Kunguru katua juu ya kichwa changu, nashauriwa niende Bagamoyo, ni sahihi?

Nshukuru mkuu, lakini nikikaa mwenyewe tu nikaomba kwa imani Bwana wa Majeshi si atanisikia?
Kweli jambo hili limeni shake kiaina.
Tafadhali acha kumpa nafasi SHETANI ajiinue kupitia kwako. YESU NDIO JIBU KWA KILA KITU. Tua mzigo ulionao kwake naye atakupumzisha.
 
kutokana na uzoefu gani unaongea haya? kwasababu watu unajua wanaongea kitu wasichokijua. kama wengine walivyosema, kama kweli hiyo kitu imetokea, na ina mazingira ambayo si ya kawaida kwa reasonable person, unatakiwa uende kwa watumishi wa Mungu wakuombee. wewe unayesema hautakiwi kuombewa na mtu hauelewi, si kila mtu anaweza kuomba maombi yakajibiwa, unatakiwa uwe na connection na Mungu katika moyo wako, yaani uokoke. kama ungekuwa umeokoka hata huyo kunguru angekukimbia asingekugusa. mtu ambaye hajaokoka ataomba miaka mia, hatapata, hadi atubu dhambi,, aokoke. wengi walimfuata Yesu wakapona, pamoja na kwamba walikuwa na uwezo wa kuomba kivyao, wengi waliwafuata mitume na kina paulo wakaombewa wakapona, pamoja na kwamba walikuwa wanaweza kuomba kivyao. kiwete alikaa mlangoni pa hekalu akiomba miaka na miaka, hadi kina petro na yohana walipopita wakaweka mkono juu yake akatembea. hata leo hivi, kuna watumishi wa Mungu walio na karama tofautitofauti, ambao Mungu anawatumia kufungua matatizo ya watu, Mungu anawatumia kutenda kazi zake hapa duniani. MUNGU HUFANYA KAZI KUPITIA WATU, NA HAWA NDIO WACHUNGAJI NA WATU WENGINE WALIOOKOKA, wanaoongozwa na Roho wake kila siku. HII NAONGEA KWA WATU WENGINE, KWA HUYU JAMAA, SIONGEI KITU KWASABABU NIMEONGEA VYA KUTOSHA KUHUSU YEYE. kama uamuzi atakuwa ameshachukua. NAONGEA NA WATUU WOTE WENYE MATATIZO YOYOTE HAPA NDANI, MSIDANGANYIKA NA USHAURI WA KWAMBA UNAWEZA KUPIGA MAGOTI CHUMBANI KWAKO UKASALI, LAZIMA UENDE SEHEMU AMBAYO UTAKUTA WATUMISHI AMBAO MUNGU ANAWATUMIA, HAPO NDO UTASHIRIKIANA NAO KUJIFUNZA MAMBO YA MUNGU, NA PIA MUNGU ANAWEZA AKAWATUMIA KUKUOMBEA. bila Maombi ya Musa, Harun alikuwa afe, bila maombi ya Musa ukoma wa miriam dadake musa usingepona, bila maombi ya musa, mungu angewaangamiza wana wa israel. lazima uende kwa mtu ambaye Mungu amempa karama ya kufungua watu. katika biblia imeandikwa "pozeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo, mmepata bure toeni bure", kumbe kuna watu ambao Mungu amewapa uwezo wa kufufua, kutoa pepo, kutakasa wenye ukoma, kufungua watu nk. only some people, si kila mtu, Mungu humpa kila mtu karama kama vile yeye apendavyo, kwaajili ya kazi yake ya ukombozi wa mwanadamu hapa duniani. i hope you understand this.
Hakuna zaidi ya kuwa na Imani. Hata nani akuombee bila imani ni kazi bure. Inayoponya ni imani. Ukiomba uponyaji kwa Imani, utapona kwa Imani. Mungu ukimwamini atakuponya na kama uponyaji utapitia kwa mtu fulani basi Mungu atakuongoza mwenyewe au atakuletea hata huyo mtu. Uponyaji unatoka kwa Mungu na si kwa mtu awaye yote!!!! Ni Mungu peke yake anayeponya!!!! Wala si mtu fulani, wala si dhehebu fulani!!! Watu wasijiinue kuwa wao wanaponya maana kwa kufanya wanatenda dhambi, ujue pia yakuwa hata shetani anafanya miujiza mingi tu, na si kila muujiza watoka kwa Mungu. Tatizo letu kubwa siku hizi tumekuwa watu wa kufuata na kutafuta miujiza wala si Neno la Mungu! Kunguru kutua kichwani wala haijaashiria uchawi wowote, hii hakuna tofauti na mtu anayeogopa bundi akilia usiku wakati ndiyo muda wake huo. Vitu hivi vyatokea and it is only by coincident imetua kwa huyu jamaa. Inawezekana pia kunguru alikuwa na ujumbe kwa mtu aliyekuwa anaongea na huyu jamaa!!! na kunguru kufanya hivyo malengo ya yule jamaa aliyekuwa naye yameshindwa kutimia akabaki akiduwaa kuangalia kunguru!! Kwanini mnaangalia upande hasi tu? Mbona msiangalie upande chanya pia?
 
Mzizi wa Mbuyu said:
Nshukuru mkuu, lakini nikikaa mwenyewe tu nikaomba kwa imani Bwana wa Majeshi si atanisikia?
Kweli jambo hili limeni shake kiaina.
.
Umekuwa shaked kwa kuwa ndani ya nafsi yako unaamini uchawi upo na unaweza kukudhuru....!
Angalia wafanyibiashara wa kutibu maradhi ya wasi wasi na kutokujiamini wapo wa aina nyingi, kuna maprofesa maji marefu, kuna wanao jihita mitume na manabii... sasa kazi kwako maana wajinga ndio wali wao.
 
