Kunaulazima wa kuwa na bajeti za magazeti ofisini, ili hali kuna internet?

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,987
20,270
Nimejaribu kuzungukia maofisi ya umma na binafsi tz hasa hapa bongo nikaona ofisi hizo zina bajeti ya magazeti ilihali zina mtandao wa internet!

Binafsi siamini kama mfanyakazi wa ofisi ya umma au binafsi anayatumia kikamilifu magazeti hayo zaidi ya mtandao wa internet.

Ndugu wana jf, kunaulazima wa kuwa na bajeti za magazeti ofisini? Na je mfanyakazi akiwa ofisini ni haki kutumia mtandao wa internet kwa shughuli zake?
 
Unaifahamu historia ya mmoja wa wafalme wa France ambaye alitawala wakati kulikuwa na njaa kubwa kwa wananchi wake?. Siku moja mmoja wa washauri wake alikuja na kumwambia mfalme wananchi wana njaa kubwa,mikate imepanda bei kiasi watu ni shida hata kupata selesi moja ya mkate kwa siku. Jibu la mfalme lilikuwa:WHY SHOULDN'T THEY EAT CAKE!. Maskini mfalme alikuwa hajui hiyo cake ipo maili millioni moja kwa maskini kuipata. Huyu mfalme alipinduliwa si muda mrefu baada ya kutoa kauli hii.Mara kadhaa tukiwa tumejitosheleza huwa tunasahau kwamba kuna wenzetu hawana hata kitu kidogo tulichonacho sisi!. Si kila ofisi ina internet facilities na by the way,kuna advantages za kusoma magazeti/vitabu phyically vs reading on internet.
 
Dah hiyo ofisi inadili na nini? Inawezekana hata Syimbioni Kikwete haina?!
Huwezi amini but huu ndio ukweli, ofisi hizi za wilaya 90% hazina computer, ndio ofisi zinazohudumia watumishi wengi wa serikali, Ni OFISI YA RAIS, TUME YA UTUMISHI WA UMMA, IDARA YA UTUMISHI WA WALIMU zinajulikana sana kama TSD. Uendeshaji wa ofisi ni mgumu coz wanasema hakuna fedha, walimu wanalazimika kugharamia nyaraka wanazohitaji. Hii ndio ofisi ya Rais Wilayani.
 
Wakati mwingine wanalazimisha na aina ya magazeti ya kuweka ofisini, Uhuru na Mzalendo tu!
 
Kaka ukiruhusu ofisini watu wasome magazeti hahha sijui km kazi zitafanyika. halafu internet kwa ofisi ni gharama zaidi ya magazeti baba
 
Huwezi amini but huu ndio ukweli, ofisi hizi za wilaya 90% hazina computer, ndio ofisi zinazohudumia watumishi wengi wa serikali, Ni OFISI YA RAIS, TUME YA UTUMISHI WA UMMA, IDARA YA UTUMISHI WA WALIMU zinajulikana sana kama TSD. Uendeshaji wa ofisi ni mgumu coz wanasema hakuna fedha, walimu wanalazimika kugharamia nyaraka wanazohitaji. Hii ndio ofisi ya Rais Wilayani.
Ebwana eheee hii ndo nalisikia leo! Kumbe tuliojili nanakosa mambo mengi sana! Yani ofisi inakuwa kama chuma cha sangoma?Halafu mbunge anaposho kumi na moja?????Huu ni utani na dhihaka kubwa kwa watz, ndio maana ukienda wilayani kufuatia nyaraka fulani basi waweza kuchukua hata miezi sita kwa ishu ya siku moja!
 
halafu internet kwa ofisi ni gharama zaidi ya magazeti baba

Chimunguru,
Si kweli kuwa Internet ni gharama kubwa kuliko kununua magazeti. Mbali na kuyapata mapema, pia unapata mengi ambayo gharama yake ni pungufu ya bei ya magazeti hayo kwa mwezi. Wajanja wengi siku hizi ngumu sana kufanya kazi kwenye ofisi isiyo na mtandao kwani imepunguza hata gharama za kutuma barua posta kila siku.
 
Pole ba jabir,huo ni wizi mtupu!hyo bajet ya magazet tena magazet ya chama tu/serikal ni kuwaibia waTZ,tena yakishasomwa bosi hurudi nayo kwake na wakat mwingne hayo magazet hubak ofisin kwa bosi ht wafanyakaz wngne hawasomi au hubak kwenye shangingi la muheshimiwa.km kuna internet ni bora wai2mie hyo kuliko kununua magazet.
 
Back
Top Bottom