Kuoa na kuishi mbali na mkeo/mmeo

Tasia I

JF-Expert Member
Apr 21, 2010
1,223
193
JF habari,
Jamani me hua najiuliza swali moja,
hivi logic ya kuoa halaf bado mtu mkaishi mbali na mkeo/mmeo inakuawap?
kwanfano mtu ni bachela, na unaishi mbali na unaetegemea kumwoa, mungu akajalia mkaoana,
lakini bado ukabaki huko uliko na yeye mmwenza wako akabaki huko aliko. sasa mantiki ya kuoa inakua wap hapa!
Lengo hua ni kumfunga mtu asijarib kukutoka au ni kuoa kweli!!!
 
Kama msingi ni mbovu wa ndoa yenu itakufa hata kama mko pamoja!
 
JF habari,
Jamani me hua najiuliza swali moja,
hivi logic ya kuoa halaf bado mtu mkaishi mbali na mkeo/mmeo inakuawap?
kwanfano mtu ni bachela, na unaishi mbali na unaetegemea kumwoa, mungu akajalia mkaoana,
lakini bado ukabaki huko uliko na yeye mmwenza wako akabaki huko aliko. sasa mantiki ya kuoa inakua wap hapa!
Lengo hua ni kumfunga mtu asijarib kukutoka au ni kuoa kweli!!!

Nafikiri ni njia mojawapo ya kuoneshana kuwa mmeamua kuwa pamoja, umbali sio tatizo! Na naamini watu wakishaoana, mikakati inaanza ya kuhakikisha mnapokuwa pamoja, tofauti mkiwa wachumba tu!
 
Maisha mkuu. Utakuta rizki inapatikana huko mbali ambapo huwezi kumleta/kumpeleka mke/mme wako.
 
JF habari,
Jamani me hua najiuliza swali moja,
hivi logic ya kuoa halaf bado mtu mkaishi mbali na mkeo/mmeo inakuawap?
kwanfano mtu ni bachela, na unaishi mbali na unaetegemea kumwoa, mungu akajalia mkaoana,
lakini bado ukabaki huko uliko na yeye mmwenza wako akabaki huko aliko. sasa mantiki ya kuoa inakua wap hapa!
Lengo hua ni kumfunga mtu asijarib kukutoka au ni kuoa kweli!!!

ndo maana KUOA, kwa tafsiri nyepesi kabisa ni TENDO LA NDOA............
 
Kua mbali si hoja muhimu nikuaminiana,hata mkionana mara 2 au 1 kwa mwaka inatosha ikiwa lengo lenu moja na sikuizi mitandao kibao ndio kabisa,sio yale ya zamani yakuandikiana mpaka ikifika na wewe uloiandika uhoi kwakusubiri majibu.
 
Arabianfalcon,
kweli mke na mme muwe apart kwa mwaka muonane mara 1??
unajua hapa sizungumzii kama ile et nimeoa hala naishi na mke wangu then
inatkea napata safari ya kimasomo labda nje ya nchi kwa mwaka.
sio kama hii, nazungumzia ile nioe hala nipo tz na mke wang tz lakini me mwanza ye mbea?????
 
Nafikiri ni njia mojawapo ya kuoneshana kuwa mmeamua kuwa pamoja, umbali sio tatizo! Na naamini watu wakishaoana, mikakati inaanza ya kuhakikisha mnapokuwa pamoja, tofauti mkiwa wachumba tu!
unajua nimeamua kuuliza hivi baada ya jana kutoka kazini nikiwa nimechka kweli, nikawa nipo seatingtu nimekaa nakula music.
nikaanza kuwaza hapa ningekua na mpenzi wangu japo ningechangamka.kuchezacheza nae, na utani wa hapa na pale.
lakini ndo likaja hili wazo kua mbona kunakuoa na bado ukakaa mbali na mkeo??
sasa maana ya kuoa iko wap??
 
JF habari,
Jamani me hua najiuliza swali moja,
hivi logic ya kuoa halaf bado mtu mkaishi mbali na mkeo/mmeo inakuawap?
kwanfano mtu ni bachela, na unaishi mbali na unaetegemea kumwoa, mungu akajalia mkaoana,
lakini bado ukabaki huko uliko na yeye mmwenza wako akabaki huko aliko. sasa mantiki ya kuoa inakua wap hapa!
Lengo hua ni kumfunga mtu asijarib kukutoka au ni kuoa kweli!!!

ukweli ni kuwa familia ambayo haikaii pamoja haiwezi kuishi pamoja..........................in everyway distance is a barrier to true love and blissful marriage..............................utakuta kila mmoja wao tayari anafamilia yake ya kisirisiri................................mahitaji ya mwanadamu hayawei kuchakachuliwa kwa utani utani wa kuishi mbalimbali............................angalia uchagani........dume lipo mjini mama kaachwa ataabike kijijini.....jamaa mjini ana vimwali na mama kule kijijini anagaragzwa mgombani......lol.............................na baadaye ni vvu tu huwakaba kabali na haiwaachi..........lol
 
Nafikiri ni njia mojawapo ya kuoneshana kuwa mmeamua kuwa pamoja, umbali sio tatizo! Na naamini watu wakishaoana, mikakati inaanza ya kuhakikisha mnapokuwa pamoja, tofauti mkiwa wachumba tu!

kuwa pamoja ni kuishi pamoja siyo kinadharia tu................................mahitaji ya kuwa pamoja hayawezi kuchakachuliwa hata siku moja......................
 
