Kunguni (bedbugs) ni wadudu wenye uwezo wa kukaa mwaka mzima bila kula

Hofstede

JF-Expert Member
Jul 15, 2007
3,577
1,107
Pengine watu watajiuliza kuwa nini kimejiri mpaka kuwazungumzia wadudu hawa. Kunguni hawathibitika kuwa na uambukizi wa ugonjwa wowote kwa binadamu, ila ni wadudu ambao wasumbufu sana hasa nyakati za usiku ukiwa umelala, usiombe kulala hoteli yenye kunguni balaa, hili lilinitokea kipindi fulani nilikuwa nafanya field kijiji kimoja (magubike) tukalala hotelini siku kumi zilikuwa kama miaka kumi kwa usumbufu wa wadudu hawa. Swali ni je wadudu hawa hunawiri sehemu zenye hali gani?, Ninajua chawa humea zaidi kwa kutokuwa na usafi wa mwili,

Imegundulika pia kuwa wadudu hawa huishi vizuri hata sehemu safi kama mtakavyoona kwenye video hapo chini. Ni wachache sana kati yetu wanaoweza sema hawajawahi kuumwa na mdudu huyu kwani wapo sehemu mbalimbali, mahotelini, kwenye usafiri(daladala, train) na hata baadhi ya club za unywaji, majumbani na maofisini pia.

Kinachoshangaza pia ni uvumilivu wa mdudu huyu kuishi hata mwaka bila kunyonya damu huku akisubiri mtu apatikane.

Je wataalam wanaweza kutuelezea sababu za mdudu huyu kuwa uwezo mkubwa wa kuishi muda mrefu bila diet?

unaweza kufahamu zaidi mdudu huyu hapa Kunguni

au hapa chini
[ame="http://www.youtube.com/watch?v=lpkTC3bs4Cg"]kunguni2[/ame]
 
ni kweli wanaweza kukaa mwaka bila kula au wanakula vitu vingine mbali na damu
 
A number of health effects may occur due to bed bugs, including skin rashes, psychological effects, and allergic symptoms. Diagnosis involves both finding bed bugs and the occurrence of compatible symptoms. Treatment is otherwise symptomatic.
 
Sina hamu na hawa jamaa, walinishughulikia hadi nikawa natokwa maji kwenye kitovu! Nikapatwa na homa pia na mwili kuwashwa. Actually nilikuwa siwajui jamaa mmoja akaja geto akasema ww unalalamika kuumwa kila siku unajua sababu? Nikamwambia hapana. Akaniambia "kitandani kwako kuna kunguni". Baada ya kuwaua wote kweli sikuwashwa wala kutoka maji kitovuni.
Pia nilishawahi kwenda sehemu moja kunaitwa Kilindi nikalala kwenye Gesti ya kijijini; Aisee, usiku mmoja niliona kama mwaka mzima; Palikuwa hapatoshi, hakulaliki hakukaliki!
 
Uliwauwaje?
 
Back
Top Bottom