Kuona vitu vilivyopotea na mwizi aliechukua

Ukienda kwa hawa jamaa wanakuinitiate utaandamwa na matukio haya mfululizo na suluhisho litakuwa ni kuwafuata wao mwisho wa siku utajikuta bila kitu! Wabaya sana hawa ni NGUVU ZA GIZA.
 
Ni PM nikuelekeze mahali napajua utapata huduma hiyo. Andaa kwanza 50,000 nitakupa namba ya m-pesa
 
hiyo ni zuga tu ya madawa ya kulevya yaletayo maruweruwe kichwani.
wala sikushauri ndugu yangu.

Nilipomaliza fomu 4
nilikuwa nafanya kazi ya kumsaidia MGANGA wa Kienyeji aliyejulikana kwa jina la Omari , alinifundisha mambo mengi sana, hasa ya kitapeli, aliweza kumtapeli mama mmoja shilingi Laki nne - alichokifanya ni kumweleza ugumu wa matatizo yake kwa kuwasha Moto kwa njia ya kuchanganya LIQUID moja na POWDER. Chemical zote hizo ni COMMON lakini kwa mtu asiyejua kama yule mama angeona ni muujiza na kwamba matatizo yake ni makubwa.

hivyo hela inatafutwa kwa njia nyingi ndugu yangu

Hayo mambo ndio yanaitwa ushirikina, hayana ukweli wowote. Pahala ambapo ungeweza kusaidiwa ni polisi lakini sikushauri kwa sababu na wao waliibiwa mishahara yao wako kwenye juhudi za kujisaidia ili waweze kuishi. Watakutoa upepo utabaki mkavu na vitu vyako hutaviona! Nakushauri we endelea kumwomba mungu na uongeze juhudi za kazi utapata vingine kama hivyo na zaidi
 
Tukiacha mambo ya kuonyesha vilivyoibiwa, vipi kuhusu kunasishana wagoni kama wale wa Temeke??

Wapi wanatoa hiyo huduma?
 
hiyo ni zuga tu ya madawa ya kulevya yaletayo maruweruwe kichwani.
wala sikushauri ndugu yangu.

Nilipomaliza fomu 4
nilikuwa nafanya kazi ya kumsaidia MGANGA wa Kienyeji aliyejulikana kwa jina la Omari , alinifundisha mambo mengi sana, hasa ya kitapeli, aliweza kumtapeli mama mmoja shilingi Laki nne - alichokifanya ni kumweleza ugumu wa matatizo yake kwa kuwasha Moto kwa njia ya kuchanganya LIQUID moja na POWDER. Chemical zote hizo ni COMMON lakini kwa mtu asiyejua kama yule mama angeona ni muujiza na kwamba matatizo yake ni makubwa.

hivyo hela inatafutwa kwa njia nyingi ndugu yangu

Kwa hiyo na wewe ni Mganga?
 
Jamani mimi ni muhanga wa kuibiwa kwa kweli ni karibu mwaka sasa umepita kuna mwizi alivunja gari na kuondoka na vitu muhimu sana sasa kila mahali na kila ninayemuhadithia anasema ni kwamba ni mchoro uliochorwa na mtu aliye karibu na mimi sasa bila kuzunguka maneno nasiikia kuna waganga wana tv ya asili ambayo inaonyesha tukio zima lilivyofanyika naomba mtu anejua sehemu nzuri ya kupata huduma hii na yenye uhakika anijuze na pia kama kuna madhara ya kuangalia iyo tv niambie najua humu kuna watu washa experience kuibiwa vitu muhimu

Yaani wewe mwenyewe unajiita Muhanga, halafu unataka usaidiwe, msaada wa nini sasa kwa mabo ya kujitakia?
Tafuta maana ya neno hilo 'muhanga' utaona ulivyojichanganya.

Sikupi pole mpaka urekebishe kauli.
 
ni imani tu, mie niliwai kuibiwa, cha kwanza nilienda polisi kutowa ripoti na siku ya pili yake nikaelekezwa kwa mzee mmoja magomeni mapipa, akaniuliza siku ngapi zimepita toka uibiwe, nikamwambia ni jana tu, akasema vitu vyako utavipata, ajanipa dawa wala nini,siku ya iliyofuata polisi wananipigia simu kwamba mwizi ameenda polisi kujisalimisha na vitu vyangu vyote. sasa sijui mkwala wa huyo dingi ama nini,

yapili niliwai kuibiwa spea dukani kwangu, mwizi aliiba turbo, nikasema ngoja niende tena kwa huyo mdingi, kilichofuata siku ya pili tumeikuta turbo imewekwa nje ya duka, mdingi ajanipa dawa yoyote ninywe wala chochote sijui nifanye nini.

