Kunani CHADEMA?

ray jay

JF-Expert Member
Sep 27, 2011
1,084
485
KAULI ZENYE UTATA…..!!!
Wenje (Mbunge) v/s Adam Chagulani (Diwani)
Sababu "ukabila + kambi"
"Meya wa Mwanza hatufai ang'oke na wenje si msukuma hajali maendeleo yetu’’_Adam
‘’Adam ni mzushi na mkabila ni zao la Zitto Z Kabwe’’ Wenje
WENJE ANAJENGA KAMBI YA MBOWE, CHAGULANI KAMBI YA ZITTO.

Shibuda (Mbunge) v/s John Heche (Mkt BAVICHA)
Sababu "Ukanda +Kambi”
"Shibuda ni mamluki, hatumuhitaji arudi CCM’’_Heche
"Heche aniombe radhi na asitumie BAVICHA kwa maslahi yake, ninayajua mengi ya CHADEMA msinilazimishe niyamwage hadharani’’_Shibuda
HECHE ANATAJWA KATIKA WALINZI SHUPAVU WA “UNTOUCHABLE DOMINANCE” KTK CHAMA.


Mbowe v/s Sugu - kuhusu Clouds
Sababu "self-interest"
“Clouds wazushi , wanaibeba CCM na wanadhaminiwa na JK’’ Joseph Mbilinyi aka Sugu.
“Clouds ni chombo chetu sote, tunaweza kukitumia’’ Mbowe

Mwenyekiti BAVICHA v/s Makamu Mwenyekiti BAVICHA.`
Sababu “power factor”
“Tamko la Heche ni tamko lake, mimi sikushirikishwa wala hakukuwa na kikao cha kuidhinisha kauli hiyo, ana sababu binafsi na BAVICHA halihusiani nazo _ Makamu Mwenyekiti”
“Tamko la mwenyekiti ni tamko la BARAZA _ Mwenyekiti”


Dr. Slaa V/S Lema
Sababu " Uongo wa Lema"
" Kauli ya Lema juu ya Vigogo wa CCM kuhamia Chadema si kauli ya Chama ni yake mwenyewe kwa kuwa sisi kama chama hatuna taarifa rasmi juu ya hilo’’ *_ Dr. Slaa

My take;
Katika kipindi cha miaka michache hapo nyuma tulishuhudia kasi kubwa ya kukua kwa chama hiki na watanzania walio wengi hasa vijana wakionesha kukikubali na kukipenda. Ni chama ambacho kiliweza kutoa fursa kwa kila mmoja kushiriki shughuli za chama, kuchagua na kugombea. Tuliweza kuona vijana wengi wakipata nafasi kama madiwani na wabunge na hili lilihamasisha wengine kukiamini na kuwatumia vijana hawa kama mifano hai.

Imani imeanza kupotea:
Kulingana na matukio mbalimbali ndani ya chama hasa migongano na mifarakano ambayo imekuwa ikiendelea na kufikia baadhi ya watu kutishiwa ama kufukuzwa kabisa uanachama ktk chama.
Akihojiwa juzi na Clouds Fm Mhe. Mbowe alidai kuwa “mifarakano hii si jambo la msingi na mwenye akili hapaswi kujadili hili” kauli hii kutoka kwa Mwenyekiti wa Chama imeshtua wengi, kwani mifarakano hiyo ambayo haina msingi wa kuimarisha chama na haina misingi ya kikatiba wala kisera katika chama bali ni matakwa ya watu na hulka binafsi ni vitu vinavyotishia uhai na makuzi ya Chama,KWA MTAZOMO WANGU-MIFARAKANO HII NI VYEMA IJADILIWE TENA KWENYE KAMATI YA MAADILI NA KUTOLEWA KARIPIO KALI.

Ni nani hasa “UNTOUCHABLE DOMINANCE” katika CHADEMA…?
Ukifuatilia kwa undani mifarakano hii katika Chama inayo sababu zinazoshabihiana sana na mfanano wa hali ya juu, yote kwa pamoja yanatokana na kuwepo kwa kundi hili la “untouchable dominance” ambalo Mbowe anatajwa kuwa ni kinara wake na ndio maana anajaribu kuweka namna ya kutojadiliwa mifarakano hiyo. Tangu kuasisiwa kwake Chadema kumekuwepo na dhana hii ya kuwepo watu rasmi kuandaliwa kwa nafasi Fulani ya juu ya chama hicho. Mnamo mwaka 2004 katika mchakato wa kumpata mgombea urais, alinukuliwa muasisi wa chama hiko Mzee Mtei akieleza kauli inayofafanua hili linaloendelea leo katika Chama, alisema kwa kutumia lugha ya kigeni “.. We can’t give this position to anyone ..”
 

Attachments

  • KUNANI CHADEMA.docx
    17.5 KB · Views: 98
Acha upotoshaji wa wazi wazi CDM pako shwari,wewe ndo hujielewi
 
mleta thread apongezwe kwa jumla kwamba kwa akili zake zote hiki ndicho kitu chema kabisa alichotuletea.Pongezi hizi hazina maana kuwa alicholeta ni sahihi!
 