Mimi ndiye niliyemtuma, yule wala si kunguru wa uchawi, namtumia kwenye maonyesho yangu ya sanaa za jukwaani.
Nimemfundisha mambo mengi sana.
Wala usiogope ndugu yangu.
Hutadhurika.
 
nikiwa mcheza mpira kwenye klabu moja ya ligi kuu hapa TZ, miaka ya 1990 hivi, iliwahi kunitokea mkasa kama huo, tulikua tunatoka mazoezini pale viwanja vya Tangamano kujiandaa na mechi ya Coatal Union, nikiwa nimenyoa kipara na jasho jingi linanitoka, mara kunguru hawa weusi almaarufu kama kunguru wa Zanzibar akatua kichwani mwangu na kuruka zake, hakika ni tukio lililonitisha saana, hasa ukizingatia mkoa wa Tanga miaka hiyo ulikua unasika sana kwa maruhani na mizungu ya kimazingara.
tukio lilitokea mbele ya wenzangu kama lilivyomtokea mkuu, nikapewa ushauri wa kwenda kumuona mganga wa timu na kumueleza matatizo yangu, maana klabu yetu ilikua na mganga tunayesafiri nae .
mimi nikagoma maana nikajua kitakachofuata hapo ni kwenda kukeha makaburini usiku kucha.
kiukweli sikuchukua hatua yoyote , sikwenda kwenye maombi wala kwa mganga na hadi hii leo naishi kwa amani, nikiwa nimecheza mpira wa miguu kwa mafanikio kwa miaka zaidi ya kumi na tatu.
Ndege wakati mwingine huchanganyikiwa na kupoteza mwelekeo, hupaswi kuogopa, adui yako mkubwa sasa hivi ni uoga.
 
Kunguru huyo alikuwa na njaa. Kama njiwa ningekwambia nenda kwa mzee wa upako
 
Kunguru huyo alikuwa na njaa. Kama njiwa ningekwambia nenda kwa mzee wa upako
kinachotuua katika imani za kishirikina si ndege alietua, ila uoga....hakuna cha uchawi wa njiwa wala nini, uwoga tu.
 
You are right Nguvumali. Matokeo ya kutojiamini ndio kutafuta msaada nje ya uwezo wetu hata kwa mambo tunayoweza kutatua sisi wenyewe.

Imani za ushirikina na imani kwa Mungu ni pande mbili zinazoakisi kitu hicho hicho: kutojiamini.
 
sikutanii, sisi sote tulikuwepo huko misri miaka ya nyuma, nakwambia hicho kitu si cha kawaida. hauwezi kukaa home na kupiga maombi tu, usichezee shilingi ******, huo ni uhai wako, nikiamua kukupa semina hapa, haitaisha leo juu ya mambo hayo yanavyofanyika. si ajabu kama kweli unachosema ni sahihi, wameshachukua nyota yako kichwani na mambo yako yakianza kuharibika utavaa kandambili na kutembelea daladala, unaweza kukosa hata nauli ya daladala. SI KILA MTU ANAWEZA KUTOA PEPO. na huyo anayekwambia nenda msikitini, huko ndo wanaenda kujaza kabisa. NENDA PALE UBUNGO, mdogo wangu alikuwa na tatizo kubwa la ajabu, ameenda pale, wale waliokuwa wanamloga wamepigwa na Mungu hadi wameamua kuokoka kabisa. kwenye uhai usichague kanisa, najua inaweza kuwa pengine hautaki kubadili dini, just try only for this, halatu utakuja kuniambia. kama utasubiri uombe mwenyewe hapo, hakuna daktari anaweza kujitibu. KAMA SHETANI ALIVYO NA MAAJENTI WAKE, HIVYO NA MUNGU ANAO WAFUASI WAKE SPECIAL, HAO NDO KAMA YULE JAMAA PALE UBUNGO, EFATHA, FENANDIS, MUNUO NA WENGINE WENGI. pale wanapiga maombi na hata nyota iliyoibiwa inarudi laivu, pale wanaharibu kalenda, vitabu vya kichawi ambavyo maadui zako wanaweza kuwa wameshakuandikia kukupangia tarehe, wanateketeza mitego, wanaharibu kabisa hata kama wameshakuzika wakati bado unatembea, kuna wachungaji kibao pale ukifika ukaeleza tatizo lako watakushambulia na nakwambia utakuja hapa kuniandikia msg. na mambo yako mengine ambayo hujaandika hapa yatanyoka. mimi nilienda pale baada ya kuona mdogo wangu yamemnyookea, nimesali pale na karibia nitakuwa mchungaji pia. si siri wakubwa, usichezee. na wengine wote wenye tatizo kama hili, njooni BUREEE.

Upele umempata mkunaji..., naona thread umeiteka kabisaaa.
Angalia tu usianze kuhubiri na kunena kwa lugha...
 
miongoni mwa wanao kushauri hivyo wamo pia mawakala wa aliyekutumia ndege huyo, yaani washirikina wenziye hivo hao ni wapiga debe, sasa wewe usikubari kwenda huko bagamoyo, YESU tu ndiyo suruhisho lake watajisalimisha wote, nawe uwaombee na wakikuona unadunda wambie huyo ni yesu amefanya....maana imeandikwa tuwaombee wanaotuudhi...
 
Wapendwa nashukuruni woote mliochangia jambo hili, nimejifunza mengi kutoka kwenu.
Uamuzi wangu ni siri yangu, ila ushauri wenu umniongezea kujiamini mno kwamba kwa vyovyote vile hakuna jambo baya litakalo nitokea.......
Thanks............
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom