Kuomba kujiuzulu ni uwajibikaji?

Njoka Ereguu

JF-Expert Member
Apr 7, 2012
821
335
Imekuwa ni desturi kwa wanasiasa wa Tanzania kusema nimeomba kujiuzulu na wananchi tunashangilia na wakati mwingine inasemekana Mkuu wa Nchi (Rais) amemkatalia waziri fulani kujiuzulu. Ilikuwa hivyo Waziri na Naibu Waziri Wizara ya Afya hivi karibuni tu wakati wa mgogoro na madaktari.

Kwa mtazamo wangu siyo sasa na inaondoa maana halisi ya uwajibikaji. Endapo kiongozi amedhamiria kujiuzulu kwa nia ya kuwajibika kwa wananchi kwa makosa yake au kwa kushindwa kutekeleza au kisimamia yale aliyoapa kuyatekeleza sioni msingi wa yeye kuomba na kusubiri majibu kutoka kwa Rais. Anatakiwa kuamua mwenyewe bila kusubiri huruma na visingizio kuwa hata Riasi ameona mimi sina kosa. Huo siyo uwajibikaji hata kidogo, ni lazima dhamira iliyokusukuma iwe kushindwa kuwajibika kwa wananchi na hivyo ni aibu kwako, familia ndugu jamaa na marafiki kuendelea kubakia katika nafasi hiyo na ili wewe kuonyesha hauridhikia na hali hiyo au uovu uliopo basi unapofanya uamuzi wa kujiuzulu wakati barua inaelekea kwa aliyekuteua (Rias) wewe unakuwa tayari umeita media na kutangaza kuwa umejiuzulu wadhifa wako bila kujali kama raisi ataridhiua au la. Kusubiri majibu kutoka kwa Rais hii ni kupotosha umma na maana ya kujiuzulu kwa nia ya kuwajibika.

Ukiangalia hata hili la PM kusema leo ameomba kujiuzulu na watu wanatumwa kumwoba asifanye hivyo haina maana na inakuwa haina dhamira ya wazi ya kufanya hivyo zaidi ya kutafuta huruma kutoka kwa umma. Hii kama ni kujiuzulu ingekuwa na maana zaidi kama angefanya hivyo wakati ule aliposhindwa kutoa majibu Dodoma baada ya kumalizika kwa bunge.
 
Back
Top Bottom