Original Pastor
JF-Expert Member
- Nov 14, 2007
- 1,274
- 50
Laaahaula lakwata ukistaajabu ya musa.....
Sasa gonjwa gani tena hilooooooooooooo
Sasa gonjwa gani tena hilooooooooooooo
Huo ni unyanyapaa tu wa wazungu. Mbona waafrika ni wasafi kuwazidi hao wazungu ambao wanaweza kumaliza hata wiki bila kugusa maji. Kwao mapafymu tu. Mnuko unatumiwa kama silaha ya dharau, ubaguzi, nk kama ulivyoitoa hapo juu. Si kweli kwamba waafrika wote wana kikwapa, japo yawezekana wachache wakawa wachafu.
.... Wakatuomba tuwashauri hawa jamaa wawe WANAOGA kila siku. Nimejaribu kuwafahamisha hawa jamaa kwamba hawa wageni wanaoga kila siku, isipokuwa hawajazoea kutumia Deodorant. Supervisors hawaamini kwamba mtu anayeoga kila siku atakuwa ananuka kikwapa kiasi hicho.
Kivumbi kilichonipata ni kwamba, nilipowashauri hawa jamaa kuhusu tatizo hili na kuhusu matumizi ya Deodorants, baadhi yao hawakufurahishwa na ushauri wangu. Moja wao (kutoka Congo- Kinshasa) kanishutumu kwamba nimeishabadilika kimaadili kwa kuiga tabia za wazungu!!!
Sasa swali ni je, ni kweli kwamba Waafrika peke yao ndio wenye kunuka KIKWAPA? Pili, utamshauri vipi mtu kuhusu suala personal kama hili? Na mwisho kabisa, je dada zetu wanadeal vipi na hali kama hii katika mahusioano yao? Haswa tukizingatia kwamba mke au rafiki lazima anajuwa kilema cha mume au boyfriend wake.
Je, wakina dada wanawaambia ukweli waume na marafiki zao ili kukabiliana na hili TATIZO? Nasita kutumia neno AIBU kwa sababu nafahamu kwamba kuna baadhi ya jamii na makabila ambayo yanatumia zaidi harufu zao (Olfaction) kuliko kuona au kugusa katika maisha yao ya kawaida. Lakini nimeishashuhudia mara kadhaa Wazungu na makabila mengine wakiwanyanyasa watu weusi kwa sababu ya tatizo la KIKWAPA. Msemo kwamba WAAFRIKA WANANUKA ndio imekuwa joke kwenye sehemu nyingi za kazi.
Things in Perspective:
Huo ni unyanyapaa tu wa wazungu. Mbona waafrika ni wasafi kuwazidi hao wazungu ambao wanaweza kumaliza hata wiki bila kugusa maji. Kwao mapafymu tu. Mnuko unatumiwa kama silaha ya dharau, ubaguzi, nk kama ulivyoitoa hapo juu. Si kweli kwamba waafrika wote wana kikwapa, japo yawezekana wachache wakawa wachafu.
Nina rafiki yangu mmoja wa kizungu, yeye anatoka na wanawake weusi tu, nilipomuuliza kwanini anapenda pussy nyeusi, akanijibu weusi ni wasafi sana kuliko weupe, kwasababu tunajihisi tunanuka kwahiyo tuna kuwa na extra care kuhusu usafi wa miili yetu. Wa IRISH wanaoga once a week tena friday, sasa sijui hapa nani ananuka.
wao wananuka ndio maana wakagundua ma deodorant na maperfume ili kuficha harufu
...tukubali kukosoana.
Unaposhauriwa harufu ya mwili wako ni kero kwa wenzako, fanya jitihada kusawazisha hitilafu hiyo. Kunuka mdomo, kikwapa, na hata sehemu za siri sio sifa... ni karaha. Haijalishi wewe ni Muafrika, Mzungu au mhindi. Personal Hygiene ni muhimu.
Huenda wenyewe tunastahmiliana kutokana na ugumu wa hali za maisha, lakini harufu mbaya haimpendezi kila mmoja wetu, iwe ni Tanzania au hata huko ugenini. Jifikirie umo kwenye taxi yenye kiyoyozi halafu dereva ananuka kikwapa!
Tujitahidini jamani
Ulichosema mkuu ni sawa. Hata sisi hatupingi kuambiwa kuwa msafi mwili, kinywa, mavazi. Haya yote ni sawa. Tunachopinga na kukataa ni ku-categorize watu wa rangi fulani kwamba ndo wenye kikwapa. Hii si kweli. Kunuka kikwapa ni uchafu wa mtu binafsi, hauna cha rangi wala kabila. Mtu yeyote asipojitunza atanuka. Hivyo dhana ya kwamba waafrika tunanuka (kwa sababu tu waafrika) ni dhana potofu, ya kibaguzi, na madharau. Ndo mana mi nikasema mbona hata wao wachafu tu, tena wananuka sana. nasema hivi kwa vile niliwahi kukaa nao mpaka kwenye familia zao: wengi hawaogi hata kwa wiki zima. Wanabaki na kazi ya kujimwagia rashi tu.
Malalamiko makubwa kutoka kwa ma-supervisors wao ni kwamba baadhi ya hawa jamaa wanatoa harufu kali sana (Kikwapa), haswa wakati wa kupiga boksi. Wakatuomba tuwashauri hawa jamaa wawe WANAOGA kila siku. Nimejaribu kuwafahamisha hawa jamaa kwamba hawa wageni wanaoga kila siku, isipokuwa hawajazoea kutumia Deodorant. Supervisors hawaamini kwamba mtu anayeoga kila siku atakuwa ananuka kikwapa kiasi hicho.
Kivumbi kilichonipata ni kwamba, nilipowashauri hawa jamaa kuhusu tatizo hili na kuhusu matumizi ya Deodorants, baadhi yao hawakufurahishwa na ushauri wangu. Moja wao (kutoka Congo- Kinshasa) kanishutumu kwamba nimeishabadilika kimaadili kwa kuiga tabia za wazungu!!!
Kwa maoni yangu Wazungu ni wachafu sana kuliko weusi kwenye kila kitu kuanzia mavazi, miili yao na hata majumbani mwao ambapo si ajabu kukuta wale wenye kupenda mbwa kulala nao vitandani.
Hata wachina wana dhana hiyohiyo kwamba tunanuka. Na sababu ni kwamba hatuogi. Kunuka kwapa tunanuka kweli ila sidhani ni kwa sababu hatuogi may be madaktari hapa ukumbini watuambie ni kwa nini tunanuka.Na weupe wapo wanaonuka. Mchina joto lipo more 37oC anakuuliza je kuna joto leo ukimwambia ndiyo anadhani una-pretend tu. wanachukulia sisi weusi tulishaunguzwa na jua hatusikii kitu tena.
Harufu anayoitoa binadamu inategemea na misosi unayopiga, usafi kwa ujumla wa mwili na nature ya mwili. Sio suala la rangi kwa asilimia 100.