Kuna vituo vingapi vya "Fire" vya Serikali Dar?

On the same infrastructure tip...vipi zile sehemu ambako watu wamejenga kiholela holela? Maana kuna sehemu kama pale Tabata, Ubungo, au hata mitaa ya Tangi bovu ambako hakuna njia hata gari na hata baiskeli na pikipiki hazifiki. Kuna nyumba na sehemu za starehe (baa na migahawa) zinazofikika kwa miguu tu. Huko kukitokea moto itakuwaje?

Hivi kweli tunaamini watu hujenga "holela"?
 
Hivi kweli tunaamini watu hujenga "holela"?

Nah...you know what I meant. Ndio, watu wamejenga lakini wamejenga kwa kupewa ruhusa (rasmi or otherwise) kujenga kwenye maeneo hayo.

Hivyo viwanja kwanza sidhani hata kama vimepimwa kitaalamu maana vipi vipo tu. Na nadhani kuna ushahidi wa kutosha kuthibitisha kuwa viwanja hivyo hutolewa kifisadi fisadi.

The whole allocation scheme is orchestrated by mafisadi and people with ufisadi tendencies. We all know that.
 
Oh kitu kingine....mifumo mingine ya dharura (emergency systems) ikoje? Kwa mfano mtu akiwa nyumbani kwake na ghafla bin vuu anaanza kusikia maumivu ya kifua (possible heart attack). Mtu huyo ana options gani? Do emergency systems such as 911 or 999 work? are they even there?

Na hospitali kubwa kama za wilaya na mikoa zina magari mangapi ya kubebea wagonjwa? Ok, hata kama wanayo ya kutosha, mtu akipatwa na dharura ataweza kweli kupiga simu na kutoa directions za alipo?

Wait a minute....I think I'm getting way ahead of myself and going too far here....Lol
 
Jengo lenyewe la wizara ya mambo ya ndani pia liliwahi kuungua - sitakaa nisahau kumwona polisi akipiga simu 999 - kisa ? makao makuu ya wanausalama yanaungua ! Tunakoelekea kuna siku tutakuta makao makuu ya polisi yanalindwa na kikampuni binafsi cha polisi kama ultimate security au msaada wa makampuni binafsi za fire ukitafutwa kuzima moto kwenye makao makuu ya fire brigade ya city. Huko ndiko tunakopelekwa na serikali yetu hii ya CCM kwani si ajabu akatokea mtu kama the Boss wa JF na kutulaumu kwa kulilia huduma za bure za serikali.
 
Hapa mnakosea. tatizo ni kuwa swali la Mzee Mwanakijiji halitoshelezi.


FM.. swali langu halijakosewa kwa sababu lengo lake ni kuchokoza; gari la faya si suluhisho la matatizo ya moto kwenye mji mkubwa kama wa Dar.

Kinachotakiwa kuulizwa ni kuna infrastucture ya aina gani ya kupambana na moto katika jiji la Dar es Salaam? Gari la zimamoto hata siku moja halitakiwi kutegemea maji iliyoyabeba peke yake kupigana na moto. Panatakiwa kuwa na fire hydrants sehemu nyingi ili gari liweze kufyonza maji hapo. Kwenye majengo makubwa panatakiwa na njia ya maji iliyokuwa dedicated kwa ajili ya kuweza kufyonzwa panapotokea janga la moto. Zimamoto wanapokuja kwenye tukio wanatakiwa kuunganisha mipira yao hapo, yale ya kwenye gari ni ya hatua za mwanzo tu.

Hii ni nadharia na halisia ya kitu ambacho mtu yeyote anayetaka kupambana na moto au majanga ya moto anatakiwa kujua. Miundombinu hii inahitajika lakini guess what.. serikali imeonelea ni bora kujenga barabara za "juu kwa juu" ili tuonekane kama majuu!

Tulikuwa na system ya fire hydrants katika sehemu ya jiji letu na hata katika majengo lakini kama kawaida yetu tuliona ni anasa na hatukuzihudumia mpaka sasa hivi zimebakia historia.

Wao watauliza zina umuhimu gani wakati wanaweza kuagiza zile fire extinguishers kwa kila jumba huko wao wenyewe ndio wenye maduka au rafiki zao wenye maduka ya kuingiza vitu hivyo?

