Kunywa pombe kuna faida gani??

Hakuna kisichokuwa na madhara kinapotumika kwa kiwango cha kuzidi. Magari ni mazuri lakini tunalalamikia mwendo kasi! Kadhalika na pombe kama ukifanya mwendo kasi ndio madhara yake. Vingenevyo, pombe ni kinywewa murua na kinachoburudisha kuliko vinywaji vyote. Na ndio maana kinaweza kunywewa kwa muda mrefu kuliko kinywewa kingine. Watu mara nyingi wanaisingizia pombe kwani huwawezesha kuyafanya yale yaujazao moyo wao kwa kisingizio cha pombe!

Umenena mkuu!!
 
Pombe inafaida sana kuliko hasara, unakuwa na madeni usiyoweza yalipa! inaongeza IQ
 
Kwangu mm pombe huwa inaniongezea Upendo huwa nawapenda hata maadui zangu.

Umenifunja mbafu sangu!! hahaaaaaa!!
Yaani unaweza kugawa pesa hata kwa adui zako!? hii safi sana.
Ila mie kuna watu nawajua wakinywa wanongea English kwa kwenda mbele tena nzuri sana tu...sijui inakuwaje?
 
Kwa wale mnao andika kuwa pombe haina faida - are you truly serious?
- Tanzania Distillers (Konyagi)
- Mabibo Wine and Spirit (Heineken)
- Serengeti Breweries (Chui Chui)
- Tanzania Breweries (Safari tangia zamani)
- Jumlisha Mabaa yote na Nyumba zote za starehe (ni mengi mno haya kuyaorodhesha hapa)

Hivi hapa tunaongelea ajira na pato la kiasi gani? Mnataka hawa watu na familia zao waende jehanamu mapema?

Hivi mbona hamna uchungu na jirani zenu?
 
Afya jingi (mashavu hiha).

Nna bro wangu anakata ulabu kwa kwenda mbele. Jamaa ngano imemfanya kapasuka mwili kinoma....

Mwambie awahi Hosipitali kucheki Inni.
Kwa wale msio elewa Ukinywa sana Pombe Ini linakua halifanyi kazi vizuri. Matokeo yake maji yanajaa tumboni (Kitambi)

Kuna mwana JF anaweza kutupatia stori ya Mwanafunzi alifariki in One of the colleges. kama sio CBE ni IFM.
Wenzake walikua wanamwambia '' umechna mwanangu'' anaona sifa anaongeza kilaji. Siku ya siku alidondoka tu, alipopelekwa Hosipitali tayari Kwishen Kabisa. Doctor alichowaambia ni kwamba mbona huyu alioshakufa siku nyingi. Sababu ya pombe. Take care guys.
nawakilisha
 
Kwa wale mnao andika kuwa pombe haina faida - are you truly serious?
- Tanzania Distillers (Konyagi)
- Mabibo Wine and Spirit (Heineken)
- Serengeti Breweries (Chui Chui)
- Tanzania Breweries (Safari tangia zamani)
- Jumlisha Mabaa yote na Nyumba zote za starehe (ni mengi mno haya kuyaorodhesha hapa)

Hivi hapa tunaongelea ajira na pato la kiasi gani? Mnataka hawa watu na familia zao waende jehanamu mapema?

Hivi mbona hamna uchungu na jirani zenu?

Hata TCC Ina wafanyakazi wengi sana na inalipakodi kubwa tu!! Lakini unaambiwa uvutaji wa sigara unadhuru afya yako.
 
Mwambie awahi Hosipitali kucheki Inni.
Kwa wale msio elewa Ukinywa sana Pombe Ini linakua halifanyi kazi vizuri. Matokeo yake maji yanajaa tumboni (Kitambi)

Kuna mwana JF anaweza kutupatia stori ya Mwanafunzi alifariki in One of the colleges. kama sio CBE ni IFM.
Wenzake walikua wanamwambia '' umechna mwanangu'' anaona sifa anaongeza kilaji. Siku ya siku alidondoka tu, alipopelekwa Hosipitali tayari Kwishen Kabisa. Doctor alichowaambia ni kwamba mbona huyu alioshakufa siku nyingi. Sababu ya pombe. Take care guys.
nawakilisha

Ngoja nimtafute kwenye simu yake....-...->>>>


>>> Argh! Hapokei bana.
Sijui yuko baa.
Kwa hiyo mkuu kitambi chochote ni dalili ya ini kudhoofika hata km hunywi?!
 
Kwangu mimi Pombe haina faida(kwa mtu) bana,ina hasara(inakuletea umasikini,ngono zembe,ujasiri wa kijinga unaoweza pelekea upigane/upigwe au kufanya uhalifu wowote ule,magonjwa kama kisukari na matatizo ya ini(gongo)

Sanasana pombe ina faida kwa serikali tu maana inapata kodi nyingi kutoka makampuni yanayotengeneza vilevi...Ni mtizamo tu

Mhhhh! Balatanda inaelekea tuna mtazamo unaofanana katika mambo mengi sana. Yaani nilikuwa nasoma ulichoandika utadhani nimekiandika mimi Mkuu. Nakubaliana na yote uliyoyaandika. Nilikuwa na jamaa (sasa ni marehemu kutokana na pombe) yangu alikuwa kaweka sana mambo ya pombe . Na yeye alikuwa anakunywa zote tu kuanzia beer, nyagi na Whisky na mwenyewe alikuwa anaona sifa sana hasa tukiwa katika majumba ya starehe au mabar.

