaraka, waznz wanalalamikia hali mbaya ya maisha.
kwa mfano mchele mbovu uliokuwa unalalamikiwa na CUF kabla ya kuingia madarakani sasa unauzwa kwa bei ya juu huku waziri wa Cuf wa biashara hajui nini afanye.ile ahadi ya kuigeuza zenj kuwa kisiwa cha biasha imekuwa kama hadithi ya kuku na watoto
hali ya wizara ya afya chini ya Mh Juma duni imezidi kuwa mbaya kuliko hata utawala wa ccm pekee.

Naanza kuamini sasa yale maneno ya MWALIMU NYERERE kuwa ' bila CCM imara nchi itayumba'.
 
Back
Top Bottom