Kuomba kura wakati wewe hujajiandikisha

mkirua vunjo

Member
Nov 11, 2011
25
5
Jamani naona kweli kwa upande wangu ni kichekesho kikubwa sana, inakuwaje mtu uombe upigiwe kura wakati wewe mwenyewe hujajiandikisha!
Naomba ma great thinkers mjaribu kuangalia hili.
Ni kwamba Mgombea wa CCM Arumeru Sioi Sumari hajajiandikisha kupiga kura popote Tanzania, sasa leo anakuja kuomba kura, hii inakuwaje
 
Kwani nchi hii inaruhusu uraia wa nchi mbili???endapo amejiandikishia Kenya hakika sio Rai wa Tanzania na kama ni Rai basi aliidanganya Serikali ya Kenya yaani ali temper na documents/facts, hafai kuwa kiongozi.

Lakini kwa watu makini, kitendo cha yeye kuomba kura ilhali hakujiandikisha katika eneo hilo, ni ishara tosha kuwa mtu huyo si mwenzao, ni mtu asiyejari sio tu mustakabali wa wana Arumeru, bali hajali hata mustakabali wa Taifa. Hafai pia kwa kigezo hicho.
 
Nasikia jamaa ni Mamluki wa Kenya hivyo pengine amejiandikisha Kisumu au Nairobi kupiga kura hiyo ndio bongo bwana!!!!
 
Ni ujinga wa wapiga kura kama watampa hizo kura aziombazo hii inamaana asingempigia kura mgombea wa ccm kama asingeshinda kura za maoni jamani hata hili nalo haliwafumbui macho watanzania kwamba mambo ya ccm ni valuvalu?
 
kaka hii ni hoja nzito sana,hebu iwekee heading ya moja kwa moja ili watu wasiipite,SUMARI KUOMBA KURA WAKATI HAJAJIANDIKISHA
 
Jamani naona kweli kwa upande wangu ni kichekesho kikubwa sana, inakuwaje mtu uombe upigiwe kura wakati wewe mwenyewe hujajiandikisha!
Naomba ma great thinkers mjaribu kuangalia hili.
Ni kwamba Mgombea wa CCM Arumeru Sioi Sumari hajajiandikisha kupiga kura popote Tanzania, sasa leo anakuja kuomba kura, hii inakuwajie

Jamani sasa siasa za Tanzania zimefika pabaya. Huyu mtu ananini cha ajabu hata akang'ang'aniwa na ccm? Hawayaoni haya mapungufu yote? Passport mbili, uraia wa mashaka na hajawahi hata siku moja kupiga kura kwakuwa hayumo kwenye daftari la kidumu. Tanzania kazi tunayo.
 
Ili kugombea ubunge hakuna sifa ya kwamba lazima uwe umejiandikisha kama mpiga kura kwenye jimbo unalogombea au mahali pengine popote TZ.

Kama mnataka hiyo sheria itungwe basi pendekezeni kwenye katiba mpya na mtaona madhara yake. Itakapowakata mnaowataka msije mkalalamika.

Point hapa ni kwamba uandikishwaji wa wapiga kura kwa TZ haufanywi kila siku. Kuna vipindi maalum ambapo watu huandikishwa na mara nyingi wanaandikishwa kwenye sehemu wanazokaa.

kwa mfano Watanzania wote wanaokaa nje ya nchi hawatakuwa na nafasi ya kugombea uongozi wowote Tanzania. Hivyo hivyo watu wengi wanaofanya kazi mbali na kwenye wilaya zao za kuzaliwa hawataweza kugombea huko maana watakuwa hawajajiandikisha huko.

Tusianze kutaka sheria zetu zifuate matakwa yetu kisiasa, madhara yake huko mbele yatakuwa makubwa mno. Ila kama Watanzania tunalitaka hili basi tupendekeze kwenye katiba mpya.
 
