Kununua mali ya wizi ni kosa?

Mtumiabusara

JF-Expert Member
Nov 18, 2009
473
40
Hebu fikiria kuwa kuna mtu amekuletea mali ya wizi mfano simu ya bei kubwa (zaidi ya Tsh 600,000) akakuuzia bei poa kama Tsh 30,000, Je utakataa kununua? Kumbuka kuwa muuzaji humjui mmekutana tu barabarani na ni eneo ambalo halina watu, kiasi ambacho huwezi kufanya chochote kumchukulia hatua za kisheria


Kuna namna mbili au 3 za kukabiliana na hali hii
  • Kwanza inawezekana wakati unanunua, ulikuwa unajua kabisa hii ni mali ya wizi, lakini hujui imeibiwa wapi au kwa nani, na wewe kwa sababu ulikuwa unatamani kuwa na simu kali umeamua kuinunua, na umeshawaonesha watu mbalimbali kuwa umenunua hii simu kwa bei mbaya
  • Pili inawezekana ulinunua huku ukijua kabisa aliyeibiwa ni fulani, ukaona ni bora niinunue ili nimrudishie baadae, kwani usipofanya hivyo kwa wakati huo, huyo jamaa anaenda kumuuzia mtu mwingine ambaye humjui. Baada ya kununua ukaipenda, ukaona ngoja ukae nayo kwanza kwa siku au miezi kazaa
Sasa mweye mali amejitokeza, anataka uanzishe uchunguzi wa kumtafuta mwizi wake (aliyeiba simu) huku ukijua kabisa ile mali umeuziwa wewe, utashirikiana naye kwenye huo uchunguzi?

Siasa za Tanzania ndipo zilipofikia sasa, Chadema wanataka tume huru ya kuichunguza NEC ilivyotangaza matokeo, na CCM ambao wanatakiwa waunge mkono hoja hiyo wao ndio labda wamenufaika na kazi iliyofanywa na NEC

Tafakari, ungekuwa wewe ungefanyaje?
 
Back
Top Bottom