Kuna vigezo gani vya kusema kiswahili kimetokana na kiarabu?

Juma Bundala

Member
Mar 9, 2012
71
5
Baadhi ya wataalamu wa Lugha ya kiswahili wamejadili kuwa maneno mengi ya kiarabu kwenye kiswahili kama SHUKRUNI,AHSANTE,SHIKAMOO,NK nimaneno ya Kiarabu.Naomba kujua kama kiswahili ni Kiarabu au kimetokana na Kiarabu,je Wabantu ambo ni Msingi wa Kiswahili Pwani ya Afrika Mashariki na kati tuwaweke wapi?
 
Mkuu shule ni kireno na sio kiarabu.
Maneno tunotumia ya kisw ambayo asili yake ni kiarabu ni km: daftari, kalamu, mstari, mbatata, dawati, shubaka, sanduku, na mengine mengi. Pia tumechanganya na eng na kibantu
 
Mkuu shule ni kireno na sio kiarabu. Maneno tunotumia ya kisw ambayo asili yake ni kiarabu ni km: daftari, kalamu, mstari, mbatata, dawati, shubaka, sanduku, na mengine mengi. Pia tumechanganya na eng na kibantu
hapo sawa toa neno SHULE,je maneno uliyoyaweka nikigezo tosha cha kusema kisw ni kiarabu na siyo kibantu?
 
hapo sawa toa neno SHULE,je maneno uliyoyaweka nikigezo tosha cha kusema kisw ni kiarabu na siyo kibantu?
Sikusema km sio kibantu, ni lugha ilichonganya lugha nyengine za wenzetu, kiarabu ni mojawapo.
Kwenye kisw kuna eng, kuna kiarabu, kuna kijerumani, kuna kireno, kuna mpk kihindi.
Kihindi - pesa, chai nk
 
Kiswahili krioli ilokuwa na kusarifiwa na kuwa lugha kuu katika afrika mashariki na kati , mi siamini kama kiswahili ni kibantu moja kwa moja ,kwani kila lugha huwa na kabila lake , kiswahili haina kabila ila kuna watu ambao wengi wao wana lugha zao na pia huzungumza kiswahili, mfano Wazaramo ni waswahili , wabarawe nk.
kuna maeneo machache mno ambapo kiswahili ni lugha ya kwanza kwa wakaazi wa maeneo husika mfano Zanzibar, mombasa nk.
lugha nyingi hutohoa maneno mengi kutoka lugha nyengine...Kingereza wana maneno si chini ya 40 % ni ya kilatini. lakini kingereza sio katika lugha za kilatini kama Kitaliano,kifaransa,kihispania ama kireno

kama ndugu yangu unasoma kwa ajili ya mtihani andika kuswahili ni kibantu.
 
Wanadai ni kiArabu kwa kutumia misingi mitatu. 1;kuwa kiswahili kimechukua maneno kutoka lugha ya kiarabu hii pekee haitoshi kusema kiswahili ni kiarabu lugha sifa yake kuu lazima ichukue maneno kutoka lugha nyingine kama ilivyoelezwa hapo na wachangiaji kama ilivyochukua kutoka katika lugha nyingine za kibantu kama neno "kitivo",kutoka kipare au kisambaa."ikulu" neno la kinyamwezi ,kingoni n.k 2:neno kiswahili limetokana na kiarabu "sahil wingi swahil" hii pekee haitoshi kusema kiswahili ni kiarabu kigezo cha kutumia msamiati mmoja hakitoshi kusema ndo lugha yenyewe 3:kiarabu kimehusishwa na dini ya kislamu na kwa kuwa wakazi wengi wa pwani ya afrika mashariki ni waislamu basi wakadai kisw.ni kiarabu.dai hili si la msingi kwa kuwa hatuwezi kutumia dini kufasili kugha bali tunatumia lugha kufasili dini.na dini nyingi zimeletwa na wageni.na wakazi wa pwani ya afrika mashariki walikuwepo hata kabla kuja hao wageni na walitumia lugha yao ambayo inasadikiwa kuwa kisw. kiswahili tunaweza sema kimetokana na lugha za kibantu kwa kuwa kibantu kimeweza kuthibisha kisayansi na kihistoria dai lake
 
Muuliza swali hajapewa majibu ya kisayansi. Mimi namjibu hivi: Suala la lugha ya Kiswahili kuitwa kiarabu limeshikamanishwa na sababu za kihistoria zaidi. Kwa hiyo watoa mawazo hapo juu wanaegamia zaidi kwenye sababu za kihistoria. Ila tukiijadili lugha ya Kiswahili kwa faiwati tofauti, yaani sababu za kisemantiki, tutafikia hitimisho kwamba Kiswahili ni kibantu. Hoja kuntu zipo. Sema tu nizishushe!
 
Back
Top Bottom