​du tukiweka za ccm page itajaa hivyo rudi hukohuko hatukutaki humu pole sana na siasa za maji taka
 
​du tukiweka za ccm page itajaa hivyo rudi hukohuko hatukutaki humu pole sana na siasa za maji taka
 
mbona mnatumia usalama wa taifa kuwawinda ili muwauwe si magarasa hayo upepo umekataa kupita mkaja na mbinu mpya liwalo na liwe?
 
Mh!mnjamba jamba kisa cdm imewashika kunako mumeshindw sasa mnaleta usalama wa taifa magamba na cuf hamna maana nendeni kuzimu huko.
 
Mkuu fuatilia red hapo chini. Halafu uje tena
KAULI ZENYE UTATA…..!!!
Wenje (Mbunge) v/s Adam Chagulani (Diwani)
Sababu "ukabila + kambi"
"Meya wa Mwanza hatufai ang'oke na wenje si msukuma hajali maendeleo yetu''_Adam
''Adam ni mzushi na mkabila ni zao la Zitto Z Kabwe'' Wenje
WENJE ANAJENGA KAMBI YA MBOWE, CHAGULANI KAMBI YA ZITTO.

Shibuda (Mbunge) v/s John Heche (Mkt BAVICHA)
Sababu "Ukanda +Kambi"
"Shibuda ni mamluki, hatumuhitaji arudi CCM''_Heche
"Heche aniombe radhi na asitumie BAVICHA kwa maslahi yake, ninayajua mengi ya CHADEMA msinilazimishe niyamwage hadharani''_Shibuda
HECHE ANATAJWA KATIKA WALINZI SHUPAVU WA "UNTOUCHABLE DOMINANCE" KTK CHAMA.

Msimamo wa Chama ktk hili unajulikana wala hakuna mgawanyiko.

Mbowe v/s Sugu - kuhusu Clouds
Sababu "self-interest"
"Clouds wazushi , wanaibeba CCM na wanadhaminiwa na JK'' Joseph Mbilinyi aka Sugu.
"Clouds ni chombo chetu sote, tunaweza kukitumia'' Mbowe
Hapa umepotosha makusudi. Nilimsikiliza Mbowe mimi mwenyewe. Mbowe alikubaliana kabisa na Sugu kuwa Clouds walikuwa tatizo kwao. Hivyo, siku walipomkabisha Mbowe ndo wakakubaliana uwe ndo mwanzo mpya wa Clouds kutopendelea ccm wala chadema, kwamba kitakuwa Chombo cha habari cha vyama vyote. Tofauti ya Sugu na Mbowe iko wapi?
Mwenyekiti BAVICHA v/s Makamu Mwenyekiti BAVICHA.`
Sababu "power factor"
"Tamko la Heche ni tamko lake, mimi sikushirikishwa wala hakukuwa na kikao cha kuidhinisha kauli hiyo, ana sababu binafsi na BAVICHA halihusiani nazo _ Makamu Mwenyekiti"
"Tamko la mwenyekiti ni tamko la BARAZA _ Mwenyekiti"
This is very minor issue to be honesty. Halafu hawa wote ni viongozi wa baraza walioko chini ya katibu mkuu. Kwa maoni yangu, Makamu aliteleza na ndo maana sasa baada ya kuelekezwa amekaa kimya. Huwezi kutegemea jambo hili likaisumbua Chadema in the future. Ni dogo sana

Dr. Slaa V/S Lema
Sababu " Uongo wa Lema"
" Kauli ya Lema juu ya Vigogo wa CCM kuhamia Chadema si kauli ya Chama ni yake mwenyewe kwa kuwa sisi kama chama hatuna taarifa rasmi juu ya hilo'' *_ Dr. Slaa

Wewe umesikia wapi lema akimpinga Dr Slaa kuwa hiyo ni kauli ya Chadema? Lema is right anaongea anachojua and msg sent. Dr Slaa is right, ile siyo tamko la Chama bali maoni ya Lema. Tatizo liko wapi?
Mwisho, ndani ya Chadema hakuna makambi mkuu, hiyo ni strategy ya magamba.
 
Ata kule South Afrika wanaharakati wa ukombozi walikuwa wanatofautiana ki mtazamo mara nyingine lakini mwisho wote kwa pamoja wakaikomboa South Afrika kutoka kwenye serikali dhalimu ya KIKABURU ambayo kwa matendo yake haina tofauti na serikali ya CCM refer to ULIMBOKA incidence utaelewa.
 
WALA MSIHANGAIKE WADAU WANGU WA CHADEMA NA HUYU MWEHU ALIELETA HII THREAD , NENO MOJA TUU LINAMTOSHA NALO NI HILI
-du tukiweka za ccm page itajaa hivyo rudi hukohuko hatukutaki humu pole sana na siasa za maji taka

-mbona mnatumia usalama wa taifa kuwawinda ili muwauwe si magarasa hayo upepo umekataa kupita mkaja na mbinu mpya liwalo na liwe?
 
M4C inapigwa mawe ndani ya serikali,Chama,Tiss, magamba na Makada ambao wote ni 5% na inakubalika na Umma ambao ni 95%. hauitaji kuwa na Phd ya online kutambua hili.
 
Ahsante sana kwa majibu mazuri...waumbue chadema ni moto moto moto wa kuotea mbali......
 
Back
Top Bottom