majata
JF-Expert Member
- Oct 7, 2010
- 431
- 179
ukiangalia kwa kina mwenendo wa nchi yetu kwasasa unaweza kukubaliana na mimi kwamba hali ya taifa letu imefika pabaya, nasema hivyo kutokana na mambo yanayoendele nchinichini.
Mfano: mgomo wa madaktari, migomo ya walimu, migomo ya wafanyakazi, kuporomoka kwa shilingi yetu, na hali ngumu ya maisha kwa asilimia kubwa ya watanzania.
Ukiangalia kwa kirahisi mambo haya yanaonekana ni madogo kwani mara kadhaa yametokea lakini yamekuwa yakizima yenyewe bila sababu za msingi na serikali inajisahau kutafuta suruhu ya kudumu pindi yanapokuwa yameisha, hii inafanana na kupuuzia volcano hai eti kwasababu inaunguruma tu na haijawahi kulipuka.
Itafika wakati migomo hii itapata mafuta baada ya kuungwa mkono na wananchi kwani wananchi wengi wamechoshwa na yanayoendelea katika nchi yao, watawala hasa rais na wabunge wamewasaliti raia waliowapa kura(hasa wabunge wa ccm) hata inapobidi kujadili mambo yenye maslahi ya taifa wao wanaangalia wasikiudhi chama.
Kuliepusha swala hili viongozi hasa wabunge wajadili mambo yenye maslahi
Kwa taifa kama wabunge huru na sio kama watumwa wa vyama vya siasa.
"Viongozi nafasi iliyopo kutuepusha na machafuko ni sasa, msidharau matatizo ya wenzenu wakati yakwenu mnatatua maramoja"