Kunanini leo

frema120

JF-Expert Member
Jan 1, 2012
5,099
1,337
Habari wakuu?
naelekea airport nimekutana
na magari mengi sana ya
FFU defender na magari ya
kuwasha mawili.....

Yapo kasi sana,
mwenye taarifa yoyote
hatuzuje kama hali ni
tete tufunge maofisi.....

V
SENGEREMA
 
Waislam wote tunaenda kusali ijumaa kinondoni.bakwata na ccm vinalindwa kwa nguvu zote na polisi
 
Kutawalika kwa nchi ni pale nchi inapokuwa na utulivu na watu pamoja na serikali kufanya mambo yanayoleta maendeleo kwa ajili ya maisha ya kila siku na ya baadae, lakini kwa sasa naona hii nchi imeshindwa kutawalika kama viongozi wa CDM walivyosema hapo siku za nyuma kwani kila siku ni tifu tu hakuna mambo muhimu yanayofanyika kwa ajili ya maendeleo ya nchi hii si kwenye mikutano maneno ni ya hovyo matendo hovyo sijui tunakoelekea
 
C unajua leo hao jamaa walipanga leo baada ya swala wangeenda kumtoa Muft wa Bakwata na Ndalichako NECTA
 
habari wakuu?
Naelekea airport nimekutana
na magari mengi sana ya
ffu defender na magari ya
kuwasha mawili.....

Yapo kasi sana,
mwenye taarifa yoyote
hatuzuje kama hali ni
tete tufunge maofisi.....

V
sengerema


airport ya wapi? Kia au wapi? Be specific bwana
 
Kuna tetesi za waislam kuandamana baada ya sala ya mchana.These demos may be related to the demos seen in Egypt, Libya and Yemen targeting the US Embassies.
whatch out!
 
Kuna tetesi za waislam kuandamana baada ya sala ya mchana.These demos may be related to the demos seen in Egypt, Libya and Yemen...

Kwani kuna chochote kilichotokea huku Tz? Ile filamu iliyoleta hasira ni ya kipumbavu mtupu, na aliyeitengeneza atashtakiwa hata na waigizaji, kwani alibadilisha maneno waliyotamka ili kuchochea hasira za kidini. Mhusika ameshapatikana na ni mtapeli fulani kutoka Misri aliyesuka mpango huu akiwa jela Marekani. Story kamili inaweza kupatikana kwa kubofya hapa, ingawa bado inaendelea kupatiwa updates:
"Innocence of Muslims - Wikipedia, the free encyclopedia"
 
Kitu ambacho wengi tusichokiona ni nini vyanzo vya majanga bali tunapenda kudandia matukio yafuatayo!

Ukitazama kwa undani mathalani filamu hiyo ya kifedhuli kwanini imetangazwa tarehe inayohusiana na siku ya kulipuliwa WTC? Je nini kimejificha nyuma ya hilo? na kwanini litengenezwe na kuanzishiwa tarehe hiyohiyo? kama itatuwia vigumu kupata majawabu hapo haya basi na tujiulize ni kitu gani kilifanya kiwanda cha madawa cha Sudani kilipuliwe kwa mabomu!? Je nini kinawafanya hao waheshimiwa wanaoogopwa sana duniani waendelee kufanya mauaji kwa kutumia drone Afghanistan, Yemen, Pakistan na Somalia na kwanini si Turkey, Greece na Spain ambako pia kuna maandamano!?
 
Back
Top Bottom