Moja ya sababu kuu ya kuishi mbali kwa wanandoa ni harakati za kusaka maisha na ndoa ina maana zaidi ya hicho unachokifikiria ww.Acha utoto,kuwa uyaone.
ndo maana KUOA, kwa tafsiri nyepesi kabisa ni TENDO LA NDOA............
 
Lakini kama uliamua huo umbali unaweza kuwa kipimo cha mapenzi kwamba je unaweza kukaa mbali na mke/mume wako bila kumsaliti?
 
ukweli ni kuwa familia ambayo haikaii pamoja haiwezi kuishi pamoja..........................in everyway distance is a barrier to true love and blissful marriage..............................utakuta kila mmoja wao tayari anafamilia yake ya kisirisiri................................mahitaji ya mwanadamu hayawei kuchakachuliwa kwa utani utani wa kuishi mbalimbali............................angalia uchagani........dume lipo mjini mama kaachwa ataabike kijijini.....jamaa mjini ana vimwali na mama kule kijijini anagaragzwa mgombani......lol.............................na baadaye ni vvu tu huwakaba kabali na haiwaachi..........lol
Mkuu uko sahihi kabisa. Hili ni tatizo ambalo limewakabili ndugu zetu wengi wakajikuta ndoa ikivunjika. Kumbuka mke akutoka kwao kuja kula na kulala bali kaja kukufuata wewe. hivyo hata ala machopo chopo kibao bila penzi lako ni bure. Yuko radhi kulala njaa lakini awe na mpendwa wake.
 
kuwa pamoja ni kuishi pamoja siyo kinadharia tu................................mahitaji ya kuwa pamoja hayawezi kuchakachuliwa hata siku moja......................

Nakubaliana na wewe Ruta, lakini kama mmefikia hatua ya kufunga pingu, lazima ziwepo juhudi za kuweza kuishi pamoja! Ofcoz hata mimi sikubaliani kwamba wanandoa wanakubaliana kuishi mikoa tofauti miaka yote.......mhhhh!!! hapana! Sometimes we have to sacrifice something to save our marriage!
 
JF habari,
Jamani me hua najiuliza swali moja,
hivi logic ya kuoa halaf bado mtu mkaishi mbali na mkeo/mmeo inakuawap?
kwanfano mtu ni bachela, na unaishi mbali na unaetegemea kumwoa, mungu akajalia mkaoana,
lakini bado ukabaki huko uliko na yeye mmwenza wako akabaki huko aliko. sasa mantiki ya kuoa inakua wap hapa!
Lengo hua ni kumfunga mtu asijarib kukutoka au ni kuoa kweli!!!

Ni majaribu makubwa sana na yanaweza kabisa kusababisha kuvunjika kwa ndoa. Juzi nilikuwa naongea na rafiki yangu nikamuulizia kama alipata bahati (alipokuwa Dar) ya kukutana na marafiki zetu wa siku nyingi tuliokuwa na chuoni. Hawa tulipokuwa chuoni walipendana sana walikuwa kama chanda na pete na hatimaye wakaoana kwa harusi kubwa sana. Akaniambia aliishia tu kuongea na madame walishindwa kukutana kutokana na ratiba zao kupishana. Madame akalalamika kwamba mume kahamishiwa Arusha ana kazi nzuri sana kule na Mrs naye ana kazi nzuri sana Dar lakini gharama za kusafiri kila wakati ili kukutana zimeanza kuleta kutia dosari kwenye ndoa maana wakati mwingine hukatika miezi chungu nzima bila kuonana. Tukabaki tunasikitika tu kwamba kama wasipofanya maamuzi haraka ya kuwa pamoja kama familia basi ndoa yao inaweza kabisa kuingia mizengwe kutokana na majaribuni makubwa kwa wote wawili. Hili la kuwa na ndoa halafu mnaishi mbali mbali kwa kweli linaleta dosari kubwa sana hasa kama kuishi huko mbali mbali kutakuwa ni kwa muda mrefu.
 
Lakini kama uliamua huo umbali unaweza kuwa kipimo cha mapenzi kwamba je unaweza kukaa mbali na mke/mume wako bila kumsaliti?
huko ni kujitia majarbuni. sasa ukishindwa na ukamsaliti ndo uprove kua huwezi then umwite mkeo au??
na yeye kule akifanya hivyo??
 
Back
Top Bottom