Kunani tumaini iringa?

Mzito Kabwela

JF-Expert Member
Nov 28, 2009
18,857
7,615
Nimeona tangazo kwenye gazeti la Daily News la wiki iliyopita kwenye nafasi za Kazi. Imeandikwa kuwa Wanafunzi wa Tumaini Iringa waliosoma sheria wasiapply. Nani mwingine ameliona? Ni kwanini? Manake nilitaka nimpeleke mdogo wangu kusoma Sheria pale.

Yeyote mwenye uelewa na hicho chuo anisaidie tafadhali.

Mzi
 
Kama hali ni hii inamaanisha Mamlaka zinazohusika hasifanyi kazi yake ipasavyo. Wewe iweje Waziri na Mamlaka zinazohusiana na elimu waangalie chuo kinaanzishwa hakina vigezo then wakikubali. Huu ni uzembe Mkubwa. Kama ni waalimu mbona Graduates wengi sana tu. Na kama ni uongozi kwanini serikali isishirikiane na utawala wa chuo kuchunguza uzaifu upo wapi mpaka. Graduates hawa wa Tumaini wasikubalike. TUKIENDELEA HIVI IPO SIKU AJIRA ZITAKUWA ZINATANGAZWA KWA KUONYESHA WANAFUNZI WALIOMALIZA VYUO FULANI NDIO WANASTAHILI TU!. NAOMBA MUNGU TUSIFIKE HUKO.
 
Mi nahisi kuna issue nyingine tofauti.
Kwani wangeweza kuwamwaga kimya kimya kwenye kuteua short lists bila ya kutangazia umma kuwa wahitimu wa tumaini hawawataki.
 
Du nilikuwa nasubiri siku hii ifike ; Na si kwa matarajio ya furaha bali ni kwa huzuni! and the list will not stop here tutasikia mengi
 
Nimeona tangazo kwenye gazeti la Daily News la wiki iliyopita kwenye nafasi za Kazi. Imeandikwa kuwa Wanafunzi wa Tumaini Iringa waliosoma sheria wasiapply. Nani mwingine ameliona? Ni kwanini? Manake nilitaka nimpeleke mdogo wangu kusoma Sheria pale.

Yeyote mwenye uelewa na hicho chuo anisaidie tafadhali.

Mzi

Daily News ya lini na kampuni gani imesema hivyo? Nina Daily News ya leo hapa mezani kwangu na sioni kitu kama hicho!
 
Safi, hakuna mtu anayeweza kusema wanafunzi wa chuo fulani wasiapply, inawezekana baadhi ya wahitimu wa LLB Tumaini Univ. wameonyesha UPOPOPO wao kazini so jamaa wanaona ni kheri wawataarifu kabisaaa kuwa wasiapply au kuna ishu nyingine. Mi nashauri uongozi wa chuo chini ya Prof Bangu walifuatilie hili wajue kulikoni na pia wanachuo wawe serious jamani, tunajisahau sana katika masomo, starehe zimetutinga hatusomi na mwisho wa siku tunaingia na migi kwenye paper au hata kupewa paper ili ufaulu, kufaulu mitihani sio kigezo cha kujua masomo, unapokuwa kazini ndipo hapo hali huwa mbaya. Hii sio safi kabisa.
 
1.labda tayari walishaaply au wao walielekezwa wa apply vipi.
2.labda ni taasisi,shirika la dini hivyo haliwataki wale kwa vile linadhani watakuwa na msimamo fulani
 
hii post inanikumbusha ile post ya "kuna nini KCMC" je mnajua VC wa Iringa ndo yule Prof.Shao aliyepigiwa kelele kule KCMC hadi majuzi bodi ikamtema??je mnategemea product gani kwa VC huyu asiye kuwa na mahusiano mazuri na wafanyakazi wa Taaasisi anazoziongoza.Wadau tuchangie hili
 
Back
Top Bottom