Alikuwa anakunywa hata nusu crate au zaidi ali mradi tua aonekana yeye ni mwanaume wa shoka. Kama tukiwa usweken amnbapo miaka hiyo beer zilikuwa hazipatikani basi mwendo ulikuwa ni nyagi au whisky tena kavu kavu. Siku moja akaamka asubuhi anadai moyo unaenda mbio kumpeleka hospitali ilionekane kwamba afya ilikuwa imeathiriwa sana na unywaji wa pombe kupita kiasi na daktari (ambaye alikuwa ni rafiki wetu wa karibu sana) akamshauri sana aachene na pombe au apunguze sana. Jamaa hakusikia kwani yeye alidai anakula vizuri sana ugali na nyama choma hivyo haiwezi kumuathiri kihivyo.

Miaka michache iliyopita alipata stroke mbaya sana ambayo ikamfanya hawezi kufanya lolote lile bila kupata msaada wa mkewe na hii ilisababishwa na unywaji wa pombe kali. Alikuwa mtu mkubwa katika moja ya mabenki nchini na walimsaidia sana kumtibu kule South Africa lakini hakukuwa na mafanikio na mwaka jana mwezi May alirudisha namba katika umri ambao bado ni mdogo sana. Pombe kama unakunywa basi kunywa aste aste ukitaka kufakamia ili uonekane wewe ni mkali mbele ya kadamnasi au kunywa kila siku iendayo kwa Mungu basi ujue unaidhuru sana afya yako. Always remember that too much of anything is harmful.
 
Ulevi (pombe za aina yote, mvinyo n.k) vyote huwa vina alcohol aina ya Ethanol. Japokuwa Alcohol hutumiwa kwenye madawa kama viyayushaji (solvents) vya ule mchangayiko wa chemikali unaofanya dawa. Kwa ujumla wake Alcohol ni sumu.

Alcohol aina ya Ethanol ndio inayokuwa ndani ya ulevi kwa ufahamu wangu ndio inayosababisha mtu kuwa katika hali ya kulewa. Madaktari huweza kusema kiasi cha alcohol mwilini (blood alcohol level) kwa kupima ethanol iliyo kwenye damu. Na hichi ndicho kipimo wanachotumia polisi kushtaki watu wanaokamatwa wakiendesha magari na huku wamelewa.

Ama manufaa madogo ya pombe au vileo ni:


  1. Kupata fedha kwa wauzaji.
  2. Kudhaniwa na wanywaji kuwa inatoa dhiki na fikira kwa muda.
  3. Kutumika kuhifadhia baadhi ya vyakula.
  4. Kusafisha sehemu za jeraha na kuua viini.
  5. Kudhaniwa na wanywaji kuwa inasisimua au kuchangamsha.
  6. Kutumika katika mafuta aina ya virashio na manukato.

Ulimwengu wa leo umejikubalisha kwamba kuna pombe halali na haramu. Hata hivyo, manufaa haya yanazidiwa na madhara yake mengi yaliyo dhahiri na yanayo athiri afya ya mnywaji. Ubinadamu na utu wako, jamii na akili.

Inajulikana kuwa pombe ndio mama wa maasi yote, kwani kwayo hiyo pombe tumeshuhudia mauaji, ubakaji, liwaati, uvutaji wa kokeni na bangi, uzinifu, wizi, utovu wa adabu na kadhalika. Pombe uharibu afya yako hasa ini. Pombe udumaza akili na vile vile kuzuia kufikiri. Pombe husababisha ajali za barabarani na hata kupoteza maisha ya watu.

Pombe uchochea manyanyaso ndani ya majumba. Ukiwa addict wa pombe usababisha uharibifu wa kifedha. Kukosa hayaa, heshima, ustaarabu, na kufanya matendo ya kipuuzi mara nyingi. Kutoa maneano machafu, matusi. Kugombana na watu. Kutoa harufu mbaya mdomoni. Kuharibu ndoa kwa kukosa kutimiza haki za mke/me na watoto. Kupoteza wajihi wako na kuonekana mzee kabla ya umri wako... n.k n.k n.k

"Ulevi si dawa bali ni maradhi"

"Enyi Mlioamini! Bila ya shaka ulevi, na kamari, na kuabudu masanamu, na kupiga ramli, ni uchafu katika kazi ya Shetani. Basi jiepusheni navyo, ili mpate kufanikiwa".
Al-Maaidah: 90

Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wa.fi.raji, wala wala.wi.ti, wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang'anyi.
1 Wakorintho 6:9-10
 
Mi nikinywa pombe zinanisaidia maana nakuwa naongea kiingredha vibaya sana yaani kina flow tu chenyewe.
 
......kila mtu anajua mwisho wake au mungu ndio anajua..kunywa pombe kama unataka ...
 
dhana nzima ya maisha ya binadamu ni kuwa na furaha, sasa kama mtu anapata furaha kati ya mambo haya ya Ufusuka, Ulevi, Kupata stimu kupitia bange / Madawa, Sigara etc - ni poa tu sababu hakuna binadamu ataishi milele hapa duniani.

Huwezi kujua faida, raha au hasara ya mtumiaji wa vitu hivi kama hujawahi kutumia likewise huwezi kujua wokovu maana yake nini kama wewe si mmoja wao.

utamu wa ngoma - jifunge kibwebwe - then uingie uwanjani. Mtoa mada jaribu kupiga serengeti kumi kumi kila siku kwa siku 30 then then ukija hapa JF utatuambia faida au hasara. wengine sisi tunajua pombe ina faida nyingi tu.
 
Back
Top Bottom