Kuoana bila kutaka watoto - yawezekana?

hapa BONGO hilo halipo, labda muwe na matatizo ya kiafya, We dont do what we actually want to do ourself:popcorn:
 
Kwamba watu wawili mnaopendana mnaamua kuoana na kuishi maisha ya pamoja bila kutaka kuwa na watoto au kupanga kuwa na watoto. Je hili linawezekana katika jamii yetu au kila ndoa inapimwa kwa mafanikio ya kuwa na watoto na kwamba bila ya watoto ndoa inaonekana kama haikamiliki na hivyo mtu yuko radhi kufanya "lolote" ili awe na watoto?

Watu hushangilia NDOA IMEJIBUUUUU!!! :clap2:
Hapo kwenye bluu mpaka kuiba mtoto wa mwenzio, we need to change:roll:
 
Rafiki yangu mmoja kwa sababu za kibinafsi ameamua kutuma ujumbe huu:

Mkuu;

Kama unanisema mimi vile.

(ndoa) Ina maana miaka 5+ tupu hatuna mtoto.

It feels bad kwake na kwangu. japo tuna kila kitu inatuumiza sana.

Upande wangu ni ngumu zaidi kwani umri umekwenda almost 47 now. Wasiwasi wa kufa bila kuacha mtoto wa kunirithi unaniandama.

Na tamaa ya kuanza kupata mto wa nje inanininyemelea.

Nampenda wa sasa lakini pia nahitaji mtoto.

Kuongea rahisi. lakini practically ina ugumu sana hasa kwetu sisi vijana.

Of course ni matatizo ya Mrs.

Unaweza ukaweka JF bila ku-disclose.
 
Mimi ningefurahi sana kumpata mwanaume ambaye hatataka kuning'ang'aniza kuzaa. Kuwa na watoto siyo lazima tuzae tunaweza kulea watoto wa kuasili au wa ndugu zetu.Sijali maneno ya watu .

Kina kaka mnasemaje?
 
nadhani wapo wa kaka wa namna hiyo.. mpigie BWANA magoti tu utashangaa alivyo na namna ya kujibu.
 
Shetani ana bidii sana, analeta style za maisha fulani fulani hivi na zinapata ushabiki na uanachama kabisa. Hata hivyo jamii ya kifamilia itaendelea kuwepo tu mpaka mwisho wa dahali, regardless hizi mbinu za Freemason zitakazowakamata baadhi ya wanadamu.
 
.......Hivi inakuwaje wanandoa kuamua kutozaa na huku wana uwezo wa kuzaa? Kama mmoja wapo ana matatizo hapo hakuna jinsi ni kuvumiliana tu kama ndoa inavyosema.......lakini kama mna kizazi na hamtaki familia kubwa bora kuzaa mtoto hata mmoja.

Mtoto mmoja napo asipokuwa na sibling hata mmoja napo tabu kweli kweli.........ahhhhh!! Hii issue ya wanandoa kuamua kutozaa mie naona haijakaa sawa labda kama wana matatizo kwenye via vya uzazi.
 
Pretty, labda wengine wanaupendo kwa wao wawili tu.. ile sehemu ya "zaendi mkaijaze nchi" inaweza ikafanywa na wengine lol
 
Wewe kweli ni Pretty. Safi sana . . . .wala sina cha kuongezea hapo labda kama kuna mtu anataka ufafanuzi
 
Pretty, labda wengine wanaupendo kwa wao wawili tu.. ile sehemu ya "zaendi mkaijaze nchi" inaweza ikafanywa na wengine lol

Hii ya kusema KUZAA IFANYWE NA WENGINE ndo inaonekana ina sura fulani ya ubinafsi, coz haijali jamii.
 
Mimi ningefurahi sana kumpata mwanaume ambaye hatataka kuning'ang'aniza kuzaa. Kuwa na watoto siyo lazima tuzae tunaweza kulea watoto wa kuasili au wa ndugu zetu.Sijali maneno ya watu .

Kina kaka mnasemaje?

sawa Tausi,
hebu angalia huo ujumbe kwenye avatar yako,
nadhani ni jibu tosha la hilo wazo lako hapa!!!!
 
Vip kama mmoja anazaa mwingine hazai halafu mmoja amwombe mwenzie azae nje halafu walee huyo mtoto wote, is it possible kwa africa??
 
Vip kama mmoja anazaa mwingine hazai halafu mmoja amwombe mwenzie azae nje halafu walee huyo mtoto wote, is it possible kwa africa??[/QUOTE]

Binafsi niseme tu kwamba, haya maongezi yote itategemea na aina ya ndoa uliyonayo.

Kama ndoa yako ni yaserikalini, ya mkataba na nyingine nisiyoijua (ambazo kwangu mimi sio ndoa) hilo linawezekana as long as ninyi wawili mumeamua.

Lakini nikija kwenye ndoa ambayo mimi ninaijua na ambayo ndiyo nimo ndani yake (Ya Kikristu), Iwapo mmoja anamatatizo ya uzazi ni suala la kujipanga tu kama mnataka mtoto muweze kuasili, na sio mmoja kutoka nje ya ndoa kwani hakutakuwa na maana ya ndoa tena. Ndoa ni uvumilivu, ndoa ni ya mke mmoja na mume mmoja bila kujali sababu yoyote ile iwayo yote haitakiwi kuvunjika. Sababu pekee ya kuvunjika kwa ndoa hiyo ni kifo, kama ni watoto mtaasili.

Otherwise kwa wale ambao Mungu amewajaalia, automatically lazima watazaa na watazaa kwani maandiko yanatamka hivyo, ni sehemu ya ndoa yenyewe, ndio ukamilifu wa ndoa.

Siafiki kabisa suala la watu wenye uwezo wa kuzaa, na wapo ndani ya ndoa, halafu wanapanga kutokuzaa, Mungu awasamehe sana sana.
 
Back
Top Bottom