Jamani naona kweli kwa upande wangu ni kichekesho kikubwa sana, inakuwaje mtu uombe upigiwe kura wakati wewe mwenyewe hujajiandikisha!
Naomba ma great thinkers mjaribu kuangalia hili.
Ni kwamba Mgombea wa CCM Arumeru Sioi Sumari hajajiandikisha kupiga kura popote Tanzania, sasa leo anakuja kuomba kura, hii inakuwaje

Kama ana sifa za kuwa mbunge apewe tu,ila hapo yeye kapoteza sifa ya kupiga kura.Usijichanganye mkuu.
Elewa,unaweza kujiandikisha kupiga kura usipige kura (siyo kosa kisheria) na unaweza kuchaguliwa kwa kura wakati haujajiandikisha kupiga kura .

Ili kugombea ubunge hakuna sifa ya kwamba lazima uwe umejiandikisha kama mpiga kura kwenye jimbo unalogombea au mahali pengine popote TZ.

Kama mnataka hiyo sheria itungwe basi pendekezeni kwenye katiba mpya na mtaona madhara yake. Itakapowakata mnaowataka msije mkalalamika.

Point hapa ni kwamba uandikishwaji wa wapiga kura kwa TZ haufanywi kila siku. Kuna vipindi maalum ambapo watu huandikishwa na mara nyingi wanaandikishwa kwenye sehemu wanazokaa.

kwa mfano Watanzania wote wanaokaa nje ya nchi hawatakuwa na nafasi ya kugombea uongozi wowote Tanzania. Hivyo hivyo watu wengi wanaofanya kazi mbali na kwenye wilaya zao za kuzaliwa hawataweza kugombea huko maana watakuwa hawajajiandikisha huko.

Tusianze kutaka sheria zetu zifuate matakwa yetu kisiasa, madhara yake huko mbele yatakuwa makubwa mno. Ila kama Watanzania tunalitaka hili basi tupendekeze kwenye katiba mpya.

safi sana,bila chaguzi ndogo kama hizi hatungeweza kugundua upungufu/kasoro za sheria zetu za uchaguzi.Lazima mabadiriko kama haya yafanyike katika katiba mpya kwa lengo la ku-clear with no dought na kutoa nafasi za mtu ku appeal ktk rufaa kama atakuwa ameshindwa.
 
Wadhamini wake nao ni mbumbumbu, walidhaminije mtu ambaye yeye hana dhamana (shahada ya kupiga kura) au walidhamini pesa zake.
Hapa hakuna kitu hata akishindwa inavyoelekea atalilia mapesa yake wala si kingine, ngoje tumsikie anavyojinadi jukwaani.
Juzi alikuwa King'ori akitoa elfu tano ushahidi upo kama ataleta ubishi.
 
Tume ya Taifa (NEC) kukata ku up date daftari la kudumu la wapiga kura wakidhani wanawakomoa CDM kwa kuwa DISFRANCHISED younger voters ambao wengi wao ni wafuasi wa CDM na hawakuwa na sifa ya kupiga kura 2010 because they were < 18 years old sasa inawatokea puani CCM.

Ingawa sheria haikatazi mtu wa aina hiyo kugombea UBUNGE lakini kisiasa huo ni MTAJI mkubwa kwa CDM. Inaonekana huo Siyoi amekwenda Arumeru kuchua Ubunge kwenye BRIEFCASE au ukitaka Waarumeru wameletewa mbuzi kwenye gunia. SIYOI SIO mwenzao. Nitashangaa sana Waarumeru wakimpatia kura.
 
Kipindi tume wanapita kuandikisha daftari la kupiga kura,Sioi alikuwa UK anakoishi...Hana hata kadi ya kupigia kura leo hii anataka Ubunge wapi na wapi...
Hupati kitu hapa hata utoe Chapaa...
 
Attachments

  • IMG-20120219-WA0001.jpg
    IMG-20120219-WA0001.jpg
    86.8 KB · Views: 120

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom