Kuna watu tunaimani na mwanahalisi kuliko hata serikali yetu

Nani ambaye hajui kuwa Kubenea anahudhuria vikao vya propaganda kule CDM? Unategemea aende kinyume na maazimio ya vikao?

Serikali ya JK bwana ngangari kweli, pamoja na mtandao wa propaganda ulioandaliwa na CDM bado inadunda na kwa bahati nzuri wananchi walio wengi wameshajua janja hiyo ya CDM. Mbona akina Ananilea Nkya Hellen Kijo Bisimba wako kimya? au bado wanaandaa zengwe lingine ili watakapoibuka CCM chali? tehe tehe tehe, JK usihofu Watanzania walio wengi wako nyuma yako.
MWANAHALISI ndo usalama wetu wa taifa,TISS imejaa wahuni wanaolinda wahuni wenzao na sio mali zetu kama taifa
 
Mitaa gani hiyo unayokaa ambayo ina watu wenye uwezo mdogo wa kuchanganua mambo hivyo? Lazima utakuwa ulisoma zile shule za SCHOOL BUS ambazo hazifundishi uraia tangu mwanzo. Kuna uhusiano gani kati Gazeti na Serikali? Kweli wewe ni mweupe.
wakati serikali inahangaika kutuaminisha kuwa mwanahalisi ni gazeti la uzushi na uchochezi asilimia kubwa ya wananchi ninaokaa nao huku mitaani wanasisitiza kuwa WANALIAMINI MWANAHALISI KULIKO SERIKALI YETU
 
MWANAHALISI ndo usalama wetu wa taifa,TISS imejaa wahuni wanaolinda wahuni wenzao na sio mali zetu kama taifa

Father of All kanena. Unajua hakuna tofauti kati ya kubenea na Ulimboka. Hivi Ulimboka anathubutu vipi kusema kuwa mtu aliyemtesa walikuwa wanakutana mara kwa mara? wapi? kwa nini? na je madaktari waliomtuma walikuwa wakilijua hilo. Tutajuaje sasa kama Ulimboka hajutii kipigo alichopata kwa sababu tayari alishajazwa mapesa?

Ningekuwa chama cha Madaktari, Ulimboka ni Jambazi kwa chama hicho, baada ya matibabu kama binadamu mwenzetu, ambacho kingefuatia ni kumshtaki kwa vile alisaliti waliomtuma kwa kwenda kufanya mikutano ya faragha na watu wasihusika.
 
Nani ambaye hajui kuwa Kubenea anahudhuria vikao vya propaganda kule CDM? Unategemea aende kinyume na maazimio ya vikao?

Serikali ya JK bwana ngangari kweli, pamoja na mtandao wa propaganda ulioandaliwa na CDM bado inadunda na kwa bahati nzuri wananchi walio wengi wameshajua janja hiyo ya CDM. Mbona akina Ananilea Nkya Hellen Kijo Bisimba wako kimya? au bado wanaandaa zengwe lingine ili watakapoibuka CCM chali? tehe tehe tehe, JK usihofu Watanzania walio wengi wako nyuma yako.
Inafaa uweke habari unazoziita za propaganda zilizoandikwa na Mwanahalisi!.

Maana kama hazipo basi wewe ndiyo unapropaganda uchwala!.
 
Father of All kanena. Unajua hakuna tofauti kati ya kubenea na Ulimboka. Hivi Ulimboka anathubutu vipi kusema kuwa mtu aliyemtesa walikuwa wanakutana mara kwa mara? wapi? kwa nini? na je madaktari waliomtuma walikuwa wakilijua hilo. Tutajuaje sasa kama Ulimboka hajutii kipigo alichopata kwa sababu tayari alishajazwa mapesa?

Ningekuwa chama cha Madaktari, Ulimboka ni Jambazi kwa chama hicho, baada ya matibabu kama binadamu mwenzetu, ambacho kingefuatia ni kumshtaki kwa vile alisaliti waliomtuma kwa kwenda kufanya mikutano ya faragha na watu wasihusika.
Kama ni kweli alijazwa mapesa,
1.je alijazwa na nani?
2.kwa faida ya nani?
3.na ili iweje? au kwanini?
4.hayo mapesa ilikuwa ni rushwa au mshahara?
 
wakati serikali inahangaika kutuaminisha kuwa mwanahalisi ni gazeti la uzushi na uchochezi asilimia kubwa ya wananchi ninaokaa nao huku mitaani wanasisitiza kuwa WANALIAMINI MWANAHALISI KULIKO SERIKALI YETU

Huku mitaani kwetu wananchi wengi wanyonge wanashukuru sana kwa kipigo alichopata ULIMBOKA kwa vile sasa wanapata matibabu kama kawaida, na wanashangaa kwa nini Serikali haikumshataki Said kubenea kwa nini anamtetea mtu ambaye alikuwa ni tishio kwa afya za wanyonge kuliko hata gonjwa hatari za Ukimwi.
 
