Kuoa na kuolewa???

Tumain

JF-Expert Member
Jun 28, 2009
3,154
70
Mwanamke/mwanamume ambaye hakuolewa/hakuoa hata kama ni tajiri, au ana cheo kwa hakika ni "Maskini na Mhitaji"
"Nisingependa kuishi bila kuoa hata kwa usiku moja tu, hata kama ningekuwa namiliki dunia yote!"
Kweli au si kweli..
 
Si kweli,unaweza kuishi bila kuoa na maisha yakawa safi tu,je padri anaishije?
 
Mwanamke/mwanamume ambaye hakuolewa/hakuoa hata kama ni tajiri, au ana cheo kwa hakika ni "Maskini na Mhitaji"
"Nisingependa kuishi bila kuoa hata kwa usiku moja tu, hata kama ningekuwa namiliki dunia yote!"
Kweli au si kweli..

Kweli. Ila angalia usijekuwa unachanganya "kuoa" na "kuwowa"!
 
Ni mila na tamaduni zetu tu zinazo fanya mtu aone kuna ulazima wa kuoa/kuolewa. ndiyo maana kuna watu umri ukifika au kupita wana lazimisha kuingia kwenye ndoa ambazo hazi dumu au zina jaa matatizo. Ukiangali uta kuta mtu wa umri fulani akionekana hajaoa au kuolewa anaonekana ana kasoro au ni mhuni na wakati hata kwenye ndoa zenyewe kuna wenye kasoro na wahuni kibao. Mimi nasema ndoa siyo ya kila mtu. Usioe/kuolewa kama haupo tayari. Marriage should be a personal decision influenced by only your desire and will.
 
FL1 umenikumbusha kidhungu cha question tags!
Jane took your book - tookn't she?
She goes to school everyday- goesn't she lol!

BWT

Sidhani kama ni watu wote wanaoa ama kuolewa! Na kama ingekuwa ni kweli mbona wapo wanaotoka kwenye huo muunganiko na hawatamani kurudi tena? Labda kwa wanaume
 
Watu wengi hawaoi na kuolewa kwa kufuata utaratibu wa kufunga ndoa.ila yale mambo ambayo wangeyahitaji kwenye ndoa wanayapata kwa njia mbadala hata hao baadhi ya masista na mapadri.Njia hizi mbadala ni kama MBA,nyumba ndogo,mabuzi,vimada,serengeti boys na mambo yanayofanana na hayo.
Ni watu wachache ambao wamepewa neema na Mungu ya kuweza kumudu kukaa bila ndoa.
 
fl1 umenikumbusha kidhungu cha question tags!
Jane took your book - tookn't she?
She goes to school everyday- goesn't she lol!

Bwt

sidhani kama ni watu wote wanaoa ama kuolewa! Na kama ingekuwa ni kweli mbona wapo wanaotoka kwenye huo muunganiko na hawatamani kurudi tena? Labda kwa wanaume

mj1 we acha tu wakati huo bwana
 
wakati naolewa ningekuwa na akili hii ya sasa, nahic nicngeolewa! mbona c lazima ni maamuzi tu na hii kasumba ya kutafcr vibaya ambao hawajaolewa/oa ndio inafanya wa2 wajichomeke ili mradi tu.
 
Kwani sasa hivi kinachokufanya uendelee kuolewa ni nini?
 
FL1 umenikumbusha kidhungu cha question tags!
Jane took your book - tookn't she?
She goes to school everyday- goesn't she lol!

BWT

Sidhani kama ni watu wote wanaoa ama kuolewa! Na kama ingekuwa ni kweli mbona wapo wanaotoka kwenye huo muunganiko na hawatamani kurudi tena? Labda kwa wanaume

ha hea haaa haaaa, yaani MJI umeniacha kwenye sakafuni mwenzio, nimecheka mpaka mchozi
 
ndoa si kwa kila mtu, kuna wengine jinsi walivyo wameumbwa wakae bila ndoa, na wakiwa hivyo maisha yanakwenda bila matatizo, sasa ambao hawajaumbwa kuolewa/kuoa wanapojifanya kuingia kuingia humo kilazima lazima huwa wanakiona cha mtema kuni, wengine wanaishia kutoka kwa kasi ya ajabu na kutothubutu kutia mguu wao kwenye ndoa tena milele.
 
Kwani sasa hivi kinachokufanya uendelee kuolewa ni nini?

cja complain lolote kuhusu mie kuolewa lakini nikasema ningekuwa na akili niliyonayo sasa nicngeolewa....kwasasa coz imeshatokea then nasonga mbele yakinishinda njiani nita2a mzigo....
 
Kwa nini unasema hayo? hebu tueleze vizuri,unamaanisha ndoa ni mbaya.Kwa sababu watu wengi ambao hawapo kwenye ndoa wanamuomba Mungu usiku na mchana wapate ndoa,mie naona kama maneno yako ni makali yanakatisha tamaa.
 
ZD mie ndo huwa naona kila mtu aingie mwenyewe akaicheki atakavyoikuta huko ndani ni juu yake kuiboresha
na sisi wanawake katika bible tumeandikiwa kabisa
" mwanamke mpumbavu huivunja ndoa kwa mikono yake mwenyewe " kama sijakosea kunukuu
 
Thanx FL1 ,Nadhani ndoa hazifanani,kila moja ina ushuhuda wake.
 
Kwa nini unasema hayo? hebu tueleze vizuri,unamaanisha ndoa ni mbaya.Kwa sababu watu wengi ambao hawapo kwenye ndoa wanamuomba Mungu usiku na mchana wapate ndoa,mie naona kama maneno yako ni makali yanakatisha tamaa.

ZD uckate tamaa kwa lolote, ndio mana wanasema walio ndani wanataka kutoka na walio nje wanataka kuinga, mie sio kwa ubaya lakini nahic ningekuwa na akili ya sasa na nikajua maana ya ndoa kama nijuavyo sasa ningebaki nje ya uwanja tu....ndoa ni tamu/raha/karaha zake so uckatishwe tamaa na lolote.
 
Back
Top Bottom