Kung'ara kwa E. Lowassa ndani ya CCM ni pigo la Mwaka kwa Nape Nnauye!

eedoh05

JF-Expert Member
Apr 20, 2011
632
234
Njia ya mwongo siku zote ni fupi. Pia wa kukosa atakosa tu. Toka kelele za Nape zianze dhidi ya Mh. Edward Lowassa inaonesha kelele hizo zinampaisha EL toka utukufu hadi utukufu. Akiwa kiongozi ndani ya umoja wa vijana ccm-UVCCM Nape alimtuhumu E.L. juu ya ufisadi wa mkataba wa ujenzi wa maghorofa pale kwenye viwanja vya UVCCM - barabara ya Morogoro DSM. Kelele zile hazikufua dafu.

Mara alipoteuliwa kuwa Katibu Mwenezi wa CCM, Nape akadhani kuwa amepata uwanja mpana wa kushindana na E.L. Bahati mbaya, akatutumka kwa nyodo na ngebe akajiaminisha kuwa atamsambaratisha E.Lowassa. Kumbe kelele za chura hazimtishi mteka maji. E.Lowassa anazidi kuyateka maji mbele ya chura; kibaya zaidi anayanywa maji hayo mbele ya huyo chura. Vikao vinavyomsafisha E. Lowassa, mfano CC na NEC msemaji wake ni Nape, Juzi kamtangaza E. Lowassa kupita mchujo wa wagombea u-NEC tokea Monduli. masikini Naapeee!...

Na si hivyo tu, hata wale wanaosemwa kuwa wafuasi na mashabiki wa E.Lowassa ndani ya chama wanaonekana kama ni maarufu kuliko huyo Nape. Hapo ndipo ninapodhani, ukitaka kumzibia mtu itakubidi upande juu kujenga zege kuziba mafanikio yake.

Edward Lowassa kweli ni mpambanaji ambaye huwageuza wabaya wake miguu juu vichwa chini, Nape kashageuzwa kichwa chini miguu juu, humsikii tena akibwabwaja juu ya mafisadi na ufisadi. Juzi hapa, ndani ya jamiiforums kuna mada ilisema usiku wa manane Nape alionekana akiwa pamoja na jopo lililotoa mlungula kwa mmoja wa waliokuwa madiwani wa CDM katika hoteli ya La Cairo jijini Mwanza. Kama ndivyo ilivyo, ni heri E. Lowassa asiyesema lolote juu ufisadi kuliko mnafiki nape; anakemea rushwa huku akitoa rushwa na hongo. HONGERA Edward Lowassa kwa kushinda vita dhidi ya unafiki wa Nape.

Katibu Mwenezi ni mkristo, akumbuke imeandikwa: utatoaje kibanzi kwenye jicho la mwenzio wakati wewe jichoni kwako kuna boriti?

ADIOS!
 
SSM ni pesa, huna pesa huna kura!!! EL ni influential and will remain so unless utajiri wake umetaifishwa!!! Kama mtu ana nguvu ya kupitisha wajumbe wake wa NEC waliokataliwa si mchezo.
 
eedoh05 Huyo ndie Nape ninayemfahamu, antumimia Rusian style ya unafiki. Ameirithi hii.
 
Last edited by a moderator:
eedoh05 Ndani ya CCM hata Kikwete anajua Lowasa ni maarifa kuliko wote including Nape ukinisha uliza wana CCM wenzake
 
Last edited by a moderator:
Huyu nape nadhani hata akiambiwa amlambe miguu EL hadharani atatii bila shuruti. Hakyanani njaa mbaya. Kwa namna ubao ulivyogeuka huwezi tena kumuamini nape, Kwa lipi sasa??? Huwezi kumwita mtu mwizi leo halafu kesho unampigia magoti??? nape sio mzalendo kabisa, hivi yale aliyokuwa akiyasema kuhusu wale mapacha wa3, yameishia wapi??? Au ndo anataka watanzania tujilazimishe kuya-delete kwenye vichwa vyetu halafu tujifanye kama vile hakuna tulichokisikia??? nape wewe huwezi kusimamia maadili, wewe ni fisadi mwenzao tuu. Itabidi ukamuombe radhi hadharani Rostam Aziz, ulimkosea saaana, mjinga sana wewe nape.
 
nape ndio vijana wanaochipuka ndani ya ccm wakiwa hawana maarifa ya kutetea ujana wao na elimu zao bali wanaangalia tumbo kwanza ndio uzalendo
 
mbuzi wa masikini hazai akizaa anazaa chongo........... makelele yote ya kuvua gamba sijui yameishia wapi.........masikini kijana huyu alifikiri ssm ni yakwake..........kumbe hajui ina wenyewe ................. akajipange upya sasa......na edo akikamata nchi nape kwishney atasahaulika kama mangula............
 
Ukiona mwanaume anatumia carolite,ujue kichwa chake hakina ubongo,anaweza akalopoka chochote bila kufikiria.
 
Naona Nape anawanyima usingizi magwanda. Hivi Slaa ameshaongea na waandishi wa habari au bado yuko nyumbani anaomboleza?
 
Duuh kijana Nape hamuwezi lowasa mwenye chama hakika atafukuzwa uenezi!

Nape na campaign yake ya kuvua gamba ndani ya ccm imegonga mwamba kwa lowasa!

Kumuona Ritz kwenye huu uzi ni nadra!
 
Back
Top Bottom