Mi naona Mwanahalisi na serikali lao moja sema wamepishana lugha. Isingekuwa hivyo Kubenea asingefaidi pesa ya serikali kwenda India kila wiki eti kutibiwa. Kubenea ni mtu wao ingawa wamepishana lugha,msipate taabu watasuluhisha na kurudiana just soon.

Haya majina yenu mengine bana, we unaitwa father of all lakini matendo yako na mtazamo wako wala havifanani na jina lako, kwanini hata usingejiita Zero brain?
 
Kama ni kweli alijazwa mapesa,
1.je alijazwa na nani?
2.kwa faida ya nani?
3.na ili iweje? au kwanini?
4.hayo mapesa ilikuwa ni rushwa au mshahara?

Safi sana hayo ndiyo maswali ambayo Chama cha Madaktari kinapaswa kumuuliza Ulimboka atakapopona ili aweleze watanzania kama alitumwa na madaktari kudai haki zo kwenye bar.
 
mimi sikuichagua hii serikali,sina imani nayo hata chembe.

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
 
Haya majina yenu mengine bana, we unaitwa father of all lakini matendo yako na mtazamo wako wala havifanani na jina lako, kwanini hata usingejiita Zero brain?

Tatizo hpa JF mtu akiongea mambo ya msingi anapondwa, Father kasema kweli. Kwanza wewe Kakubilo siamini kama wewe ni Mtanzania, siyo Wanyasa wa Malawi mnaotusumbua kule Ziwa Nyasa?. Unamtetea Kubenea kwa madudu yake, eti anahojiwa BBC kwa nini amefungiwa anasema "kwa sababu naandika habari za kiuchungi ambazo vyombo vingine vinaopopa kuandika" Alifikiri BBC wametandaza nafasi za kazi akaanza kuponda wanahabari wenzake ili yeye apate kazi nini?
 
Father of All kanena. Unajua hakuna tofauti kati ya kubenea na Ulimboka. Hivi Ulimboka anathubutu vipi kusema kuwa mtu aliyemtesa walikuwa wanakutana mara kwa mara? wapi? kwa nini? na je madaktari waliomtuma walikuwa wakilijua hilo. Tutajuaje sasa kama Ulimboka hajutii kipigo alichopata kwa sababu tayari alishajazwa mapesa?

Ningekuwa chama cha Madaktari, Ulimboka ni Jambazi kwa chama hicho, baada ya matibabu kama binadamu mwenzetu, ambacho kingefuatia ni kumshtaki kwa vile alisaliti waliomtuma kwa kwenda kufanya mikutano ya faragha na watu wasihusika.

Kama ni kweli alijazwa mapesa,
1.je alijazwa na nani?
2.kwa faida ya nani?
3.na ili iweje? au kwanini?
4.hayo mapesa ilikuwa ni rushwa au mshahara?

Safi sana hayo ndiyo maswali ambayo Chama cha Madaktari kinapaswa kumuuliza Ulimboka atakapopona ili aweleze watanzania kama alitumwa na madaktari kudai haki zo kwenye bar.
Tusubiri Uli kujibu wakati kuna mtu anajua!.
Angalia hapo nilipopweka nyekundu, thatha kwa kauli hiyo lazima na majibu ya maswali unayo.
 
Tatizo hpa JF mtu akiongea mambo ya msingi anapondwa, Father kasema kweli. Kwanza wewe Kakubilo siamini kama wewe ni Mtanzania, siyo Wanyasa wa Malawi mnaotusumbua kule Ziwa Nyasa?. Unamtetea Kubenea kwa madudu yake, eti anahojiwa BBC kwa nini amefungiwa anasema "kwa sababu naandika habari za kiuchungi ambazo vyombo vingine vinaopopa kuandika" Alifikiri BBC wametandaza nafasi za kazi akaanza kuponda wanahabari wenzake ili yeye apate kazi nini?
Ulitaka asijibu swali au jibu ndilo hukulipenda?.
Serikali haipendi uhuru wa vyombo vya habari na wanahabari, kumbuka yaliyomtokea aliyekuwa mkurugenzi wa TBC, kisa aliweka usawa katika chombo cha taifa wakati wa kampeni za uchaguzi 2010 na kuwaelimisha wananchi juu ya haki yao za kuchagua viongozi wao!
 
Huku mitaani kwetu wananchi wengi wanyonge wanashukuru sana kwa kipigo alichopata ULIMBOKA kwa vile sasa wanapata matibabu kama kawaida, na wanashangaa kwa nini Serikali haikumshataki Said kubenea kwa nini anamtetea mtu ambaye alikuwa ni tishio kwa afya za wanyonge kuliko hata gonjwa hatari za Ukimwi.
Huu ndio msimamo na mtazamo wa majitu yanayo nufaika na "system" ya kifisadi na rushwa. Mlaaniwe!
 
