Kunyongwa Kwa Mkuu Wa Majeshi: Watanzania Tumejifunza Nini?

Hivi huwa tunajifunza kwa maana ya kujifunza au tunajifunza kwa kutamka?

Kama tungekuwa tunajifunza kupitia semina warsha makongamano na study tour zilizofanywa na "washika dau" wa nchi hii..hata maendeleo yasongekua hivi
 
Sawa kunyongwa tutajitetea na swala la haki za binadamu lakin je hawa mafisadi wanaopewa vyeo mpaka bungeni wamechukuliwa hatua gani za kisheria????
Kwakweli ni ajabu kwelikweli,fisadi mwingine anaitwa Lowasa naye alichukuliwa na CDM wakamsafisha akapeperusha bendera ya UKAWA.Yani hii nchi haishi vituko
 
Kesho ukifanyiwa wewe ndio utajua kuwa kukosa utawala wa sheria hakufai

Maendeleo yanagharama zake,, na hizo ndio gharama za maendeleo, ukiupa uzembe na upumbavu nafasi pia ujuwe lazima kuna gharama zake, watanzania wanasuffer gharama za uzembe na upumbafu kwa sababu ya kuukumbatia uzembe na upumbavu..
hakuna taifa lolote lililoendelea duniani kwa kufuata hicho unachokiita utawala wa sheria, utawala wa sheria huja baada ya kudicpline watu kwa ubabe na ukatili then baada ya hapo watu huishi kwa kufuata huo utawala wa sheria kwa hofu ya kuogopa kurudi kule walikotoka kwenye ubabe, hata hiyo USA baba wa dunia alianzia huko...rudi kasome historia.
 
ujui kuwa ili upate cheo nchi hii ni mpaka uwe fisadi?
Yani kama tumerogwa vile,hemu tizama Lowasa jinsi CDM walivyomshikia bango wakati ule kwamba ni Fisadi then badae haohao wakamfanya raisi wao tena wakamuita shujaaa,yani vituko kila siku
 
Kwa hii tabia ya kuupigia magoti ufisada na matumizi mabaya ya madaraka tanzania haitakuja ifanikiwe katika jambo lolote.ufisadi umefika mahali tuna amini hata kujenga vyoo mashuleni lazima iwe kwa hisani ya wazungu.hakuna siku ntaumizwa na siasa zetu kama nilipo sikia na kuona hata zoezi la kutahiri watu wetu nalo linafanyika kwa hisani ya wazungu.idiots
 
Mkuu Wa Majeshi wa Korea Kaskazini Amenyongwa Mpaka Kufa Baada ya Kukutwa na Tuhuma Za Ufisadi Katika Nchi Hiyo. Hukumu Ya Kunyongwa Imekuja Baada ya Mkuu Huyo Wa Majeshi Kutoonekana Hadharani Toka Januari.

Sisi Watanzania Na Serikali Yetu Kwa Ujumla Tumejifunza Nini Toka Kwa Wenzetu Katika Suala La Uwajibikaji Na Utekelezaji Wa Sheria Bila Kupindisha Hasa Wakati Huu Tunapotumbua MAJIPU Na Tukiwa Tunasubiria Uanzishwaji Wa Mahakama Ya Mafisadi?

Masikini, angekuja Tanzania wala hayo yasingemkuta. Muda huu angekuwa anafagia darasa la chekechekea ili watoto wakae kwenye mazingira mazuri.
 
Rais wa Korea kaskazini toka apokee kijiti cha kuwa Rais toka kwa baba yake ameshawaua viongozi wa juu wa kijeshi 4 na wanajeshi wengine 15 na taharifa ya huyu mkuu wa majeshi imetoka juzi baada ya kukaa kikao cha Nchi wanaopingana na kurushwa bomu la majaribio la masafa marefu..aliondolewa huo wazifa wake na kufungwa kifungo cha Nyumbani kwa muda mrefu kabla ya kuuawa na imekua siri kubwa katika Nchi ya korea Kaskazini ili kuficha wanaomsapoti kuleta madhara hii ni kwa mujibu wa spy wa south korea na ndio hao waliotoa Taharifa ya kuuawa kwake..unapewa kesi unauawa huyu dogo hakuna anaemwamini kwa alie karibu yake yoyote mwenye kuwasiliana na South Korea akipata Taharifa unakula kitanzi..
 
Yona na mramba siyo mfano mzuri kwa kuwa kosa Lao bado ni dubious, jiulize tukitoa hukjmu hiyo kwa IPTL, dowans na Richmond tutanyonga wangapi na ni akina nani?
 
Mkuu Wa Majeshi wa Korea Kaskazini Amenyongwa Mpaka Kufa Baada ya Kukutwa na Tuhuma Za Ufisadi Katika Nchi Hiyo. Hukumu Ya Kunyongwa Imekuja Baada ya Mkuu Huyo Wa Majeshi Kutoonekana Hadharani Toka Januari.
Tunachojifunza ni kwamba viongozi kama huyo Kim Jong ni hatari mno,na anawaua watu wanaompinga kwa kisisngizio cha ufisadi....usidanganyike....fidhuli mkubwa huyo!
 
Mkuu Wa Majeshi wa Korea Kaskazini Amenyongwa Mpaka Kufa Baada ya Kukutwa na Tuhuma Za Ufisadi Katika Nchi Hiyo. Hukumu Ya Kunyongwa Imekuja Baada ya Mkuu Huyo Wa Majeshi Kutoonekana Hadharani Toka Januari.

Sisi Watanzania Na Serikali Yetu Kwa Ujumla Tumejifunza Nini Toka Kwa Wenzetu Katika Suala La Uwajibikaji Na Utekelezaji Wa Sheria Bila Kupindisha Hasa Wakati Huu Tunapotumbua MAJIPU Na Tukiwa Tunasubiria Uanzishwaji Wa Mahakama Ya Mafisadi?
Tumejifunza kuwa na sisi tuanze kuwanyonga hawa mafisadi wa kijani
 
Daudi Bashite angekua korea tungekua tushamsahau
Tena huyu asingenyongwa sjui angefanywaje yan ili apotee taratibu
 
Back
Top Bottom