Tujiulize kuna vifaa vingapi vya kupigana na moto katika kumbi zetu za starehe, nyingi ambazo zimeezekwa na makuti? Zaidi ya hapo, ni wangapi wanajua kuvitumia ? Na jee sehemu za milango ya tahadhari ziko wazi na zinaweza kutumika? Mara nyingi milango hii utakuta imewekewe grili kwa nje ili kuzuia vibaka! Ngazi ngapi za tahadhari ziko wazi katika majengo yetu? Ni mara ngapi wafanyakazi na wanafunzi katika maofisi, mashule, hospitali wamepewa faya drill ili kuhakikisha kuwa wanajua nini cha kufanya panapotokea moto? Vituo ni nyongeza tu, ni sehemu ya infrastructure na tamaduni nzima ya kupambana na moto. Matatizo yetu ni makubwa kuliko uhaba wa vituo na vitendea kazi!

FM.. haya unayoyasema tulishayapigia kelele kwenye vifo vya watoto Tabora watu wakaona tunataka kulipiza kisasi, tukapigia kelele kwenye milipuko ya Mbagala tukaonekana tunaleta "siasa".. kimsingi hakuna ambacho tutakisema au kukipendekeza leo hii ambacho hakijulikani umuhimu wake au hatujawahi kukipendekeza huko nyuma.


Ndio maana elimu peke yake siyo suluhisho la matatizo yetu; watu wetu wanajua sana hadi hawajui nini cha kufanya!
 
Oh kitu kingine....mifumo mingine ya dharura (emergency systems) ikoje? Kwa mfano mtu akiwa nyumbani kwake na ghafla bin vuu anaanza kusikia maumivu ya kifua (possible heart attack). Mtu huyo ana options gani? Do emergency systems such as 911 or 999 work? are they even there?

wewe unauliza hili.. kwani yule Mbunge aliyepata pressure Bungeni walimfanya nini? si walimpepea? Hiyo ndiyo emergency response 101; kwani wale watoto waliokufa TABORA kwa kukosa hewa huku mijitu na akili zao inapumua pembeni walifanyiwa nini zaidi ya kunyanyuliwa na kuwekwa nje kupungwa na upepo badala ya CPR! na kiongozi mmoja smart akaja na 'mapenzi ya Mungu' ya "bwana ametoa na bwana ametwaa"
 
Tatizo ni serikali ya Chama Cha Majambazi ambayo haielewi ni vipi tutaendelea na tunakwenda vipi huko tunakotaka kwenda. Wao wamepata madaraka na priority zao ni kwenda kujionyesha nje ya nchi kwa mabwana zao.
 
wewe unauliza hili.. kwani yule Mbunge aliyepata pressure Bungeni walimfanya nini? si walimpepea? Hiyo ndiyo emergency response 101; kwani wale watoto waliokufa TABORA kwa kukosa hewa huku mijitu na akili zao inapumua pembeni walifanyiwa nini zaidi ya kunyanyuliwa na kuwekwa nje kupungwa na upepo badala ya CPR! na kiongozi mmoja smart akaja na 'mapenzi ya Mungu' ya "bwana ametoa na bwana ametwaa"
si ya kucheka lakini inabidi emergeny response 101 kipepeo tu.
 
Hapa mnakosea. tatizo ni kuwa swali la Mzee Mwanakijiji halitoshelezi. Kinachotakiwa kuulizwa ni kuna infrastucture ya aina gani ya kupambana na moto katika jiji la Dar es Salaam? Gari la zimamoto hata siku moja halitakiwi kutegemea maji iliyoyabeba peke yake kupigana na moto. Panatakiwa kuwa na fire hydrants sehemu nyingi ili gari liweze kufyonza maji hapo. Kwenye majengo makubwa panatakiwa na njia ya maji iliyokuwa dedicated kwa ajili ya kuweza kufyonzwa panapotokea janga la moto. Zimamoto wanapokuja kwenye tukio wanatakiwa kuunganisha mipira yao hapo, yale ya kwenye gari ni ya hatua za mwanzo tu. Tulikuwa na system ya fire hydrants katika sehemu ya jiji letu na hata katika majengo lakini kama kawaida yetu tuliona ni anasa na hatukuzihudumia mpaka sasa hivi zimebakia historia. Tujiulize kuna vifaa vingapi vya kupigana na moto katika kumbi zetu za starehe, nyingi ambazo zimeezekwa na makuti? Zaidi ya hapo, ni wangapi wanajua kuvitumia ? Na jee sehemu za milango ya tahadhari ziko wazi na zinaweza kutumika? Mara nyingi milango hii utakuta imewekewe grili kwa nje ili kuzuia vibaka! Ngazi ngapi za tahadhari ziko wazi katika majengo yetu? Ni mara ngapi wafanyakazi na wanafunzi katika maofisi, mashule, hospitali wamepewa faya drill ili kuhakikisha kuwa wanajua nini cha kufanya panapotokea moto? Vituo ni nyongeza tu, ni sehemu ya infrastructure na tamaduni nzima ya kupambana na moto. Matatizo yetu ni makubwa kuliko uhaba wa vituo na vitendea kazi!