Mi naona Mwanahalisi na serikali lao moja sema wamepishana lugha. Isingekuwa hivyo Kubenea asingefaidi pesa ya serikali kwenda India kila wiki eti kutibiwa. Kubenea ni mtu wao ingawa wamepishana lugha,msipate taabu watasuluhisha na kurudiana just soon.

Hayo ni mawazo ya ajabu kuamini kuwa kwa kuwa serikali inagharamia matibabu ya Kubenea, basi lao moja. Hivi kuna mtu anaweza kushirikiana na mtu anayetaka kukuua? Serikali inapaswa kuwatibu watu wote hata kama haiwapendi.

Pesa ilizonazo serikali ni za wananchi wote wanaoipenda hata wanaoichukia. Hilo ni jambo moja, lakini la pili serikali, kwa kugharamia matibabu ya Kubenea, ina lengo la kujikosha kwa ubaya iliomtendea ili angalao Kubenea aone kama wanampenda. Pengine iwapate wajinga wachache watakaoamini kuwa serikali haihusiki na sakata la kumwagiwa tindikali na wajinga zaidi ni wale watakaoamini kuwa Kubenea na Serikali, lao moja.

Serikali inataka kujenga urafiki na Kubenea kwa kugharamia matibabu ambayo msingi wake ni serikali. Nina hakika Kubenea hawezi kuisamehe serikali kwa kuchelea mateso ya tindikali LIWALO NA LIWE, Kubenea ataendelea kuianika mpaka itakapotubu. Hata ningalikuwa mimi nisingaliisamehe kamwe.
 
Wana jf tunapashwa kutambua jambo moja kuwa kwenye mtandao wa mafisadi lazima kuna makuadi wake kibao , watatetea mpaka povu liwatoke sababu ni kama mbwa wanasubiri kula makombo ya mabwana zao mfano mzuri ni akina ritz na wengi wa aina hiyo.

Siyo siiri kwamba kila mtu mwenye macho na akili anajua nchi hii mambo yanavyokwenda kombo. Ufisadi na uchafu mwingi unafanywa na viongozi wetu tulio wachagua.kila mtu anakiri kuwa kuna ufisadi, lakini hakuna hata mmoja anasema fisadi ni huyu.

Serikali yenyewe inakiri kuwa kuna ufisadi wa kutisha lakini wakati huo huo inaogopa kusema mafisadi ni akina nani. Sasa tumwamini nani kama serikali na vyombo vyake vyote vinakuwa na kigugumizi kutaja mafisadi ,si afadhali mwanahalisi wanathubutu kusema na ndio maana tunawaamini.

Nchi yenye asali na maziwa inakuwaje nchi ya mwisho kwa umasikini ? Viogozi wezi wameigeuza nchi hii jalala!!!!!!!!! Mungu tunusuru tunaitaji mageuzi ya mfumo mzima hata kama hayatatuletea tija lakini angalau tuondokane na baraha la vingozi uchwala hawa
 
Nikiulizwa leo nimpe nani tuzo ya mwandishi jasiri wa habari za uchunguzi ,
jibu langu ni moja tu...SAID KUBENEA.

Mnaomponda inawezekana mnafanya hivyo ajili ya matumbo yenu, kubenea huwezi kumlinganisha na waandishi wa gazeti 'kongwe la chama cha mapinduzi' ambao mbele ya hela wapo tayari kuita kijiko kuwa ni koleo!

Binafsi namlinganisha Kubenea na shujaa mwingine wa tasnia ya habari HAYATI STAN KATABALO,RIP.
 
Nani ambaye hajui kuwa Kubenea anahudhuria vikao vya propaganda kule CDM? Unategemea aende kinyume na maazimio ya vikao?

Serikali ya JK bwana ngangari kweli, pamoja na mtandao wa propaganda ulioandaliwa na CDM bado inadunda na kwa bahati nzuri wananchi walio wengi wameshajua janja hiyo ya CDM. Mbona akina Ananilea Nkya Hellen Kijo Bisimba wako kimya? au bado wanaandaa zengwe lingine ili watakapoibuka CCM chali? tehe tehe tehe, JK usihofu Watanzania walio wengi wako nyuma yako.
Hayo ndio uliyoyapata kwenye hivyo vikao venu vya gongo?
 
kwenye dunia ya sayansi ya habari tunayoishi sasa, bila kuwa na ushahidi wa kisayansi na vigezo watu watakudharau. Mwanahalisi wametupa taarifaf za kisayansi kuwa baada ya kuwasiliana na huyu alikuwa anawasiliana na huyu. Hizi ni taarifa ambazo hata leo ukienda kwenye mitandao ya simu zipo. Kukanusha ni kwa wahusika wangeenda mahakamani na sio kufungia gazeti.
 
Back
Top Bottom