Naomba unielekeze huyo mzee wa magomeni mapipa anapatikanaje!
 
...Napenda kuamini kuwa kuna mahali wapo wazee wetu wana Utaalamu huu. Tatizo ni sisi Kutojitambua, Kudharauliana na kutokuwa Watafiti. Akija hapa mzungu akafanya utafiti na akagundua kuwa inawezekana utashangaa tutakavyompapatikia mzungu badala ya yule mzee wetu alyefanyiwa utafiti na huyo mzungu na kudhibitisha kuwa inawezekana...!
 
I see,

Kama akina toboa tobo wanaweza kufanya hivi, si zaidi kwa yeye aliye waumba?Mungu Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo? Guys, Mungu ni kila kitu jamani. haijalishi ulipoteza nini na wapi na lini, hana limitations endapo utamwendea. Anaweza yote ni uhakika na hana longo longo.

Ushuhuda wangu;
Mimi na rafiki yangu last year tulipoteza pesa milioni kumi na sita (16.0m). Kuna jamaa ambaye alikuwa mshikaji wa karibu sana tulimpa akalipie gharama za kutoa magari bandarini, wakati ule wakipokea pesa taslimu (cash). Jamaa alipotea nazo moja kwa moja hatukumuona tena. Nilitoa taarifa polisi nikawa na RB nikamuachia Mungu a shughulike nalo. Nilimwomba Mungu kuanzia mwezi wa tano this year 2012 (japo nilichelewa kuanza). Mwezi juni tumemkamata na hati ya nyumba yake tunayo na kesi inaendelea mahakamani, na mwelekeo ni ushindi tu, we are going to sell the house and recover our money back. Ina maana ningeanza mapema, ningepata mapema zaidi. Kila jambo limtokealo mtu hutokea kwa sababu, there is never accident all are planned in the spirits. God comes in response to prayer, and when he comes he take care of business. It is illegal for God to do any thing to humanity, communities, nations until some one pray. Prayer give God right to act upon humanity. Because he created the earth and gave it to man and man through high treason in Eden gave it to satan. God is a God of protocol, he respect his own rules.

Jamani Mungu hashindwi kitu, hakuna jambo gumu mbele zake mwendeeni. Waganga ni watumishi wa shetani, kwenda kwa mganga ni kujiunganisha shetani bila kujua ni laana na ni chukizo mbele za Mungu.

Ushauri wangu, Mrudieni Mungu, maana hakuna jambo asiloliweza hata moja.
 
mimi nina bibi yangu ni noma weka mawasiliano yako tukupigie tukuelekeze jinsi ya kufanya kama watu awajawa vichaa, uchawi upo mtu asikuambie
 
Jamani mimi ni muhanga wa kuibiwa kwa kweli ni karibu mwaka sasa umepita kuna mwizi alivunja gari na kuondoka na vitu muhimu sana sasa kila mahali na kila ninayemuhadithia anasema ni kwamba ni mchoro uliochorwa na mtu aliye karibu na mimi sasa bila kuzunguka maneno nasiikia kuna waganga wana tv ya asili ambayo inaonyesha tukio zima lilivyofanyika naomba mtu anejua sehemu nzuri ya kupata huduma hii na yenye uhakika anijuze na pia kama kuna madhara ya kuangalia iyo tv niambie najua humu kuna watu washa experience kuibiwa vitu muhimu

Mm nakushauri shika Imani yako, km Roho yako ilipona basi iepushe na maangamiz maana ktk hio tv waweza pata ambacho hukutarajia.
Hivi yawezekanaje kutafuta habari za waliohai kwa wafu?!!!
 
Ndg yangu achana na mambo ya kwa waganga,waganga wenyewe wanasaka hela.wale ni wataalamu vibaya mno kucheza na akili za watu,psychology ya matatizo ya watu wanaijua fika.utaliwa hela yako bure tu.usije ukawa km aliyeenda kwa mganga akamwambia mzee kuna jamaa ananidai elf 20 nataka asahau kabisa.mganga akamwambia toa elf 50 tu hyo kazi ndogo kwangu
 
leta 100,000/- nikupe huduma hiyo, mbona rahisi tu wewe lete pesa uone mambo mazito, hayo mambo madogo.
mwizi atakuletea mwenyewe huku akilia, maana nitapisha hukumu ambayo ww hujui ila utaijua ukileta pesa but it shld be paid thru airtel money
 
Toa huduma kwanza, then ikifanikiwa utalipwa zaid ya hiyo
 
Back
Top Bottom