Kuna vitu niliviona kwenye mpaka wa namanga kwa mabasi yanayo safirisha abilia kutoka nairobi to dar

CHASHA FARMING

JF-Expert Member
Jun 4, 2011
7,789
8,913
Nimekuwa namanga kama wiki nzima hivi kuna vitu vilinishangaza kwa siku zote nilizo kuwa pale namanga navyo ni hivi hapa.

1. MABASI YOTE YALIYO KUWA YAKITOKEA NAIROBI NCHINI KENYA KWENDA DAR AU ARUSHA YALIKUWA YAMEJAZA ABILIA SITI ZOTE.
2. MABASI YOTE KUTOKA ARUSHA NA DAR KWENDA NAIROBI KENYA SIKU ZOTE YALIKUWA TUPU KABISANA ABILIA KAMA 13 NDANI YA BASI.

NA HII NI KWA SIKU KAMA 10 NILIZO KAA PALE NIKAJARIBU KUDODOSA WATU PALE BODA WAKANIAMBIA NDO HALI ILIVYO. WAKENYA KWA SASA WANAFURIKA TANZANIA MAMIA KWA MAELUFU, KANI KWA UPANDE WA WATANZANIA HAKUNA WANO ENDA KENYA KABISA.

NI SAIDIENI KWA HILO WAKUU.
 
Ulijaribu kudodosa wanafurika Tanzania kufanya nini? Au mambo ya utarii? Uliwauliza uraia wao? wasije kuwa ni watanzania wanarudi toka Kenya?
 
Hivi jamani wapi pameandikwa utarii ndio utalíi? Inaudhi kweli kweli
 
Mkuu ungejaribu kudodosa uraia wa hao watu kama ni watz au wakenya, lakini mimi ninavyoamini watz siku hizi tunaenda sana Kenya kwa ajili ya biashara, ushahidi ni mimi mwenyewe
 
Mkuu ungejaribu kudodosa uraia wa hao watu kama ni watz au wakenya, lakini mimi ninavyoamini watz siku hizi tunaenda sana Kenya kwa ajili ya biashara, ushahidi ni mimi mwenyewe

Mkuu kama mnaenda si m takuwa pia mnarudi? Nina maana kwamba kama amefanya utafiti kwa siku kumi basi ingekuwa mabasi yanajaa kwenda na kurudi yaani watu wanenda wanafanya transactions kisha wanarudi. Yeye anasema ameona wengi wanaingia tu hawatoki. Kwangu mimi nadhani hayo ndio matunda ya EAC. Tanzania kuna opportunities nyingi sana hasa ardhi kwa hiyo nadhani Wakenya wanakuja kuinyakua. Wana strategy hao; wanakuja wanawaoa dada zetu kisha wanenda Iringa na Morogoro kujinyakulia maeneo mwanana ya kilimo. Muda si muda tutajikuta tunaelea bila ardhi. Tunajidanganya ati tuna ardi tele kumbe watu wanaingia na hawatoki!!!
 
Inawezekana ni watanzania kutoka mikoa ya Kaskazini-Magharibi (Mwanza et al) ambao hupitia Kenya wakielekea Dar....
 
Siku hizi lami tena mpya toka DSM hadi Sirari. Wafuate nini huko?

Rafiki yangu mwenyeji wa huko, aliniambia kwamba njia ya Kati haina vivutio kulinganisha na njia ya kupitia Kenya + usalama..
 
Ni kweli wakenya wapo wengi sana huku bongo wanafundisha History na Kiswahili ndo maana bongo watoto wanafeli sana siku hizi hata arts subject
 
duuu,mkuu ni kweli kabisa kwani huku kenya watanzania tunaofanya kazi tunahesabika,tofauti na huko bongoland.
 
Rafiki yangu mwenyeji wa huko, aliniambia kwamba njia ya Kati haina vivutio kulinganisha na njia ya kupitia Kenya + usalama..

Vivutio labda Bonde la Ufa. Lakini usalama si kweli huku kwetu ni salama zaidi
 
Nimekuwa namanga kama wiki nzima hivi kuna vitu vilinishangaza kwa siku zote nilizo kuwa pale namanga navyo ni hivi hapa.1. MABASI YOTE YALIYO KUWA YAKITOKEA NAIROBI NCHINI KENYA KWENDA DAR AU ARUSHA YALIKUWA YAMEJAZA ABILIA SITI ZOTE.2. MABASI YOTE KUTOKA ARUSHA NA DAR KWENDA NAIROBI KENYA SIKU ZOTE YALIKUWA TUPU KABISANA ABILIA KAMA 13 NDANI YA BASI.NA HII NI KWA SIKU KAMA 10 NILIZO KAA PALE NIKAJARIBU KUDODOSA WATU PALE BODA WAKANIAMBIA NDO HALI ILIVYO. WAKENYA KWA SASA WANAFURIKA TANZANIA MAMIA KWA MAELUFU, KANI KWA UPANDE WA WATANZANIA HAKUNA WANO ENDA KENYA KABISA.NI SAIDIENI KWA HILO WAKUU.
Nchi yangu TANZANIA imekuwa kama shamba la bibi ndani ya jumuiya ya afrika mashariki,kila aliyekosa kazi nchini kwake au aliyekosa eneo la kilimo hukimbilia Tanzania nchi yenye virgin lands and other economic opportunities.Nimetembelea na kuishi maeneo ya mikoa ya mipakani kama vile KIGOMA,KAGERA na sehemu ambazo zina dry land entry points.Warundi,Wakongo,Wanyarwanda n.k.wamejaa sehemu mbalimbali za Tanzania na wanazidi kuingia.Tunahitaji operesheni maalumu ya kuwasaka,kuwazuia watu wasio na vibali kuingia nchini na kuwaondosha wote wasio na vibali nchini mwetu.
 
Back
Top Bottom