Wana JF
Ni kitu cha kawaida kwa mzazi kumkumbushia mtoto/kijana wake kuhusu suala la mapenzi na mihemuko inayowapata vijana katika umri wa kubarehe au niseme katika level ya sekondari na kurudi chini. Hata vyuoni pia wazazi wanakumbushia vijana kuwa makini katika ulimwengu wa sasa uliojaa vishawishi vya kila namna na athari ya magonjwa yaliyopo. Kwa upande mwingine kwa watu wengi walioko kwenye ndoa suala la kukumbushana hili jambo la kila partner kuwa makini linachukuliwa kuwa ni jambo linalojulikana tunakuwa na assumption kuwa wenzi wetu wako makini hawahitaji kukumbushiwa. Mwisho wake ndo tunaona watu walioowa au kuolewa bado wanazidi kutembea nje ya ndoa zao kama vile hawako katika ndoa. Mifano mingi kuhusu hili inaonekana mitaani na hata huko makazini.
Kwa upande wangu naonelea, na huwa tunakumbusha na mwenzi wangu kuwa makini kwa kuchukua taadhari zote zinazowezekana katika kulinda, kuimalisha na kuboresha uhusiano wetu wa mapenzi. Na hili kwangu mimi linafanya kazi maana huwa tunaongea kinagaubaga athari ya mmoja wetu kuwa na mausiano mengine pembeni na faida ya kuwa waaminifu. Imefikia maali wengine wanaamua kula viapo tena kwa kwenda kwa mchungaji kukumbushia. Wana JF watu waendelee ku-assume ukiwa kwenye mausiano unajua athari ya kutoka nje ya ndoa bila kukumbushana? Hasa kwa wanandoa.