Amandla..........

Mkuu, umenikumbusha mbali. Bugando Hospital madaktari wamejengewa nyumba za mbao. Uliposema fire hiydrants nikazikumbuka kwani ziko kila jirani na nyumba ya daktari. Sijui hizo hydrants zinafanya kazi hadi leo au la.

Mwanakijiji amekumbusha kwamba hatukujifunza Ikulu ilipoungua. Binafsi nilijifunza nini Ikulu ilipoungua?

Mimi nilijifunza kwamba huduma kama fire, ambulance tayari zilishabinafsishwa rasmi hata kama haikutangazwa. Ule moto wa Ikulu haukuolewa na Fire mnayoipigia kelele. Ni kama vile mmesahau kwamba moto ule ulizimwa na Fire Section ya Knite Support.

Namba za Fire ni (022-2151885) kwa Dar na (028-2503998) pale Mwanza jIrani na Gandhi Hall. Hebu jaribu kuzipiga hata kama hakuna hatari ya moto uone utatumia muda gani kujibiwa.

Lakini jaribu Knite Support (0754-777100) au Ultimate Security (0713-123911) utafautishe response. Jaribu hata Ambulance ya Knite Support (022-2760087).

Tayari kwa mchanganuo huo tu umeshakubali kwamba Emergency Services zimeshabinafsishwa. Na muhuri wa kubinafsishwa ni pale Ikulu ilipobidi kuwaita Knite Support kuzima moto. A private company kuingiz kwenye vyumba vya ikulu kuzima moto. Unataka wabinafsishe vipi zaidi ya hapo.

Mimi nadhani tuangalie eneo jipya hili lililobinafsishwa kuliko kujadili parastatal ambayo tayari ilishakuwa marehemu.

Tusitegemee sana trainingi ya kutumia vifaa kama fire extinguisher. Sheria inatutaka hata sisi tuwe na fire extinguisher kwenye magari yetu. Unadani ni nani hapo atakuja kwako kukukumbusha jinsi ya kuitumia. Mimi ngoja niwe muwazi. Sijui kama nina uhakika kama ninaweza kuitumia ila msinicheke kwa uwazi wangu, naamini wengi mnaweza kuwa kama mimi.

Siku moja nilipinduka na gari ikabiringita mara tatu. Bahati nzuri nina mazoea ya kuendesha huku nimeweka safety-belt. Wakati gari imepinduka tairi zikawa zinaendelea kuzunguka. Mimi nikawa nahangaika kuchomokea kwenye kioo. Nilipotolewa kwa msaada wa walioshuhudia ajali wakauliza fire extinguisher iko wapi. Hata sikukumbuka kwani nilishukuru kutoka mzima.

Hivyo kwenye hatari kama hizi si rahisi kukumbuka kukimbilia fire extinguisher na hiyo panica ikiwa ni sababu ya kwanza.

Sababu ya pili ni kwamba Matumizi ya hizo extingusher ni mara chache sana kwani hakuna mtu mwenye uzoefu wa kuepukeepuka ajali hizo kiasi kwamba ikitokea basi yeye anakimbilia kwamna extinguisher. Wenye uzoefu ni hao wenye kazi yao Fire brigade.

Ni kama vile kufunga tai. Kama ofisini mwako hawalazimishi kuvaa tai basi unaweza kujikuta hujui kufunga tai siku inapohitajika.

Nimalizie hoja zangu kwa kusema kama tunataka service nzuri basi tufutewazo kwamba tuna Fire brigade tufanyie kazi kwamba tuna private fire services. Hata ambulance ukiisikia asilimia kubwa ni kwamba ni ya private hospital na si ya Muhimbili au Bugando.

Tujifunze kubadilika wakati ni huu.
 
Back
Top Bottom